2.
Injini ina matundu mawili ya kujazia oili (C, G, Kielelezo 23). Polepole weka oili
kwenye tundu moja la kujazia oili kwenye injini (C, G). Usiongoze oili nyingi kupita
kiasi. Subiri dakika moja, na kisha ukague kiwango cha oili.
3.
Weka kifaa cha kupima kiwango cha oili.
4.
Ondoa kifaa cha kupima oili na ukague kiwango cha oili. Kiwango sahihi cha oili
kiko juu ya alama inayoashiria kujaa (B, Kielelezo ) kwenye kifaa cha kupima
kiwango cha oili. Tazama sehemu ya Kagua Kiwango cha Oili.
5.
Weka na ukaze tena kifaa cha kupima kiwango cha oili.
6.
Unganisha waya wa plagi ya spaki kwenye plagi ya/za spaki. Tazama sehemu ya
Kuondoa Oili.
Kufanya Udumishaji kwenye Chujio la Hewa
ONYO
Mvuke wa mafuta unaweza kushika moto na kulipuka kw aharaka sana. Moto au
mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
•
Usiwashe na kuendesha injini kamwe wakati kifaa cha usafishaji hewa (iwapo
kipo) au chujio la hewa (iwapolipo) kimeondolewa.
NOTISI
Usitumie hewa au maji yaliyoshinikizwa kusafishia chujio. Hewa iliyoshinikizwa inaweza
kuharibu chujio na vioevu vitayeyusha chujio.
Tazama Ratiba ya Udumishaji ili kujua mahitaji ya huduma.
Miundo tofauti itatumia vichujio vya sifongo au karatasi. Baadhi ya miundo pia iinaweza
kuwa na kisafishaji cha mwanzo cha hiari ambacho kinaweza kusafishwa na kutumiwa
tena. Linganisha mifano kwenye mwongozo na aina iliyosakinishwa kwenye injini yako
na ushughulikie kama ifuatavyo.
Kichujio cha Hewa cha Karatasi
1.
Legeza sehemu za kufunga (C, Kielelezo 24).
2.
Ondoa kifuniko (A, Kielelezo 24) na chujio (B).
3.
Ili kulegeza uchafu, kwa utaratibu gongesha chujio (B, Kielelezo 24) kwenye eneo
gumu. Ikiwa chujio ni chafu, badilisha kwa chujio jipya.
4.
Weka chujio (B, Kielelezo 24).
5.
Weka kifuniko (A, Kielelezo 24) na ufunge vizuri ukitumia sehemu za kufunga (C).
Hakikisha sehemu za kufunga zimekazwa kabisa.
Chujio la Hewa la Karatasi - Nyembamba
1.
Sogeza wenzo (A, Kielelezo 25) ili kufungua kifuniko (C).
2.
Sogeza sehemu za kufunga (B, Kielelezo 25) ili kuondoa kifuniko (C).
3.
Ondoa chujio (D, Kielelezo 25).
4.
Ili kulegeza uchafu, kwa utaratibu gongesha chujio (D, Kielelezo 25) kwenye eneo
gumu. Ikiwa chujio ni chafu, badilisha kwa chujio jipya.
5.
Sakinisha chujio (D, Kielelezo 25).
6.
Sakinisha kifuniko (C, Kielelezo 25). Songeza wenzo (A) hadi eneo la kufunga.
KUMBUKA: Kagua jinsi kifuniko cha sifongo (E, Kielelezo 25) kilivyotoshea. Hakikisha
kwamba kifuniko cha sifongo kimeingia vizuri mahali pake (F).
Kufanyia Huduma Mfumo wa Mafuta
ONYO
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
•
Weka mafuta mbali na spaki, moto ulio wazi, taa za gesi, joto, na vyanzo vingine
vya mwako.
•
Mara kwa mara kagua tundu la tangi, tangi la mafuta, kifuniko cha mafuta, na
mirija kama kuna nyufa na uvujaji. Badilisha sehemu zilizoharibika.
•
Kabla ya kusafisha au kubadilisha kichujio cha mafuta, mwaga mafuta kutoka
kwa tangi ya mafuta au funga vali ya kufungia mafuta.
•
Mafuta yakimwagika, subiri mpaka yakauke kabla ya kuwasha injini.
•
Sehemu za kubadilishia ni lazima ziwe za aina sawa na ziwekwe katika eneo
sawa kama sehemu asilia. Sehemu nyingine huenda zinaweza kuharibu kifaa au
kusababisha majeraha.
Chujio la Mafuta, iwapo lipo
1.
Ondoa kifuniko cha mafuta (A, Kielelezo 26).
2.
Ondoa chujio la mafuta (B, Kielelezo 26).
3.
