Onyo
Fueli na mvuke wake unawaka na kulipuka haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka vikali au kifo.
•
Kamwe usiwashe na kuendesha wakati uunganishaji wa kisafisha hewa (iwapo kipo)
au kichuja hewa (iwapo kipo) kimeondolewa.
Notisi
Usitumie hewa au majimaji yaliyoshinikizwa kusafisha kichujio. Hewa
iliyoshinikizwa inaweza kuharibu kichujio na majimaji yatayeyusha kichujio.
Tazama Ratiba ya Udumishaji wa mahitaji ya huduma.
Modeli mbalimbali aidha zinatumia povu au kichujio cha karatasi. Baadhi ya modeli pia
zinaweza kuwa na kisafishaji cha mwanzo cha hiari ambacho kinaweza kusafishwa na
kutumiwa tena. Linganisha mifano kwenye mwongozo na aina iliyosakinishwa kwenye
injini yako na ushughulikie kama ifuatavyo.
Kichujio cha Povu ya Hewa
1.
Sogeza kufuli ya kuslaidi katika sehemu ya kufungua (A, Kielelezo 15) na ufungue
kifuniko (B).
2.
Ili kuzuia uchafu kutokana na kuanguka kwenye kabureta, kwa makini ondoa elementi
ya povu kwenye sehemu ya chini ya kichuja hewa, (C, Kielelezo 15).
3.
Safisha elementi ya povu kwenye sabuni oevu na maji (C, Kielelezo 15). Finyiza ili
kukausha elementi ya povu kwenye kitambaa safi.
4.
Koleza elementi ya povu kwa mafuta safi ya injini (C, Kielelezo 15). Ili kuondoa mafuta
ya ziada ya injini, finyiza elementi ya povu kwenye kitambaa safi.
5.
Sakinisha elementi ya povu kwenye sehemu ya chini ya kichuja hewa (C, Kielelezo
15).
6.
Funga kifuniko (B, Kielelezo 15) na usogeze kufuli la kuslaidi (A) katika eneo la
kufunga.
Kichujio cha Hewa cha Karatasi
1.
Legeza bizimu (A, Kielelezo 16).
2.
Ondoa kifuniko (B, Kielelezo 16).
3.
Ili kuzia uchafu kutokana na kuangaka kwenye kabureta, kwa makini ondoa kishajishai
cha mwanzo na kichujio (C) kutoka kwenye eneo la chini la kichuja hewa (D, Kielelezo
16).
4.
Ondoa kichujio cha mwanzo kutoka kwenye kichujio (C), (D, Kielelezo 16).
5.
Ili kulegeza uchafu, kwa utaratibu gonga kichujio katika eneo gumu, (C, Kielelezo
16) kwenye sehemu ngumu. Iwapo kichujio ni kichafu kupita kiasi, badilisha na
kichujio kipya.
6.
Osha kisafishaji cha mwazo kwenye sabuni oevu na maji, (D, Kielelezo 16). Ruhusu
kisafishaji cha mwanzo kukauka kabisa. Usiweke mafuta kwenye kisafishaji cha
mwanzo.
7.
Kusanya kisafishaji cha mwanzo kilichokauka kwenye kichujio (C), (D, Kielelezo 16).
8.
Sakinisha kichujio na kisafishaji (D) cha mwanzo kwenye sehemu ya chini ya kichujio
cha hewa, (C, Kielelezo 16). Hakikisha kichujio hutoshea kwa usalama katika sehemu
ya chini ya kichuja hewa.
9.
Sakinisha jalada (B, Kielelezo 16) na ulinde kwa bizimu (A). Hakikisha bizimu
imekazwa.
Shughulikia Mfumo wa Fueli
Tazama Kielelezo: 17, 18
Onyo
Fueli na mvuke wake unawaka na kulipuka haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka vikali au kifo.
•
Hifadhi fueli mbali na cheche, miale iliyo wazi, taa za mwongozo, heat na vyanzo
vingine vya uwakaji.
•
Angalia tundu, tangi, kifuniko na kurekebisha mara kwa mara kwa nyufa na uvujaji.
Badilisha ikiwezekana.
•
Kabla ya kusafisha ua kubadilisha kichujio cha fueli, ondoa fueli au funga vali ya
kufunga fueli.
•
Iwapo fueli itamwagika, subiri hadi ivukize kabla ya kuwasha injini.
•
Sehemu za ubadilishaji lazima ziwe sawa na zilizosakinishwa katika eneo sawa
kama sehemu asili.
