2. Ingiza kamba ya nguvu za umeme (1,E) kwenye
mzunguko wa umeme uliotengewa uendeshaji ule (8)
ulio na kipimo cha 220 -240 volts AC kwa 10 Amps
ambayo imesakinishwa vizuri kabisa kulingana na sheria
na kanuni za ndani. Mzunguko ule wa umeme haupaswi
kushughulikia matumizi mengine ya kiumeme.
3. Bonyeza kitufe cha RESET yaani weka upya (7,C).
Mwanga wa kiashiria (7,B) unapaswa kuwa ON.
ILANI Mwanga wa kiashiria lazima uwe unawaka yaani
ON ili shinikizo-kisafishaji kile kifanye kazi.
4. Bonyeza kitufe cha TEST yaani jaribio(7,A). Mwanga wa
kuashiria (7,B) unapaswa kuwa OFF.
5. Bonyeza kitufe cha RESET yaani weka upya (7,C).
Mwanga wa kiashiria (7,B) unapaswa kuwa ON.
ONYO! Hatari ya mshtuko wa umeme. PRCD
isiyofanya kazi huenda ikasababisha kifo au jeraha la
kimwili. Iwapo mwanga wa kuashiria haubakii kuwa
ON baada ya jaribio na uwekaji upya, usitumie PRCD.
6. Bonyeza swichi kuu iwe katika hali ya ON (I) (9,B).
7. Elekeza bunduki-kiachilia kwenye eneo salama, bonyeza
kitufe kinachofunga kikabaji kisha ufinye kikabaji.
Mtambo/injini ile itawaka na kisha kuzima kwa vile kikabaji
cha kifaa-kifukizi kitafinyika chini na kuachiliwa.
Ncha za Kufukizia
Turbo ile huzungusha maji kwa kasi sana ili kusafisha vizuri
kabisa. Ncha nyeusi ya kufukizia ni ya matumizi ya kawaida ya
sabuni. Ncha manjano ya kufukizia ni ya matumizi ya kawaida
ya kusuuzia na shinikizo la juu. Ncha nyekundu ya kufukizia ni ya
usafishaji mzuri zaidi.
Ncha za Matumizi
• Kwa usafishaji mzuri zaidi, weka ncha ya kufukizia kutoka
20 hadi 61 cm. (8 hadi 24 in.) mbali na eneo la kufulia.
• Ukiweka ncha ya kufukizia iwe karibu sana, hasa ukitumia
ncha ya kufukizia yenye shinikizo la juu, huenda ukaharibu
eneo linalosafishwa.
• USIKARIBIE kupita 15 cm. (6 in.) unaposafisha matairi.
Uwekaji Sabuni
Picha ya
ONYO! Kemikali huweza kusababisha michomo
isababishayo vifo au jeraha sugu. USITUMIE
kemikali iwezayo kuchoma kwenye shinikizo-
kisafishaji. Tumia sabuni salama kwa shinikizo-kisafishaji
PEKEE. Fuata maagizo ya mtengenezaji.
Ili uweke sabuni, fuata hatua zifuatazo:
1. Ondoa mtungi wa sabuni na kifuniko (1G,10). Uujazie
sabuni ya maji maji au povu.
2. Rejesha kifuniko na mtungi wa sabuni.
3. Sakinisha ncha nyeusi ya kufukizia.
6
6
1
10
NOTICE
Sabuni haiwezi kutumika na turbo, wala ncha
nyekundu au manjano ya kufukizia.
4. Paka sabuni kwenye eneo lililokauka, ukianza na
sehemu za chini za eneo linalofaa kusafishwa na
ufanye kazi ukielekea sehemu za juu, hakikisha
mipako yako ni ndefu, imesawazika na inaambatana.
5. Acha sabuni "ilowe" kulingana na maagizo ya
mtengenezaji kabla ya kusafisha na kussuza.
Usuuzaji Ukitumia Shinikizo-Kisafishaji Picha ya
1. Ondoa ncha nyeusi ya kufukizia kwenye kijiti-kipini (B)
na usakinishe ncha manjano au nyekundu ya kufukizia.
ONYO! Nyweo linalotokana na kifaa-kifukizi huenda
likasababisha uanguke na kusababisha kifo au jeraha
sugu. Endesha shinikizo-kisafishaji kwenye eneo
thabiti. Kuwa mwangalifu kabisa iwapo ni lazima utumie
shinikizo-kisafishaji kile unapokuwa ngazini au kwenye eneo
lingine la aina ile. Shikilia kifaa-kifukizi kwa mikono yote miwili
unapotumia fukizo lenye shinikizo la juu ili kuzuia jeraha wakati
nyweo la kifaa-kifukizi kimetokea.
2. Weka fukizo lenye shinikizo la juu kwenye eneo
ndogo ili uchunguzie uharibifu wa eneo. Ikiwa hakuna
uharibifu wowote, endelea kusuuza.
3. Anza na sehemu ya juu inayopaswa kusuuzwa, na
uendelee chini ukiweka mipako kama ile ile uliyotumia
kusafishia.
Kuzima Shinikizo-Kisafishaji
1. Achilia kikabaji kifaa-kifukizi.
2. Bonyeza swichi kuu (1,L) iwe katika hali ya OFF (0) (9,A).
NOTICE Uachiliaji kikabaji kile utazima mtambo/injini lakini
hautazima nguvu za umeme zinazosambazwa kwenye kifaa.
3. Funga asili ya maji.
4. DAIMA elekeza kifaa-kifukizi kile kwenye eneo salama,
bonyeza kitufe kifungacho kikabaji, na ufinye kikabaji
kile ili kuachilia shinikizo lililojazana kifaani mle.
ONYO! Maji yenye shinikizo la juu ambayo kifaa
hiki hutoa huweza kukata ngozi na tishu zake za
ndani, na kusababisha jeraha sugu na ukataji wa
sehemu za mwili. Hakikisha mpira wa maji wenye shinikizo
la juu umeunganishwa kwenye pampu na kifaa-kifukizi
wakati mfumo ule umeshinikizwa. USIRUHUSU WATOTO
wachezee au kuendesha shinikizo-kisafishaji hiki. DAIMA
elekeza kifaa-kifukizi kwenye eneo salama, finya kikabaji
kifaa-kifukizi ili uachilie shinikizo la juu, wakati wowote
unapozima shinikizo-kisafishaji.
5. Tenga kizibo cha PRCD (1,E) umemeni, na uhifadhi
kamba ya nguvu za umeme.
6. Hifadhi mpira wa shinikizo la juu (1,J) chini ya mtungi wa maji.
7. Hifadhi kifaa kifukizi (1,A) na kijiti-kipini cha plastiki
(1,M) kwenye vishikiliaji. Hifadhi ncha za kufukizia
(1,C) kwenye kishikiliaji kwenye kijiti-kipini cha chuma.
Angalia Sifa na Vidhibiti.
1
Picha ya
1 9
BRIGGSandSTRATTON.COM
BRIGGSandSTRATTON.COM