Udumishaji
Maelezo ya Udumishaji
ONYO
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Wakati wa huduma ya udumisha ikiwa ni muhimu kuinamisha kifaa, ikiwa tangi la
mafuta limeshikana na injini, hakikikisha kwamba ni tupu na upande wa plagi ya spaki
uko juu. Ikiwa tangi la mafuta si tupu, mafuta yanaweza kuvuja na kusababisha moto au
mlipuko. Ikiwa injini imeinama katika mkao tofauti, haitaguruma kwa urahisi kwa sababu
ya kuchafuka kwa chujio la hewa au plagi ya spaki kwa oili au mafuta.
ONYO
Mwako wa injini usiokusudiwa unaweza kusababisha mshtuko wa umeme, moto
au mlipuko na kupelekea kunaswa, kukatwa kwa viungo kwa kiwewe, au majeraha
mabaya ya ukataji wa ngozi.
Kabla ya kufanya marekebisho au ukarabati:
•
Tenganisha nyaya zote za plagi ya spaki na uziweke mbali na plagi za spaki.
•
Tenganisha betri katika kichwa cha hasi (injini tu zenye kianzishaji cha umeme).
•
Tumia zana sahihi pekee.
Unapokagua uwepo wa cheche:
•
Tumia kifaa kilichoidhinishwa cha kujaribu plagi ya spaki.
•
Usikague cheche huku plagi ya spaki ikiwa imeondolewa.
ONYO
Sehemu za kubadilishia ni lazima ziwe za aina sawa na ziwekwe katika eneo sawa
kama sehemu asilia. Sehemu nyingine huenda zinaweza kuharibu kifaa au kusababisha
majeraha.
NOTISI
Vijenzi vyote vilivyotumiwa kutengeneza injini hii ni lazima visalie kwenye maeneo yake
ili kupata uendeshaji bora.
Mwone Mtoa Huduma Aliyeidhinishwa wa Briggs & Stratton ili kupata huduma zote za
udumishaji na kufanyia huduma injini na sehemu za injini.
Huduma ya Udhibiti wa Mafukizo
Ili kupata huduma ya udumishaji, ubadilishaji, au ukarabati wa vifaa na mifumo
ya kudhibiti mafukizo, wasiliana na kituo chochote kinachohitimu cha kukarabati
injini au mtoa huduma aliyehitimu wa kukarabati injini. Hata hivyo, ili kupata
huduma ya kudhibiti mafukizo ya "bila malipo", ni lazima kazi ifanywe na muuzaji
aliyeidhinishwa na kiwanda. Rejelea Kauli za Udhibiti Mafukizo.
Ratiba ya Udumishaji
Saa 5 za Kwanza
•
Badilisha oili.
Mpishano wa Saa 8 au Kila Siku
•
Kagua kiwango cha oili ya injini.
•
Safisha maeneo yaliyo karibu na mafla na vidhibiti.
•
Safisha grili ya kuingiza hewa.
Mpishano wa Saa 100 au Kila Mwaka
•
Fanyia huduma mfumo wa ekzosi.
•
Badilisha Oili katika Kifaa cha Upunguzaji (iwapo kipo).
Mpishano wa Saa 200 au Kila Mwaka
•
Badilisha oili ya injini.
•
1
Safisha chujio la hewa
Mpishano wa Saa 600 au Miaka 3
•
Badilisha chujio la hewa.
Kila Mwaka
52
•
Badilisha plagi ya spaki.
•
Fanyia huduma mfumo wa mafuta.
•
Fanyia huduma mfumo wa kupoesha
•
2
Kagua uwazi wa vali
.
1
Safisha mara nyingi zaidi katika mazingira ya vumbi au wakati kuna vipengee vingi
hewani.
2
Haihitajiki isipokuwa kutokee matatizo ya utendakazi wa injini.
Kabureta na Kasi ya Injini
Usihitilafiane na kabureta, springi ya kidhibiti, viunganishaji, au sehemu nyingine ili
kubadilisha kasi ya injini. Iwapo marekebisho yoyote yanahitajika, wasiliana na Mtoa
Huduma Aliyeidhinishwa wa Briggs & Stratton ili kufanyiwa huduma.
