Eneo la Kuendeshea Jenereta Nyepesi ili
KUPUNGUZA HATARI YA MOTO
ONYO! Joto/gesi za Eksozi zinaweza kuwasha
vitu, majengo au tangi la mafuta lililoharibika
zinazoweza kushika moto, na kusababisha kifo au
majeraha mabaya. Ni lazima jenereta ya kubebeka iwe
angalau mita 1.5 (futi 5) mbali na jengo lolote, vitu
vinavyoning'inia, miti, madirisha, milango, kuta zozote,
vichaka au mimea yenye urefu wa zaidi ya sentimita 30.5
(inchi 12). Usiweke jenereta ya kubebeka chini ya deki au
aina nyingine yoyote ya jengo ambalo litazuia hewa nyingi
kupita. Ving'ora vya moshi ni lazima viwekwe na
kudumishwa ndani ya nyumba kulingana na maagizo/
mapendekezo ya mtengenezaji. Ving'ora vya kaboni
monoksidi haviwezi kugundua moshi. Usiweke jenereta ya
kubebeka kwa njia nyingine isipokuwa ambavyo
imeonyeshwa.
Angalau mita 1.5
MAFLA
Angalau
mita 1.5
(futi 5 ).
Hatua ya 2: Oili na Mafuta
Mapendekezo ya Oili Kielelezo
Tunapendekeza matumizi ya oili Zilizoidhinishwa na
Hakikisho la Briggs & Stratton ili kupata utendakazi
bora. Oili nyingine za usafishaji zinakubalika ikiwa
zimebainishwa kwa huduma ya SF au ya juu zaidi.
Usitumie vitegemezi maalum.
Hali joto ya nje inaamua mnato sahihi wa oili kwa injini.
Tumia chati kuchagua mnato bora zaidi kwa hali joto ya
nje inayotarajiwa.
* Chini ya 40°C (40°F) matumizi ya SAE 30 yatasababisha
ugumu wa kuwasha
** Zaidi ya 27°C (80°F) matumizi ya 10W30 huenda
yakasababisha matumizi zaidi ya oili. Kagua kiwango cha oili
mara nyingi zaidi.
Kukagua/Kuongeza Oili ya Injinil
Kiwango cha oili kinafaa kukaguliwa kabla ya kila
matumizi au angalau kila baada ya saa 8 za uendeshaji.
Dumisha kiwango cha oili.
1. Hakik isha jenereta iko kwenye eneo tambarare.
2. Safisha eneo linalozingira tundu la kujazia oili (1, J)
na uondoe kifuniko cha tundu la kujazia oili/kifaa cha
kupima oili.
3. Hakikisha oili imefikia alama inayoonyesha Imejaa (Full)
(5, A) kwenye kifaa cha kupima oili.
4. Ikiwa inahitajika, weka oili polepole ndani ya tundu la
kujazia oili hadi ifikie alama inayoonyesha Imejaa (Full)
kwenye kifaa cha kupima oili. Usijaze kupita kiasi.
5. Funika na ukaze kifuniko cha tundu la kujazia oili/
kifaa cha kupima oili.
6
(futi 5 ).
4
Kielelezo
1 5
ILANI Usijaribu kuwasha au kuanzisha injini
kabla haijafanyiwa huduma vizuri kwa kutumia oili
inayopendekezwa. Hii inaweza kusababisha injini
kuharibika.
TAHADHARI Epuka oili ya mot na fueli
kugusana na ngozi kwa muda mrefu au mara
nyingi. Oili ya mota iliyotumika imeonekana
kusababisha saratani ya ngozi katika maabara fulani za
wanyama. Safisha kwa kina maeneo yaliyoathirika
ukitumia sabuni na maji.
WEKA MBALI WA WATOTO. USICHAFUE.
TUMIA RASILIMALI VIZURI. REJESHA OILI
ILIYOTUMIKA KWENYE VITUO VYA
KUKUSANYA.
Ongeza Mafuta Kielelezo
Mafuta ni lazima yatimize mahitaji haya:
• Petroli safi, freshi, isiyo na risasi (unleaded) na iliyo
na angalau okteni 87/87 AKI ((91 RON).
• Petroli iliyo na hadi ethanoli 10% inakubalika.
ILANI Usichanganye oili kwenye petroli au kurekebisha
injini ili itumie mafuta mbadala. Usitumie petroli ambayo
haijaidhinishwa kama vile E15 na E85. Utumizi wa
mafuta ambayo hayajaidhinishwa kunaweza kusababisha
uharibifu kwenye jenereta na kubatilisha hakikisho.
Tazama Mwinuko wa Juu kwa mita 1,524 (futi 5,000 ft.)
na zaidi.
ONYO! Mafuta na mivuke yake
yanaweza kuwaka moto na kulipuka na
kusababisha kuchomeka, moto au
mlipuko na kupelekea kifo au majeraha mabaya.
Usiongeze mafuta wakati jenereta inatumika. Zima injini
na uwache injini ipoe kwa angalau dakika 2 kabla ya
kuondoa kifuniko cha mafuta. Jaza tangi la mafuta ukiwa
nje ya nyumba. Usimwage mafuta nje ya tangi. Weka
mafuta mbali na spaki, moto ulio wazi, taa za gesi, joto,
na vyanzo vingine vya mwako. Kagua tundu, tangi,
kifuniko kama kuna nyufa na uvujaji. Badilisha kama
itahitajika. Usiwashe sigara wala usivute sigara. Usitumie
maji kuzima moto kwenye jenereta. Tumia tu kizima moto
kilichotengenezwa kuzima moto kirahisi na mifumo ya
kiumeme kama kizima moto cha unga. Fuata maagizo
yaliyotolewa na mtengenezaji wa kizima moto kabla ya
matumizi. Jenereta hii haipaswi kutumiwa katika
mazingira yanayoweza kushika moto kirahisi.
1. Ondoa polepole kifuniko cha mafuta ili kupunguza
shinikizo ndani ya tangi.
2. Polepole ongeza mafuta ya yasiyo na risasi (A) ili
kutia mafuta kwenye tangi (B). Kuwa mwangalifu
usijaze hadi juu ya ukingo (C). Hii inawacha nafasi
ya kutosha kwa ajili ya upanuzi wa mafuta.
3. Rudisha kifuniko cha tangi la mafuta na uruhusu
mafuta yoyote yaliyomwagika kuyeyuka kabla ya
kuwasha injini.
Mwinuko wa Juu
Katika mwinuko zaidi ya mita 1524 (futi 5,000), kiwango
cha chini cha okteni 85//85 AKI (89 RON) cha petroli
kinakubalika. Ili uendelee kuzingatia utoaji moshi,
marekebisho ya mwinuko wa juu yanahitajika. Uendeshaji
bila marekebisho haya unaweza kusababisha kupunguka
kwa utendakazi, matumizi ya mafuta kuongezeka, na
mafukizo kuongezeka.
6
BRIGGSandSTRATTON.COM