Murray MP450D20 Manual Del Operador página 80

Cortacésped de empuje manual
Tabla de contenido

Publicidad

Idiomas disponibles
  • MX

Idiomas disponibles

  • MEXICANO, página 20
5.3 Operesheni Salama ka Ujumla
1. Usitumie injini katika maeneo yaliyofungwa au yasiyo
na hewa ya kutosha ambapo mvuke wa kaboni monoksidi
unaweza kusanyika.
2. Usipindue mashine wakati unawasha injini, ila tu wakati
mashine inafaa kupinduliwa ili injini iwake. Katika hali hiyo,
usiipindue sana na uinue sehemu tu iliyo mbali na opereta.
3. Washa injini kwa makini kulingana na maelekezo na miguu
yako iwe mbali na ubapa.
4. Usiwashe injini wakati umesimama mbele ya njia ya
kuteremshia uchafu.
5. Wakati injini imewashwa, inapendekezwa uhakikishe
wengo ya kudhibiti injini na mfumo wa breki (kuwepo kwa
udhibiti wa opereta) zinafanya kazi vizuri kabla ya kuanza
kukata nyasi.
6. Wakati unatumia mashine ya kukata nyasi tembea tu,
usiwahi kukimbia.
7. Chukua huduma yuziada wakati unatumia mashine ya
kukata nyasi kwenye miteremko (ona sehemu 5.4 Operesheni
ya Mteremko hapa chini) na karibu miteremko ya kasi, mitaro
au matuta.
8. Usiwahi kurudisha nyuma au kuvuta mashine hii ya kukata
nyasi wakati injini inatumika.
9. Simamisha ubapa kama mashine ya kukata nyasi inageuzwa
wakati unavuka ardhi isiyo ya nyasi na wakati unasafirisha
mashine kwenda na kutoka eneo linalokatwa nyasi;
10. Chunga trafiki wakati unatumia karibu na barabara.
11. Usiweke mikono au miguu karibu au chini ya sehemu
zinzozunguka. Kaa mbali na mashimo za kutolea uchafu kwa
wakati wote.
12. Usiwahi kuchukua au kubeba mashine wakati injini
inanguruma.
13. Zima injini, toanisha buti ya spaki plagi na uhakikishe
kuwa sehemu zote zinazosonga zimesimama kabisa:
- Kabla ya kusafisha sehemu zilizozibwa au kulainisha
sehemu ya kuteremshia;
- Kabla ya kuangalia, kusafisha au kufanya kazi kwa mashine
inayokata nyasi.
- Baada ya kugonga vitu wakati wa matumizi. Kagua mashine
kwa uharibifu na urekebishe kabla ya kuanzisha tena na kuitumia.
- Kama mashine imeanza kutetemeka kwa hali isiyo ya
kawaida (angalia mara moja - mtetemo usio wa kawaida ni
onyo la shida).
- Kabla ya kuiwacha machine bila huduma.
- Kabla ya kuongeza mafuta kwa mashine.
- Kabla ya kusafisha, kukarabati au kukagua mashine.
14. Kuwa katika kelele na mtetemeko kutoka injini ya petroli
kwa muda mrefu inafaa iepukwe - ili kupunguza hatari kutoka
kwa kelele na mtetemeko unashauriwa kuchukua mapumziko
na upunguze muda wa operesheni; vaa kinga ya kelele ya
injini kwa masikio pamoja na glavu ili upunguze mtetemeko
kwa mikono.
8
5.4 Operesheni ya Usalama kwa Mteremko
Mteremko ni sababu kubwa inayohusiana na kuteleza na ajali za
kuanguka ambayo zinaweza kusababisha majeraha makubwa.
Uendeshaji katika miteremko yote inahitaji tahadhari zaidi. Kama
una wasiwasi kwenye mteremko, usikate nyasi huko.
1. Kata nyasi toka upande mmoja hadi upande mwingine kwa
mteremko; si kutoka juu na chini.
2. Toa vitu kama mawe, matawi, na kadhalika kabla ya kuanza
kukata nyasi.
3. Chunga pia mashimo, matope, au matuta. Nyasi ndefu
zinaweza kuficha vigingi.
4. Usikate nyasi karibu na sehemu za mishuko, mitaro, au
matuta. Opereta anaweza kuteleza au kupoteza mizani.
5. Usikate nyasi kwa mteremko ulio na mwinuko wa kupita kiasi
(kiwango cha juu ya digrii 10) au maeneo ambayo ardhi ni mbaya
sana, chukua tahadhari kubwa wakati unabadilisha mwelekeo kwa
mteremko.
6. Usikate nyasi katika nyasi zilizo nyevunyevu. Kupungua
kwa nguvu ya magurudumu kukamata chini kunaweza
kusababisha iteleze.
7. Usiiwache mashine kwa mteremko bila opereta mwingine
(hata kama injini imezimika).
5.5 Usafiri
1. Mwaga mafuta kutoka kwa tenki,wacha injini ikinguruma
hadi petroli iishe (usiiwache mashine ikinguruma peke yake).
Ikiwa tanki la mafuta lazima likaushwe, litapaswa kukaushwa
nje ya nyumba.
2. Ondoa buti ya spaki plagi kutoka kwa spaki plagi.
3. Mwaga oili kutoka injini.
4. Osha mapezi ya kupoza silinda na makazi ya injini.
5. Wakati unasafirisha mashine na lori au kifaa kingine,
hakikisha kuwa imefungwa vizuri na sehemu yoyote haisongi.
6. Kwa kusafirisha bidhaa, tumia mfuko halisi wa bidhaa.
6. Uunganishwaji
6.1 Kuunganisha Mpini
6.1.1 Jinsi ya Kuunganisha Mpini wa Chini
Kuunganisha mpini wa chini imeelezwa katika jedwali lifuatalo
na modeli maalum:
Kumbukumbu
Modeli
ya Picha
MP450D20
Kielelezo 8.
MP625MD21H
Kielelezo 9.
MP550RM21/
MP675RM21H /
MP550RMD21/
Kielelezo 10.
MP675RMD21H/
MX675RMD22H
Jinsi ya Kuunganisha
mpini wa chini
Funga mpini wa chini
kwa deki na safu ya sah-
ani, parafujo na komeo
(ambazo zimefungwa
kwenye deki).
Funganisha mpini wa
chini kwa breki za mpini
kwa kutumia komeo na
kirungu.
www.murray.com

Publicidad

Tabla de contenido

Solución de problemas

loading

Tabla de contenido