mwinuko wa juu. Oparesheni wa injini katika mwinuko wa chini ya futi 2,500 (mita 762)
na marekebisho ya mwinuko wa juu hayapendekezwi.
Kwa injini za Uinjizaji wa Fueli wa Kielektriki (EFI), hakuna marekebisho ya mwinuko wa
juu yanahitajika.
Ongeza Mafuta
Tazama Kelelezo: 8
Onyo
Fueli na mvuke wako unawaka na kulipuka haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka vikali au kifo.
Wakati wa kuongeza fueli
• Zima injini na uruhusu injini kupoa angalau dakika 2 kabla ya kuondoa kifuniko cha
fueli.
• Jaza tangi la fueli nje au katika eneo linaruhusu hewa kuingia vizuri.
• Usijaze tangi la fueli kupita kiasi. Ili kuruhusu upanukaji wa fueli, usijaze kupita
chini ya shingo la tangi la fueli.
• Hifadhi fueli mbali na cheche, miale iliyo wazi, taa za mwongozo, joto na vyanzo
vingine vya uwakaji.
• Angalia tundu, tangi, kifuniko na kurekebisha mara kwa mara kwa nyufa na uvujaji.
Badilisha ikiwezekana.
• Iwapo fueli itamwagika, subiri hadi ivukize kabla ya kuwasha injini.
1.
Safisha kifuniko cha fueli kutokana na uchafu. Ondoa kifuniko cha fueli.
2.
Jaza tangi la fueli kwa fueli (A, Kielelezo 8). Ili kuruhusu upanuzi wa fueli, usijaze
juu ya chini ya shingo la tangi la fueli (B).
3.
Sakinisha upya kifuniko cha fueli.
Washa na Uzime Injini
Tazama Kelelezo: 9, 10
Washa Injini
Onyo
Uvutaji nyuma wa haraka wa kamba ya kianzishi (kuvuta nyuma kwa haraka)
kutavuta mkono kuelekea kwenye injini haraka kuliko unavyoweza kuachilia.
Mifupa ilivyovunjika, kuvunjika kwa mifupa mikuuu, michubuko, mishtuko
inaweza kutokea.
• Wakati wa kuwasha injini, vuta kamba ya kianzishi polepole hadi uhisi upinzani na
kisha vuta haraka ili kuzuia kurudi nyuma kwa haraka.
Onyo
Fueli na mvuke wake unawaka na kulipuka hara sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka vikali au kifo.
Wakati wa Kuwasha Injini
• Hakikisha kuziba cheche, mafla, kifuniko cha fueli na kisafishaji cha hewa (iwapo
vipo) viko sawa na salama.
• Usiwashe injini wakati kuziba cheche kimeondolewa.
• Iwapo injini inamwaga mafuta, weka choki (iwapo ipo) kwenye eneo la FUNGUA
au ENDESHA, sogeza transfoma ndogo (iwapo ipo) kwenye eneo la HARAKA na
uwashe injini hadi ianze kuenda.
Onyo
MADHARA YA GESI YENYE SUMU. Eneo la injini la kutolea moshi lina
monoksidi kaboni, gesi yenye sumu ambayo inaweza kuua kwa dakika. HUWEZI
kuiona, kuinusa au kuionja. Hata kama huwezi kunusa mafusho yanayotolewa,
unaweza kufikia gesi ya monoksidi kaboni. Iwapo utaanza kuhisi, mgonjwa,
kizunguzungu, au mchovu wakati unatumia bidhaa hii, izime na uende eneo
lenye hewa safi MARA MOJA. Mwone Daktari. Unaweza kuwa na sumu ya
monoksidi kaboni.
• Endesha bidhaa hii nje TU mbali na madirisha, milango na tundu za kuingiza hewa
ili kupunguza hatari za gesi ya monoksidi kaboni kutokana na kukusanyika na
kuweza kuelekea katika maeneo yaliyo na watu.
• Sakinisha ving'ora vya kutambua uwepo wa monoksidi kaboni vinavyoendeshwa
na betri pamoja na chelezo za betri kulingana na maelekezo ya mtengenezaji.
Ving'ora vya moshi haviwezi kutambua gesi ya monoksidi kaboni.
• USIENDESHE bidhaa hii nyumbani, karakarani, sehemu ya chini ya majengo,
maeneo ya kutembelea kwenye majengo, vivulini, au maeneo mengine
yaliyofunikwa nusu hata kama unatumia feni au milango na madirisha
yaliyofunguka kuruhusu hewa kuingia. Monoksidi kaboni inaweza kukusanyika
kwa haraka katika maeneo haya na inaweza kukwama kwa saa, hata baada ya
bidhaa hii kuzimwa.
