Descargar Imprimir esta página

Briggs & Stratton 106200 Manual Del Operador página 51

Ocultar thumbs Ver también para 106200:

Publicidad

Idiomas disponibles
  • MX

Idiomas disponibles

  • MEXICANO, página 22
8.
Funga kisafishaji cha mwanzo kilichokauka (D, Kielelezo 16) kwenye chujio (C).
9.
Sakinisha chujio (C, Kielelezo 16) na kisafishaji cha mwanzo (D) kwenye eneo la
chini la chujio la hewa (F) na kwenye kitufe (G). Hakikisha chujio limeunganishwa
vizuri kwenye eneo la chini la chujio la hewa na ufunge kwa sehemu za kufunga
(E).
10. Weka kifuniko (B, Kielelezo 16) na ufunge kwa sehemu za kufunga (A). Hakikisha
sehemu za kukazia zimekazwa kabisa.
Kufanyia Huduma Mfumo wa Mafuta
ONYO 
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Weka mafuta mbali na spaki, moto ulio wazi, taa za gesi, joto, na vyanzo vingine
vya mwako.
Mara kwa mara kagua tundu la tangi, tangi la mafuta, kifuniko cha mafuta, na
mirija kama kuna nyufa na uvujaji. Badilisha sehemu zilizoharibika.
Mafuta yakimwagika, subiri mpaka yakauke kabla ya kuwasha injini.
Chujio la Mafuta, iwapo lipo
1.
Kabla ya kubadilisha chujio la mafuta (A, Kielelezo 17), mwaga mafuta kutoka
kwenye tangi ya mafuta au funga vali ya kufunga mafuta. Ikiwa tangi la mafuta si
tupu, mafuta yanaweza kuvuja na kusababisha moto au mlipuko.
2.
Finya vichupo (B, Kielelezo 17) kwenye vibanio (C) ukitumia koleo. Ondoa vibanio
kutoka kwenye chujio la mafuta (A).
3.
Zungusha na uvute mirija ya mafuta (D, Kielelezo 17) kutoka kwenye chujio la
mafuta.
4.
Kagua mirija ya mafuta (D, Kielelezo 17) kama kuna nyufa au uvujaji. Ikiwa
inahitajika, badilisha mirija ya mafuta.
5.
Badilisha chujio la mafuta (A, Kielelezo 17).
6.
Funga mirija ya mafuta (D, Kielelezo 17) kwa kutumia vibanio (C).
Chujio la Mafuta, iwapo lipo
1.
Ondoa kifuniko cha mafuta (A, Kielelezo 18).
2.
Ondoa chujio la mafuta (B, Kielelezo 18).
3.
Iwapo chujio msingi la mafuta ni chafu, lisafishe au ulibadilishe. Ukibadilisha chujio
msingi la mafuta, hakikisha umetumia chujio msingi la mafuta ambalo si ghushi.
Kufanyia Huduma Mfumo wa Kupoesha
ONYO 
Wakati wa uendeshaji, injini na mafla zinakuwa moto. Ukigusa injini moto,
unaweza kuchomeka.
Uchafu unaoweza kuwaka moto, kama vile majani, nyasi na brashi, vinaweza
kushika moto.
Kabla ya kugusa injini au mafla, zima injini na usubiri dakika mbili (2). Hakikisha
kwamba injini na mafla ni salama kugusa.
Ondoa uchafu kwenye mafla na injini.
NOTISI 
Usitumie maji kusafisha injini. Maji yanaweza kuchafua mfumo wa mafuta. Tumia brashi
au kitambaa kavu kusafisha injini.
Hii ni injini inayopoeshwa kwa kutumia hewa. Uchafu au vifusi vinaweza kuzuia
mtiririko wa hewa na kusababisha injini kuwa moto sana na hii kupelekea utendakazi
usioridhisha na injini kuwa na maisha mafupi.
1.
Tumia brashi au kitambaa kavu kuondoa vifusi kwenye grili ya kuingiza hewa.
2.
Weka viunganishaji, springi na vidhibiti vikiwa safi.
3.
Weka ene lililo karibu na nyuma ya mafla, iwapo ipo, bila uchafu wowote unaoweza
kuwaka moto.
4.
Hakikisha mapezi ya kupoesha oili, ikiwa yapo, yakiwa safi.