NOTISI
Mtengenezaji wa kifaa hubainisha kasi ya juu zaidi ya injini kama ilivyosakinishwa
kwenye kifaa. Usizidishe kasi hii. Iwapo huna uhakika kasi ya juu zaidi ya kifaa hiki
ni ipi, au kasi ya injini iilivyopangwa tangu kiwandani, wasiliana na Muuzaji Huduma
Aliyeidhinishwa wa Briggs & Stratton ili kupata usaidizi. Kwa oparesheni salama na
sahihi ya kifaa hiki, kasi ya injini inapaswa tu kurekebishwa na mtaalamu wa huduma
aliyehitimu.
Kufanyia Huduma Plagi ya Spaki
Kagua pengo la plagi ya spaki (A, Kielelezo 20) ukitumia pamba ya waya (B). Ikiwa
inahitajika, rekebisha pengo la plagi ya spaki. Sakinisha na ukaze plagi ya spaki kwa
kiwango sahihi. Ili kupata maelezo maalum ya pengo na kukaza, rejelea sehemu ya
Maelezo.
Kufanyia Huduma Ekzosi na Mifumo ya Kupoesha
ONYO
Wakati wa uendeshaji, injini na mafla zinakuwa moto. Ukigusa injini moto,
unaweza kuchomeka.
Vitu vinavyoweza kuwaka moto, kama vile majani, nyasi, brashi, vinaweza kushika
moto.
•
Kabla ya kugusa injini au mafla, zima injini na usubiri dakika mbili (2). Hakikisha
kwamba injini na mafla ni salama kugusa.
•
Ondoa uchafu kwenye mafla na injini.
Ni ukiukaji wa Kanuni za Rasilimali za Umma za California, Sehemu ya 4442, kutumia
au kuendesha injini katika eneo linalozungukwa na msitu, lililozungukwa na brashi, au
lililo na nyasi isipokuwa mfumo wa ekzosi una kishika spaki, kama ilivyobainishwa katika
sehemu ya 4442, kilichodumishwa katika hali fanisi ya kufanya kazi. Mamlaka nyingine
za majimbo au serikali ya kitaifa huenda zikawa na sheria sawia; Rejelea Kanuni za
Serikali ya KItaifa ya 36 CFR Sehemu ya 261.52. Wasiliana na mtengenezaji asilia wa
kifaa, muuzaji rejareja, au muuzaji ili kupata kishika spaki kilichobuniwa kwa ajili ya
mfumo wa ekzosi uliowekwa kwenye injini hii.
Hii ni injini inayopoeshwa kwa kutumia hewa. Uchafu au vifusi vinaweza kuzuia mtiririko
wa hewa na kusababisha injini kuwa moto sana. Hii inapelekea utendakazi usioridhisha
na kufupisha maisha ya injini. Mapezi ya kupoesha silinda yanaweza kuwa na vifusi
ambavyo haviwezi kuondolewa bila kufungua baadhi ya shemu za injini. Hakikisha
kwamba Mtoa Huduma Aliyeidhinishwa wa Briggs & Stratton amekagua na kusafisha
mfumo wa kupoesha hewa. Rejelea Ratiba ya Udumishaji.
1.
Hakikisha kwamba hakuna vitu vinavyoweza kushika moto karibu na nyuma ya
mafla.
2.
Tumia brashi au kitambaa kavu kuondoa vifusi kwenye maeneo ya kifuniko cha
chumba cha blowa, mafla na silinda. USITUMIE maji kusafisha injini.
3.
Hakikisha viunganishaji, springi na vidhibiti ni safi.
4.
Kagua mafla kama ina nyufa, ubabuzi, au uharibifu mwingine.
5.
Ondoa kifaa cha kusonga au kishika cheche, iwapo kipo, na ukague kama kuna
uharibifu au uzuiaji wa kaboni. Hakikisha kwamba unasafisha au kusakinisha vipuri
kabla ya kuendesha kifaa.
6.
Ikiwa yapo, hakikisha mapezi ya kupoesha oili ni safi.
1
.