Kichujio cha Fueli, iwapo kipo
1.
Kabla ya kusafisha au kubadilisha kichujio cha fueli (A, Kielelezo 17), ondoa mafuta
kwenye tangi au funga vali ya kifuniko cha fueli. Vinginevyo, fueli inaweza kuvuja na
kusababisha moto au mlipuko.
2.
Tumia koleo kufinyiza vichupo kwenye vibanio (C) (B, Kielelezo 17), kisha telezesha
vibanio kutoka kwenye kichujio cha fueli (A). Zungusha na uvute tundu za fueli (D)
kutoka kwenye kichujio cha fueli.
3.
Angalia tundu za fueli (D, Kielelezo 17) kwa nyufa na uvujaji. Badilisha ikiwezekana.
4.
Badilisha kichujio cha fueli kwa kichujio asili cha kifaa cha ubadilishaji (A, Kielelezo
17).
5.
Linda tundu za fueli kwa vibanio (C) kama ilivyoonyeshwa (D, Kielelezo 17).
Kichujio cha Fueli, iwapo kipo
1.
Ondoa kifuniko cha fueli (A, Kielelezo 18).
2.
Ondoa kichujio cha fueli (B, Kielelezo 18).
3.
Iwapo kichujio cha fueli ni kichafu, safisha au kibadilishe. Iwapo utabadilisha kichujio
cha fueli, hakikisha umetumia kichujio asili cha fueli cha ubadilishaji.
Shughulikia Mfumo wa Kupoesha
Onyo
Injini inayoendesha inazalisha joto. Sehemu za injini, hususan mafla, huwa moto
zaidi.
Kuchomeka vikali kunaweza kusababishwa unapogusana nazo.
Uchafu unaoweza kuwaka, kama vile majani, nyasi, brashi, n.k., unaweza kushika
moto.
•
Ruhusu mafla, silinda na mapezi ya injini kupoa kabla ya kugusa.
•
Ondoa uchafu uliokusanyika kutoka kwenye eneo la mafla na eneo la silinda.
Notisi
Usitumie maji kusafisha injini. Maji yanaweza kuchafua mfumo wa fueli. Tumia
brashi au kitambaa kilichokauka kusafisha injini.
Hii ni injini inayopoeshwa na hewa. Uchafu unaweza kuzuia mtiririko wa hewa na
kusababisha injini kuchemka kupita kiasi, na kusababisha utendakazi mbaya na kupunguza
maisha ya injini.
1.
Tumia brashi au kitambaa kilichokauka kuondoa uchafu kutoka kwenye grili ya
kuingiza hewa.
2.
Weka uhusiano, springi na vidhibiti safi.
3.
Weka ene lililo karibu na nyuma ya mafla, iwapo ipo, huru kutokana na uchafu wowote
unaoweza kuwaka.
4.
Hakikisha mapezi ya kupoesha mafuta, iwapo yapo, yako huru kutokana na uchafu.
Baada ya kipindi cha muda, uchafu unaweza kukusanyika kwenye mapezi ya kupoesha
silinda na kusababisha injini kuwa moto kushinda kiasi. Uchafu huu hauwezi kuondolewa
bila kutokusanyika kwa kiasi fulani kwa injini. Ruhusu Mtoa Huduma wa Briggs & Stratton
Aliyeidhinishwa kukagua na kusafisha mfumo wa kupoesha hewa kama ilivyopendekezwa
kwenye Ratiba ya Udumishaji.
Hifadhi
Onyo
Fueli na mvuke wako unawaka na kulipuka haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka vikali au kifo.
Wakati wa kuhifadhi Fueli Au Kifaa Kilicho na Fueli Kwenye Tangi
•
Hifadhi mbali na tanuru, majiko, vichemsha maji au vifaa vingine vya nyumbani
ambavyo vina taa za mwongozo au vyanzo vingine vya mwako kwa sababu vinaweza
kuwasha mvuke wa fueli.
Notisi
Hifadhi kiwango cha injini (eneo la kuendesha kwa kawaida). Iwapo injini
itainamishwa kwa udumishaji, tangi la fueli lazima liwe tupu na sehemu ya kuziba cheche
lazima iwe juu. Iwapo tangi la fueli sio tupu na iwapo injini imeinamishwa katika mwelekeo
mwingine, inaweza kuwa vigumu kuwaka kwa sababu ya mafuta au petroli kuchafua
kuchuja hewa na/au kuziba cheche.
51