Vanguard 290000 Manual Del Usuario página 51

Ocultar thumbs Ver también para 290000:
Tabla de contenido

Publicidad

Idiomas disponibles
  • MX

Idiomas disponibles

  • MEXICANO, página 15
Notisi
Vijenzi vyote vilivyotumiwa kujenga injini hii lazima visalie sawa kwa uendeshaji
bora.
Onyo
Cheche zisizotarajiwa zinaweza kusababisha moto au mshtuko wa kielektriki.
Uwashaji usiotarajiwa unaweza kusababisha kunaswa, kukatwa kwa viungo kwa
kiwewe, au majeraha makali ya ukataji wa ngozi.
Madhara ya moto
Kabla ya kutekeleza marekebisho au ukarabati:
Tenganisha waya ya kuziba cheche na uhifadhi mbali na kuziba cheche.
Tenganisha betri katika mwisho wa chanya (injini zilizo na kiwashaji wa kielektriki
tu.)
Tumia zana sahihi tu.
Usihitilifiane na springi ya kithibiti, viunganishi au sehemu zingine ili kuongeza kasi
ya injini.
Sehemu za ubadilishaji lazima ziwe sawa na zilizosakinishwa katika eneo sawa
kama sehemu asili. Sehemu zingine huenda zisitekeleze vilevile, zinaweza kuharibu
kitengo, na inaweza kusababisha majeraha.
Usigonge gurudumu la kuongeza kasi ya injini kwa nyundo au kifaa kigumu kwa
sababu gurudumu la kuongeza kasi ya injini linaweza kuvunjika wakati wa kuendesha.
Wakati wa kujaribu cheche:
Tumia kijaribio cha kuziba cheche kilichoidhinishwa.
Usikague injini wakati kuziba cheche imeondolewa.
Huduma ya Udhibiti wa Mafukizo
Udumishaji, ubadilishaji, au ukarabati wa vifaa na mifumo ya kudhibiti mafukizo
unaweza kutekelezwa na kituo chochote au mtu yeyote wa kukarabati injini. Hata
hivyo, ili kupata huduma ya kudhibiti mafukizo ya "bila malipo", ni lazima kazi ifanywe na
mtoa huduma aliyeidhinishwa na kiwanda. Tazama Taarifa ya Udhibiti wa Mafukizo.
Ratiba ya Udumishaji
Kila Baada ya Saa 8 au Kila siku
Angalia kiwango cha mafuta ya injini
Safisha maeneo yaliyo karibu na mafla na vidhibiti
Kila Baada ya Saa 100 au Kila mwaka
Badilisha kuziba cheche
Badilisha mafuta ya injini
Badilisha kichujio cha mafuta (iwapo kipo)
1
Shughulikia kichuja chewa
Safisha kisafishaji cha mwanzo (iwapo kipo)
Shughulikia mfumo wa eneo la injini la kutolea moshi
Kila baada ya Saa 250
Angalia uondoaji wa vali. Rekebisha ikiwa ni muhimu.
Kila Baada ya Saa 400 au Kila mwaka
Badilisha kichujio cha hewa
Badilisha kichuja fueli
Shughulikia mfumo wa kupoza
Safisha mapezi ya kupoza hewa
1
Katika hali ya vumbi au uchafu unaosambazwa na hewa upo, safisha mara kwa
mara.
Mfumo wa Elektroniki wa Utiaji Fueli (EFI)
Mfumo wa EFI huchunguza halijoto ya injini, kasi, na volteji ya betri kwa kuanzisha injini
na kupasha joto. Hakuna marekebisho kwenye mfumo. Matatizo ya kuanza au uendeshaji
yakitokea, wasiliana na Mhudumu Aliyeidhinishwa wa Briggs & Stratton.
Notisi
Hakikisha kuwa umefuata hatua zilizo hapa chini au huenda Mfumo wa EFI
umeharibika.
1
1
1
Usiwahi kuanza injini kebo za betri zikiwa zimelegea.
Geuza ufunguo upande wa kuzima kabla ya kutenganisha, kuondoa na kusakinisha
betri.
Usiwahi kutumia chaja ya betri kuanzisha injini.
Usiwahi kutenganisha kebo za betri huku injini ikiwa inafanya kazi.
Unapounganisha kebo za betri, kwanza unganisha kebo chanya (+) kisha uunganishe
