Briggs & Stratton BPW3400 Manual Del Usuario página 206

Tabla de contenido

Publicidad

Idiomas disponibles
  • MX

Idiomas disponibles

  • MEXICANO, página 60
Ongeza Mafuta
Takwimu
Mafuta lazima yakidhi mahitaji haya:
• Petroli iliyo safi, mbichi na isiyo na madini.
• Kima cha chini cha 87 octane/87 AKI (91 RON). Kwa
mwinuko wa juu, angalia Mwinuko wa Juu.
• Petroli iliyo na hadi asilimia kumi ya ethanoli (gasohol)
inakubalika.
ILANI Matumizi ya mafuta ambayo haijaidhinishwa
inaweza kuharibu mashine inayoosha na shinikizo
na inafuta udhamini. USITUMIE petroli ambayo
haijaidhinishwa kama vile E15 na E85. USICHANGANE
mafuta katika petroli au urekebisha injini itumie mafuta
tofauti. Ili kulinda mfumo wa mafuta dhidi ya uundaji wa
gamu changanya kidhibiti cha mafuta wakati unapokuwa
ukiongeza mafuta kwenye mashine yako. Angalia Hifadhi.
Mafuta yote ni tofauti. Ukipata matatizo ya kuwasha au
utekelezaji baada ya kutumia mafuta, badilisha mafuta
unayotumia kwa muuzaji mwingine au badilisha kampuni.
Injini hii imethibitishwa kutumia petroli. Mfumo wa udhibiti
wa utoaji moshi wa injini hii ni EM (Marekebisho ya Injini).
ONYO! Mafuta na mvuke wake vyote
vinaweza kuwaka moto na kulipuka na
hivyo basi kusababisha kuungua, moto au
milipuko inayoweza kusababisha kifo au majeraha
mabaya. Zima injini ya kioshaji cha presha na uiwache
ipoe kwa angalau dakika mbili kabla ya kutoa kifuniko cha
mafuta. Fungua kifuniko pole pole ili kutoa presha iliyo
kwenye tenki. Jaza tangi la mafuta ukiwa nje ya nyumba.
USIJAZE tenki kupita upeo yake. Wacha nafasi kwa ajili ya
upanuzi wa mafuta. Kama mafuta imemwagika, subiri hadi
iwe mvuke kabla ya kuanza injini. Weka mafuta mbali na
cheche, moto ulio wazi, taa ya kujaribia, joto, na vyanzo
vingine vya moto. Angalia mistari ya mafuta, tenki,kofia na
sehemu za kuunganisha mara nyingi kwa nyufa au
mtiririko. Badilisha kama inabidi. USIWASHE sigara au
moshi.
1. Safisha eneo karibu na kifuniko cha mafuta, toa kifuniko.
2. Anza kuongeza mafuta yasiyo na madini polepole (A)
kwa tenki ya mafuta (B). Kuwa makini ili yasifurike.
Wacha nafasi ya kama sentimita 4 (inchi 5) (C) ya
tenki kwa ajili ya upanuzi wa mafuta.
3. Weka kifuniko ya mafuta na uwache mafuta yote
yaliomwagika yawe mvuke kabla uwashe injini.
Mwinuko wa Juu
Kwa miinuko zaidi ya mita 1524 (futi 5,000), Kima cha
petroli chini yaa 85 octane/85 AKI (89 RON) kinakubalika.
Ili ufuate sheria za kuzalisha uchafu, marekebisho ya
mwinuko wa juu unahitajika. Operesheni bila marekebisho
haya yatasababisha upungufu kwa utekelezaji,
kuongezeka kwa matumizi ya mafuta, na kuongezeka kwa
uzalishaji wa uchafu. Angalia muuzaji wa Briggs & Stratton
aliyethibitishwa kwa maelezo zaidi kuhusu marekebisho
ya miinuko ya juu. Operesheni ya injini katika sehemu
za milimani zilizo chini ya mita 762 (2,500 ft.) pamoja na
mkoba wa sehemu za milima ya juu haipendekezwi.
6
6
9
Eneo la Kioshaji cha Presha
Sumu ya Kaboni Monoksidi
ONYO! Ekzosi ya injni huwa na monksidi ya
