Ongeza Mafuta
ONYO
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Unapoongeza mafuta
•
Zima injini. Kabla ya kufunua kifuniko, subiri angalau dakika mbili (2) ili
kuhakikisha injini imepoa.
•
Jaza tangi la mafuta ukiwa nje au katika eneo lenye hewa nyingi safi.
•
Usiweke mafuta mengi kupita kiasi kwenye tangi. Kwa ajili ya uvukizi wa mafuta,
usijaze hadi juu ya chini ya shingo la tangi la mafuta.
•
Weka mafuta mbali na spaki, moto ulio wazi, taa za gesi, joto, na vyanzo vingine
vya mwako.
•
Mara kwa mara kagua tundu la tangi, tangi la mafuta, kifuniko cha mafuta, na
mirija kama kuna nyufa na uvujaji. Badilisha sehemu zilizoharibika.
•
Mafuta yakimwagika, subiri mpaka yakauke kabla ya kuwasha injini.
1.
Safisha kifuniko cha mafuta kutokana na uchafu na vifusi. Ondoa kifuniko cha fueli.
2.
Jaza tangi la mafuta (A, Kielelezo 16) kwa mafuta. Kwa ajili ya uvukizi wa mafuta,
usijaze zaidi ya chini mwa shingo ya tangi la mafuta (B).
3.
Weka kifuniko cha mafuta.
Washa Injini
ONYO
Uvutaji nyuma wa haraka wa kamba ya kianzishaji (kuvuta nyuma kwa haraka)
kutavuta mkono wako kuelekea kwenye injini haraka kuliko unavyoweza kuachilia.
Kunaweza kusababisha mifupa kuvunjika, michubuko amu maungo kuteguka.
•
Ili kuzuia kuvuta nyuma kwa haraka wakati wa kuwasha injini, vuta kamba ya
kianzishaji polepole hadi uhisi upinzani na kisha uvute haraka.
•
kabla ya kuwasha injini, ondoa vifaa vyote vya nje/mizigo yote ya injini.
•
Hakikisha kwamba vijenzi vya kifaa kilichounganishwa moja kwa moja kama
vile, lakini sio tu, bapa, mashine ya kusogeza majimaji, makapi, na proketi,
vimeambatishwe salama.
ONYO
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Unapowasha injini
•
Hakikisha kwamba plagi ya spaki, mafla, kifuniko cha mafuta, na kisafishaji
hewa (iwapo kipo) vimefungwa vizuri.
•
Usishtue injini wakati plagi ya spaki imeondolewa.
•
Ikiwa injini imefurika, choki (iwapo ipo) imewekwa kwenye eneo la
IMEFUNGULIWA au ENDESHA. Songeza kidhibiti injini (iwapo kipo) hadi
kwenye eneo la HARAKA na ushtue hadi injini iwake.
•
Iwapo kuna gesi asili au ya LP iliyovuja katika eneo hilo, usiwashe injini.
•
Kwa sababu mvuke unaweza kuwaka moto, usitumie firigiji zilizoshinikizwa za
kuwasha.
ONYO
HATARI YA GESI YENYE SUMU. Eksozi ya injini ina kaboni monoksidi, gesi ya
sumu ambayo inaweza kukuua kwa dakika chache. Ingawa hauwezi kunusa
mafukizo yanayotolewa, bado unaweza kuvuta gesi hatari ya monoksidi ya
kaboni. Ukihisi mgonjwa, kizunguzungu, au mchovu unapotumia bidhaa hii,
nenda kwenye eneo lenye hewa safi MARA MOJA. Mwone daktari. Huenda ukawa
umeathiriwa na sumu ya kaboni monoksidi.
•
Gesi ya kaboni monoksidi inaweza kujikusanya katika maeneno yenye watu. Ili
kupunguza hatari ya gesi ya kaboni monoksidi, tumia bidhaa hii TU nje na mbali
na madirisha, milango na matundu.
•
Sakinisha ving'ora vya kutambua uwepo wa kaboni monoksidi vinavyotumia betri
pamoja na hifadhi ya betri kama ilivyobainishwa na maagizo ya mtengenezaji.
Ving'ora vya moshi haviwezi kutambua gesi ya kaboni monoksidi.
•
USIENDESHEE bidhaa hii ndani ya nyumba, gereji, vyumba vya chini ya ardhi,
ubati, vibanda, au majengo mengine yaliyobanwa hata kama unatumia viyoyozi
ama kufungua milango na madirisha ili hewa safi iingie. Baada ya kuendesha
bidhaa hii, gesi ya kaboni monoksidi inaweza kukusanyika kwa haraka katika
maeneo haya na inaweza kukwama kwa saa kadhaa.
•
KILA WAKATI weka bidhaa hii upande ambao upepo unaelekea na uelekeze
ekzosi ya injini mbali na maeneo yenye watu.