kebo hasi (-) kwenye betri.
Unapochaji betri, geuza swichi ya moto upande wa kuzima na utenganishe kebo
hasi ya betri (-) kutoka kwenye betri.
Usinyunyize maji moja kwa moja kwenye Moduli ya Kidhibiti cha Elektroniki.
Mfumo wa Elektroniki wa Kudhibiti Fueli
Mfumo wa Udhibiti Fueli wa Eletroniki hufuatilia halijoto ya injini, kasi, na volteji ya betri ili
kurekebisha choki wakati wa kuanzisha injini na kupasha joto. Hakuna marekebisho kwenye
mfumo. Matatizo ya kuanza au uendeshaji yakitokea, wasiliana na Mhudumu Aliyeidhinishwa
wa Briggs & Stratton.
Notisi
Hakikisha kuwa umefuata hatua zilizo hapa chini au huenda Udhibiti Fueli wa
Eletroniki umeharibika.
Usiwahi kuanza injini kebo za betri zikiwa zimelegea.
Geuza ufunguo upande wa kuzima kabla ya kutenganisha, kuondoa na / au
kusakinisha betri.
Usiwahi kutumia chaja ya betri kuanzisha injini.
Usiwahi kutenganisha kebo za betri huku injini ikiwa inafanya kazi.
Unapounganisha kebo za betri, kwanza unganisha kebo chanya (+) kisha uunganishe
kebo hasi (-) kwenye betri.
Unapochaji betri, geuza swichi ya moto upande wa kuzima na utenganishe kebo
hasi ya betri (-) kutoka kwenye betri.
Usinyunyize maji moja kwa moja kwenye Kitengo cha Kidhibiti cha Elektroniki.
Kabureta na Kasi ya Injini
Kamwe usifanye marekebisho kwenye kabureta au kasi ya injini. Kabureta iliwekwa kwenye
kiwanda kufanya kazi kwa ufanisi chini ya masharti mengi. Usihitilafiane na springi ya
kidhibiti, uhusiano au sehemu nyingine ili kubadilisha kasi ya injini. Iwapo marekebisho
yoyote yanahitajika wasiliana na Mtoa Huduma wa Briggs & Stratton Aliyeidhinishwa kwa
huduma.
Notisi
Mtengenezaji wa kifaa hubainisha kasi ya juu ya injini kama ilivyosakinishwa
kwenye kifaa. Usizidi kasi hii. Iwapo huna uhakika kasi ya juu ya kifaa hiki ni ipi, au
kasi ya injini imewekwa kwa kutoka kwenye kiwanda, wasiliana na Mtoa Huduma wa
Briggs & Stratton Aliyeidhinishwa kwa usaidizi. Kwa oparesheni salama na sahihi ya
kifaa, kasi ya injini inafaa kurekebishwa na mtaalam wa huduma aliyehitimu tu.
Shughulikia Kuziba Cheche
Tazama Kielelezo: 11
Angalia nafasi iliyo (A, Kielelezo 11) na kipimo (B). Iwapo ni muhimu, weka upya nafasi.
Sakinisha na ukaze kuziba cheche katika toku iliyopendekezwa. Kwa uwekaji wa nafasi
au toku, tazama Vipimo sehemu .
Kumbuka: Katika baadhi ya maeneo, sheria ya ndani huhitaji kutumia kuziba cheche
ambayo haipitishi nishati ili kupunga ishara za kuwaka. Iwapo injini hii ilikuwa na kuziba
cheche ambayo haipitishi nishati mwanzoni, tumia aina sawa kwa ubadilishaji.
Shughulikia Mfumo wa Eneo la kutolea
moshi
Onyo
Injini inayoendesha inazalisha joto. Sehemu za injini, hususan mafla, huwa moto
zaidi.
Kuchomeka vikali kunaweza kusababishwa unapogusana nazo.
Uchafu unaoweza kuwaka, kama vile majani, nyasi, brashi n.k. unaweza kushika
moto.
Ruhusu mafla, silinda na mapezi ya injini kupoa kabla ya kugusa.
Ondoa uchafu uliokusanyika kutoka kwenye eneo la mafla na eneo la silinda.
51

Publicidad

Tabla de contenido
loading

Productos relacionados para Vanguard 290000

Este manual también es adecuado para:

300000350000380000

Tabla de contenido