kaboni, gesi ya sumu inayoweza kukuua ndani ya
dakika chache. HUWEZI kuinusa, kuiona, au hata
kuiramba. Hata kama huwezi kunusia moshi unaotolewa,
bado unaweza kukumbana na gesi ya Carbon Monoxide.
Tumia bidhaa hii NJE PEKEE mbali na madirisha, milango
na matundu ili kupunguza hatari ya gesi ya kaboni
monoksidi kukusanyika na uwezekano wa kuwa
inasambazwa kuelekea maeneo ya nje. Weka ving'ora vya
Carbon Monoxide vinavyoendeshwa betri au ving'ora vya
Carbon Monoxide vya kuchomekwa vilivyo na chelezo cha
betri kulingana na maelekezo ya mtengenezaji. Kamsa za
moshi haziwezi kugundua gesi ya kaboni monoksidi.
USITUMIE bidhaa hii ndani ya nyumba, gereji, sehemu ya
nyumba iliyo chini ya ardhi, chumba kidogo sana, vibanda,
au nafasi zingine hata kama unatumia vipepeo au milango
zilizofunguliwa na madirisha za kuingizia hewa. Kaboni
monoksidi inaweza kujaa haraka katika nafasi hizi na
inaweza tuwama kwa masaa, hata baada ya bidhaa hii
imezimika. DAIMA weka bidhaa hii katika mwelekeo
ambao upepo unavuma na elekeza eksozikutoka nafasi
zilizojazwa. Ukianza kujisikia mgonjwa, kizunguzungu, au
dhaifu wakati unatumia bidhaa hii, tafuta hewa safi MARA
MOJA. Mwone daktari. Unaweza kuwa na sumu ya kaboni
monoksidi.
Hatari ya Moto
ONYO! Joto/gesi zinazotolewa zinaweza
kusababisha kuwashwa kwa moto, vibanda au
uharibifu wa tangi ya mafuta na hivyo basi
kusabaisha moto, na kuishia kuleta vifo au majeraha mabaya.
Ruhusu nafasi ya angalau mita 1.5 (futi 5) katika pande zote
za kioshaji cha pressure ikiwemo kioshaji cha juu.
Unganisha Bomba na usambazaji wa Maji
Kwenye Pampu
Takwimu
ILANI Kagua mpira wa maji ulio na shinikizo ya juu ili
kupata makato, mitiririko au uharibifu.
1. Vuta kwenye kola bomba yenye presha ya juu zaidi (C),
ingiza katika bunduki ya kunyunyizia (A) halafu wachilia
kola. Funga mpira huo wa maji na uhakikishe kwamba
uko salama.
2. Unganisha mwisho huo mwingine wa bomba (J)
kwenye pampu kish ukaze.
3. Kagua pahali pa kuingizia kabla ya kuunganisha
bomba la shamba kwa nafasi ya kuingizia maji (K).
Safisha skrini kama inayo chembechembe zozote au
uisawazishe kama imeharibika. USIENDESHE kioshaji
kwa presha kama skrini ya kuingiza maji imeharibika.
4. Hakikiasha kuwa chanzo cha maji kinauwezo wa
kusambaza maji kwa kiwango cha zaidi ya lita 14.38
(galoni 3.8) kwa dakika mija na 0.14-0.55 MPa (1.4-5.5
BAR au 20-80 PSI) katika mwisho wabomba la maji la
kioshaji cha presha.
5. Pitisha maji katika mpira wa maji ili kutoa uchafu.
ILANI Tumia maji baridi PEKEE (chini ya 38°C (100°F)).
ILANI Kutumia kizuizi cha mtiririko wa kuja nyuma katika
tundu la kuingiza maji la pampu inaweza kusababisha uharibifu
wa pampu. LAZIMA kuwe na angalau mita 3 (futi 10) ya mpira
wa maji ambao haujazuiliwa kati ya mashine inayoosha ikitumia
shinikizo pamoja na kizuizi cha mtiririko wa kuja nyuma.
Takwimu
10
5
BRIGGSandSTRATTON.COM
BRIGGSandSTRATTON.COM

Publicidad

Tabla de contenido
loading

Este manual también es adecuado para:

020595-03

Tabla de contenido