Baada ya kipindi cha muda, mapezi ya kupoesha silinda yanaweza kukusanya vifusi
na kusababisha injini kuwa moto kupita kiasi. Uchafu huu hauwezi kuondolewa
bila kutenganisha sehemu kadhaa za injini. Ruhusu Mtoa Huduma Aliyeidhinishwa
wa Briggs & Stratton kukagua na kusafisha mfumo wa kupoesha hewa kama
ilivyopendekezwa kwenye Ratiba ya Udumishaji.
Hifadhi
Mfumo wa Mafuta
Rejelea Kielelezo:  19.
ONYO 
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Kuhifadhi Mafuta
Kwa sababu taa za moto au vyanzo vingine vya mwako vinaweza kusababisha
milipuko, hifadhi mafuta au kifaa mbali na tanuu, stovu, hita za kuchemshia maji,
au vifaa vingine ambavyo vina taa za moto.
Weka injini bila kuinama (mkao wa kawaida wa kuendesha). Jaza tangi la mafuta (A,
Kielelezo 19) kwa mafuta. Ili kuruhusu uvukizi wa mafuta, usijaze kuzidi shingo ya tangi
la mafuta (B).
Mafuta yanaweza kuganda yanapohifadhiwa kwenye kontena ya uhifadhi kwa zaidi
ya siku 30. Inapendekezwa kutumia kiimarishaji mafuta bila alkoholi na tiba ya
ethanoli kwenye kontena ya kuhifadhi mafuta ili kuzuia mafuta kuganda na kuyaweka
yakiwa safi.
Unapojaza kontena ya mafuta kwa mafuta, ongeza kiimarishaji mafuta bila alcoholi
kwenye mafuta kama ilivyobainishwa na maagizo ya mtengenezaji. Ikiwa petroli ilio
kwenye injini haijatibiwa kwa kiimarishaji mafuta, ni lazima imwagwe kwenye kontena
iliyoidhinishwa. Endesha injini hadi mafuta yaishe.
Oili ya Injini
Wakati injini bado ina joto, badilisha oili ya injini. Rejelea sehemu ya Kubadilisha Oili
ya Injini.
Kutatua Matatizo
Usaidizi
Ili kupata usaidizi, wasiliana na muuzaji wa karibu au nenda
kwenyeBRIGGSandSTRATTON.COM au piga simu kwa nambari 1-800-444-7774
(nchini Marekani).
Maelezo
Maelezo na Sehemu za Udumishaji
Muundo: 106200
Unyonyaji Mafuta
Shimo
Mpigo
Kiwango cha Oili
Pengo la Plagi ya Spaki
Mkufu wa Plagi ya Spaki
Pengo la Hewa
Mwanya wa Vali ya Kuingiza Hewa
Mwanya wa Vali ya Ekzosi
Nguvu ya injini itapungua kwa 3.5% kwa kila futi 1,000 (mita 300) juu ya kiwango
cha bahari na 1% kwa kila 10°F (5.6°C) juu ya 77°F (25°C). Injini itaendesha kwa
kuridhisha katika pembe ya hadi 15°. Rejelea Mwongozo wa Mwendeshaji kifaa ili
kufahamu viwango salama vinavyoruhusika kwenye miteremko.
Sehemu za Udumishaji - Muundo: 106200
Sehemu za Udumishaji
Chujio la Hewa la Povu - (Kielelezo 13)
Chujio la Hewa la Povu - (Kielelezo 14)
Chujio la Hewa la Karatasi - (Kielelezo
15)
Kisafishaji cha Mwanzo cha Chujio la
Hewa (Kielelezo 15)
Chujio la Hewa la Karatasi - (Kielelezo
16)
Kisafishaji cha Mwanzo cha Chujio la
Hewa (Kielelezo 16)
Plagi ya Spaki
Kifaa cha Kutega Plagi ya Spaki
Kifaa cha kujaribu Spaki
Tunapendekeza kwamba umwone Muuzaji Aliyeidhinishwa wa Briggs & Stratton ili
kupata huduma ya udumishaji na kufanyia huduma injini na sehemu za injini.
9.95 ci (163 cc)
2.677 in (68 mm)
1.77 in (45 mm)
18 - 20 oz (,54 - ,59 L)
.030 in (,76 mm)
180 lb-in (20 Nm)
.010 - .014 in (,25 - ,35 mm)
.004 - .006 in (,10 - ,15 mm)
.006 - .008 in (,15 - ,20 mm)
Nambari ya Sehemu
591717
696263
797430
493537
590601
590602
491055S
816206
84003327
51

Publicidad

loading