Iwapo chujio msingi la mafuta ni chafu, lisafishe au ulibadilishe. Ukibadilisha chujio
msingi la mafuta, hakikisha umetumia chujio msingi la mafuta ambalo si ghushi.
Kufanyia Huduma Mfumo wa Kupoesha
ONYO
Wakati wa uendeshaji, injini na mafla zinakuwa moto. Ukigusa injini moto,
unaweza kuchomeka.
Uchafu unaoweza kuwaka moto, kama vile majani, nyasi na brashi, vinaweza
kushika moto.
•
Kabla ya kugusa injini au mafla, zima injini na usubiri dakika mbili (2). Hakikisha
kwamba injini na mafla ni salama kugusa.
•
Ondoa uchafu kwenye mafla na injini.
NOTISI
Usitumie maji kusafisha injini. Maji yanaweza kuchafua mfumo wa mafuta. Tumia brashi
au kitambaa kavu kusafisha injini.
Hii ni injini inayopoeshwa kwa kutumia hewa. Uchafu au vifusi vinaweza kuzuia
mtiririko wa hewa na kusababisha injini kuwa moto sana na hii kupelekea utendakazi
usioridhisha na injini kuwa na maisha mafupi.
1.
Tumia brashi au kitambaa kavu kuondoa vifusi kwenye grili ya kuingiza hewa.
2.
Weka viunganishaji, springi na vidhibiti vikiwa safi.
3.
Weka ene lililo karibu na nyuma ya mafla, iwapo ipo, bila uchafu wowote unaoweza
kuwaka moto.
4.
Hakikisha mapezi ya kupoesha oili, ikiwa yapo, yakiwa safi.
Baada ya kipindi cha muda, mapezi ya kupoesha silinda yanaweza kukusanya vifusi
na kusababisha injini kuwa moto kupita kiasi. Uchafu huu hauwezi kuondolewa
bila kutenganisha sehemu kadhaa za injini. Ruhusu Mtoa Huduma Aliyeidhinishwa
wa Briggs & Stratton kukagua na kusafisha mfumo wa kupoesha hewa kama
ilivyopendekezwa kwenye Ratiba ya Udumishaji.
Hifadhi
Mfumo wa Mafuta
Rejelea Kielelezo: 27.
Weka injini bila kuinama (mkao wa kawaida wa kuendesha). Jaza tangi la mafuta (A,
Kielelezo 27) kwa mafuta. Ili kuruhusu uvukizi wa mafuta, usijaze kuzidi shingo ya tangi
la mafuta (B).
Ikiwa petroli ndani ya injini haijatibiwa kwa kiimarishaji mafuta, ni lazima imwagwe
kwenye kontena iliyoidhinishwa. Endesha injini hadi isimame kutokana na ukosefu wa
mafuta. Matumizi ya kiimarishaji mafuta kwenye kontena ya uhifadhi yanapendekezwa ili
kuzuia mafuta kuganda.
Oili ya Injini
Wakati injini bado ina joto, badilisha oili ya injini. Rejelea sehemu ya Kubadilisha Oili
ya Injini.
Kutatua Matatizo
Usaidizi
Ili kupata usaidizi, wasiliana na muuzaji wa karibu au nenda
kwenyeBRIGGSandSTRATTON.COM au piga simu kwa nambari 1-800-444-7774
(nchini Marekani).
Maelezo
Maelezo na Sehemu za Udumishaji
Muundo: 25V000
Unyonyaji Mafuta
Shimo
Mpigo
Bolti ya Bano la Kuweka Kebo
Skrubu ya Kufunga Waya
Kiwango cha Oili
Pengo la Plagi ya Spaki
Mkufu wa Plagi ya Spaki
Pengo la Hewa
Mwanya wa Vali ya Kuingiza Hewa
Mwanya wa Vali ya Ekzosi
Nguvu ya injini itapungua kwa 3.5% kwa kila futi 1,000 (mita 300) juu ya kiwango
cha bahari na 1% kwa kila 10°F (5.6°C) juu ya 77°F (25°C). Injini itaendesha kwa
kuridhisha katika pembe ya hadi 30°. Rejelea mwongozo wa mwendeshaji ili kufahamu
viwango salama vinavyoruhusiwa kwenye miteremko.
24.898 ci (408 cc)
3.465 in (88 mm)
2.638 in (67 mm)
30 lb-in (3,4 Nm)
25 lb-in (2,8 Nm)
28-32 oz (,82 - ,95 L)
.030 in (,76 mm)
170 lb-in (170 Nm)
.010 - .014 in (,25 - ,35 mm)
.004 - .006 in (,10 - ,15 mm)
.006 - .008 in (,15 - ,20 mm)
61