Onyo
Kuwasha injini kunatoa cheche.
Cheche zinaweza kuwasha gesi zilizo karibu ambazo zina uwezo wa kuwaka
moto.
Inaweza kusababisha mlipuko na moto.
• Iwapo kuna gesi asili au ya LP iliyovuja katika eneo, usiwashe injini.
• Usitumie majimaji yaliyoshinikizwa ya kuwasha kwa sababu mvuke unaweza
kuwaka moto.
Onyo
HATARI YA GESI YENYE SUMU. Eksozi ya injini ina monoksidi ya kaboni, gesi
ya sumu ambayo inaweza kukuua wewe kwa dakika chache. HUWEZI kuiona,
kuinusa wala kuionja. Hata kama huwezi kunusa mafukizo yanayotolewa,
bado unaweza kuvuta gesi ya monoksidi ya kaboni. Ukianza kuhisi mgonjwa,
kizunguzungu, au mchovu wakati unatumia bidhaa hii, nenda kwenye eneo
lenye hewa safi MARA MOJA. Mwone daktari. Huenda ukawa umeathiriwa na
sumu ya kaboni monoksidi.
• Tumia bidhaa hii NJE PEKEE mbali na madirisha, milango na matundu ili
kupunguza hatari ya gesi ya kaboni monoksidi kukusanyika na uwezekano wa
kuwa inasambazwa kuelekea maeneo ya nje.
• Sakinisha ving'ora vya kutambua uwepo wa monoksidi ya kaboni vinavyotumia
betri pamoja na hifadhi ya betri kulingana na maagizo ya mtengenezaji. Ving'ora
vya moshi haviwezi kutambua gesi ya monoksidi ya kaboni.
• USIENDESHEE bidhaa hii ndani ya nyumba, gereji, vyumba vya chini ya ardhi,
ubati, vibanda, au majengo mengine yaliyobanwa hata kama unatumia viyoyozi
ama kufungua milango na madirisha ili hewa safi iingie. Gesi ya kaboni monoksidi
inaweza kukusanyika kwa haraka katika maeneo haya na inaweza kukwama kwa
saa nyingi, hata baada ya bidhaa hii kuzimwa.
• KILA WAKATI weka bidhaa hii upande ambao upepo unatelekea na uelekeze
ekzosi ya injini mbali na maeneo yenye watu.
Onyo
Uvutaji nyuma kwa haraka wa kamba ya kianzishaji (kuvuta nyuma kwa haraka)
kutavuta mkono kuelekea kwenye injini haraka kuliko unavyoweza kuachilia.
Inaweza kupelekea mifupa kuvunjika, michubuko au kuteguka maungo.
• Wakati wa kuwasha injini, kuzuia kurudi nyuma kwa haraka, vuta kamba ya
kianzishi polepole hadi uhisi upinzani na kisha uvute haraka ili kuzuia kuvuta
nyuma kwa haraka.
• Ondoa vifaa cha nje/ mizigo yote ya injini kabla ya kuwasha injini.
• Vijenzi vya kifaa kilichounganishwa moja kwa moja kama vile, lakini visivyo tu,
bapa, mashine ya kusogeza majimaji, makapi, proketi, n.k., lazima viambatishwe
salama.
Onyo
Sehemu zinazozunguka zinaweza kugusana au kunasa mikono, miguu, nywele,
nguo, au vifuasi.
Inaweza kusababisha ukataji wa viungo wenye kiwewe au majeraha mabaya ya
ukataji ngozi.
• Endesha kifaa na vilinzi vikiwa karibu.
• Weka mikono na miguu mbali na sehemu zinazozunguka.
• Funga nywele ndefu na uondoe mapambo.
• Usivae nguo zisizokubana vizuri, kamba za nguo zinazomwayamwaya au
vipengee vinavyoweza kushikwa.
42
Onyo
Injini zinazoguruma zinatoa joto. Sehemu za injini, hususan mafla, huwa moto
zaidi.
Unaweza kuchomeka vibaya sana ukiigusa.
Uchafu unaoweza kuwaka moto, kama vile majani, nyasi, brashi n.k. unaweza
kushika moto.
• Ruhusu mafla, silinda ya injini na mapezi yapoe kabla ya kugusa.
• Ondoa uchafu uliokusanyika kutoka kwenye eneo la mafla na eneo la silinda.
• Ni ukiukaji wa Kanuni za Rasilimali za Umma za California, Sehemu ya 4442,
kutumia au kuendesha injini katika eneo linalozungukwa na msitu, lililozungukwa
na brashi, au lililo na nyasi isipokuwa mfumo wa ekzosi una kishika spaki, kama
ilivyobainishwa katika Sehemu ya 4442, kilichodumishwa katika hali fanisi ya
kufanya kazi. Mamlaka mengine ya Majimbo au shirikisho yanaweza kuwa na
sheria sawia. Wasiliana na mtengenezaji asilia wa kifaa, muuzaji rejareja, au
muuzaji ili kupata kishika spaki kilichobuniwa kwa ajili ya mfumo wa ekzosi
uliowekwa kwenye injini hii.
Onyo
Spaki zinazotokea bila kusudi zinaweza kusababisha moto au mrusho wa
stima.
Uwashaji usiokusudiwa unaweza kusababisha kunaswa, kukatwa kwa viungo
kwa kiwewe, au majeraha mabaya ya ukataji wa ngozi.
Hatari ya moto
Kabla ya kutekeleza marekebisho au ukarabati:
• Tenganisha waya ya kizibo cha cheche na iweke mbali na kizibo cha cheche.
• Tenganisha betri katika kichwa cha hasi (injini tu zenye kianzishi cha umeme).
• Tumia zana sahihi pekee.
• Usihitilafiane na springi ya kidhibiti, viungo, au viungo vingine ili kuongeza kasi ya
injini.
• Sehemu za kubadilishia ni lazima ziwe za aina sawia na ziwekwe katika eneo
sawia kama sehemu asilia. Sehemu nyingine huenda zisitfanye kazi kwa njia
sawia, zinaweza kuharibu kifaa, na inaweza kusababisha majeraha.
• Usigongegonge gurudumu la kuongeza kasi ya injini kwa nyundo au kifaa kigumu
kwa sababu gurudumu la kuongeza kasi ya injini linaweza kuvunjika wakati wa
kuendesha.
Wakati wa kujaribu cheche:
• Tumia kifaa kilichoidhinishwa cha kujaribu plagi ya spaki.
• Usikague cheche na kiziba cheche imeondolewa.
Vipengele na Vidhibiti
Vidhibiti vya Mtambo
Linganisha mfano (Kielelezo: 1, 2) na injini yako ili kujifahamisha na eneo la vipengele
na vidhibiti mbalimbali.
A.
Nambari Tambulishi za Injini Modeli - Aina - Msimbo
B.
Kiziba Cheche
C.
Kisafishaji cha Hewa
D.
Kifaa cha Kupima mafuta
E.
Kuziba ya Kumwaga Mafuta
F.
Grili ya Kuingiza Hewa
G.
Kichuja Hewa
H.
Kianzishi cha Umeme
I.
Kabureta
J.
Kichujio cha Fueli (iwapo kipo)
K.
Pampu ya Fueli (iwapo ipo)
L.
Kitoaji Mafuta cha Haraka (iwapo kipo)
M.
Kipozaji cha Fueli (iwapo kipo)
N.
Kitengo cha Kudhibiti Umeme (iwapo kipo)
BRIGGSandSTRATTON.com