NOTISI
Injini hii ililetwa kutoka Briggs & Stratton bila oili. Watengenezaji au wauzaji vifaa
huenda waliongeza oili kwenye injini. Kabla ya kuwasha injini kwa mara ya kwanza,
hakikisha umekagua kiwango cha oili ni sahihi. Ongeza oili kama ilivyobainishwa na
maagizo kwenye mwongozo huu. Ukiwasha injini bila oili, injini itaharibika na haiwezi
kukarabatiwa chini ya waranti.
KUMBUKA: Kifaa chako kinaweza kuwa na vidhibiti vya mbali. Rejelea mwongozo wa
kifaa ili utambue mahali ambapo vidhibiti vya mbali viko na jinsi ya kuvitumia.
1.
Kagua oili ya injini. Rejelea sehemu ya Kagua Kiwango cha Oili.
2.
Hakikisha kwamba vidhibiti vya uendeshaji kifaa, iwapo vipo, vimezimwa.
3.
Sogeza wenzo wa kidhibiti injini / TransportGuard
hadi kwenye eneo linaloonyesha HARAKA au ENDESHA. Endesha injini katika
eneo hilo la HARAKA au ENDESHA.
4.
Sogeza kidhibiti choki (B, Kielelezo 17) hadi kwenye eneo linaloonyesha
IMEFUNGWA.
Kwa kawaida choki haihitajiki wakati wa kuwasha upya injini iliyochemka.
5.
Kianzishaji Upya, iwapo ipo: Kwa uthabiti shikilia kishikio cha kamba ya
kianzishaji (C, Kielelezo 17). Vuta kishikio cha kamba ya kianzishaji polepole hadi
uhisi ugumu, kisha vuta kwa haraka.
ONYO
Uvutaji nyuma wa haraka wa kamba ya kianzishaji (kuvuta nyuma kwa haraka)
kutavuta mkono wako kuelekea kwenye injini haraka kuliko unavyoweza kuachilia.
Kunaweza kusababisha mifupa kuvunjika, michubuko amu maungo kuteguka.
•
Ili kuzuia kuvuta nyuma kwa haraka wakati wa kuwasha injini, vuta kamba ya
kianzishaji polepole hadi uhisi upinzani na kisha uvute haraka.
•
kabla ya kuwasha injini, ondoa vifaa vyote vya nje/mizigo yote ya injini.
•
Hakikisha kwamba vijenzi vya kifaa kilichounganishwa moja kwa moja kama
vile, lakini sio tu, bapa, mashine ya kusogeza majimaji, makapi, na proketi,
vimeambatishwe salama.
6.
Kianzishi cha Nishati, iwapo kipo: Geuza swichi ya kianzishaji cha umeme (D,
Kielelezo 17) hadi kwenye eneo linaloonyesha WASHA.
NOTISI
Ili kurefusha maisha ya kianzishaji, tumia misururu mifupi ya kuanzisha (upeo wa
sekunde tano). Subiri dakika moja kati ya mizunguko ya kuanzisha.
7.
Injini inapochemka, sogeza kidhibiti cha choki (B, Kilelelezo 17) hadi kwenye eneo
linaloonyesha FUNGUA.
Injini ikikosa kuwasha baada ya majaribio 2 au 3, wasiliana na muuzaji wako wa ndani
au nenda kwenye vanguardpower.com au upige simu kwa nambari 1-800-999-9333
(nchini Marekani).
Zima Injini
ONYO
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
•
Usikabe kabureta (iwapo ipo) ili kusimamisha injini.
®
Kidhibiti Injini / Transport Guard
: Sogeza kidhibiti injini / TransportGuard
Kielelezo 18) hadi kwenye eneo linaloonyesha ZIMA au SIMAMA.
KUMBUKA: Wakati kidhibiti injini / TransportGuard
ZIMA au SIMAMA, vali ya mafuta itakuwa katika eneo linaloonyesha ZIMA. Kila wakati
sogeza kidhibiti injini / TransportGuard
SIMAMA wakati unaposafirisha kifaa.
KUMBUKA: Ufunguo (D, Kielelezo 18) hauzimi injini. Ufunguo unawasha Tu injini. Kila
wakati ondoa ufunguo (D), na uuweke katika mahali salama mbali na watoto.
Udumishaji
Maelezo ya Udumishaji
ONYO
Wakati wa huduma ya udumisha ikiwa ni muhimu kuinamisha kifaa, ikiwa tangi la
mafuta limeshikana na injini, hakikikisha kwamba ni tupu na upande wa plagi ya spaki
uko juu. Ikiwa tangi la mafuta si tupu, mafuta yanaweza kuvuja na kusababisha moto au
mlipuko. Ikiwa injini imeinama katika mkao tofauti, haitaguruma kwa urahisi kwa sababu
ya kuchafuka kwa chujio la hewa au plagi ya spaki kwa oili au mafuta.
®
(A, Kielelezo 17), iwapo upo,
®
(A, Kielelezo 18) ipo katika eneo la
®
hadi kwenye eneo linaloonyesha ZIMA au
®
(A,
59