• KILA MARA weka bidhaa hii katika eneo lenye upepo na uelekeze eneo la kutolea
moshi la injini mbali na maeneo yaliyo na watu.
Notisi
Injini hii ililetwa kutoka Briggs & Stratton bila mafuta. Kabla uweze kuwasha
injini, hakikisha umeongeza mafuta kulingana na maelekezo kwenye mwongozo
huu. Iwapo utawasha injini bila mafuta, itaharibika hadi kushindwa kukarabatiwa na
hutafidiwa chini ya udhamini huu.
Kumbuka: Kifaa kinaweza kuwa na vidhibiti mbali. Tazama mwongozo wa kifaa kwa
utambuzi na uendeshaji wa vidhibiti mbali.
1.
Angalia mafuta ya injini. Tazama sehemu Kuangalia Kiwango cha Mafuta.
2.
Hakikisha vidhibiti vya kiendeshaji cha kifaa, iwapo vipo, vimetenganishwa.
3.
Sukuma swichi ya kusimamisha (A, Kielelezo 9, 10) iwapo ipo, katika eneo la
washa.
4.
Sogeza kidhibiti cha transfoma ndogo (B, Kielelezo 9), iwapo kipo, katika eneo la
haraka. Endesha injini ikiwa katika eneo la haraka.
5.
Sogeza kidhibiti cha choki (C, Kielelezo 9) kwenye eneo la choki.
Kumbuka: Kwa kawaida choki haihitajiki wakati wa kuwasha injini iliyochemka.
6.
Sogeza kizima fueli (D, Kielelezo 9), iwapo kipo, kwenye eneo la kufungua.
7.
Vingirisha Anza, iwapo ipo: Kwa uthabiti shikilia kishikilio cha kamba ya
kianzishi (E, Kielelezo 9). Vuta kamba ya kianzishi polepole hadi uhisi upinzani,
kisha vuta haraka.
Onyo
Uvutaji nyuma wa haraka wa kamba ya kianzishi (kuvuta nyuma kwa haraka)
kutavuta mkono kuelekea kwenye injini haraka kuliko unavyoweza kuachilia. Mifupa
ilivyovunjika, kuvunjika kwa mifupa mikuuu, michubuko, mishtuko inaweza kutokea.
Wakati wa kuwasha injini, vuta kamba ya kianzishi polepole hadi uhisi upinzani na
kisha vuta haraka ili kuzuia kurudi nyuma kwa haraka.
8.
Kianzishi cha Elektroniki, iwapo kipo: Geuza swichi ya kianzishi cha umeme
(H, Kielelezo 10) kwenye eneo la washa/anza. Mtambo ukianza, achilia swichi ya
kuanza ya umeme.
Notisi
Ili kurefusha maisha ya kianzishi, tumia misururu mifupi ya kuanzisha
(kiwango cha juu cha sekunde tano). Subiri dakika moja kati ya mizunguko
inayoanza.
Kumbuka: Iwapo injini haitaanza baada ya majaribio ya kurudia, wasiliana na mtoa
huduma wako wa ndani au nenda kwenye BRIGGSandSTRATTON.com au piga simu
1-800-233-3723 (Marekani).
9.
Wakati injini inachemka, sogeza kidhibiti cha choki (C, Kielelezo 9) kwenye eneo
la kuendesha.
Simamisha Injini
Onyo
Fueli na mvuke wake unawaka na kulipuka hara sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka vikali au kifo.
• Usiruhusu hewa kuingia kwenye kabureta ili kusimamisha injini.
1.
Zima Swichi iwapo ipo: Sogeza swichi kusimamisha (A, Kielelezo 9, 10) katika
eneo la kusimamisha.
Kidhibiti cha Transfoma ndogo, iwapo kipo: Sogeza kidhibiti cha transfoma
ndogo (B, Kielelezo 9), iwapo kipo, ili kupnguza kasi kisha kwenye eneo la
kusimamisha.
Kianzishi cha Elektroniki, iwapo kipo: Geuza swichi ya kuanza ya umeme (H,
Kielelezo 10) kwenye eneo la zima. Ondoa ufunguo. Weka ufunguo mbali na
watoto.
2.
Baada ya injini kusimama, sogeza kizima fueli (D, Kielelezo 9), iwapo kipo, katika
eneo lililofungwa.
Udumishaji
43