Kusafirisha
Unaposafirisha kifaa, zungusha vali ya kufunga mafuta
hadi eneo linaloonyesha zima (
kifaa katika mkao unaosababisha mafuta kumwagika.
Kiashiria Oili Chache
Mfumo wa kiashiria oili chache umeundwa ili kuzuia
uharibifu wa injini unaosababishwa na oili isiyotosha ya
injini. Iwapo kiwango cha oili kimepungua hadi chini ya
kiwango kilichowekwa, taa nyekundu ya kiashiria oili
chache itawaka na swichi ya kiwango cha oili itazima
injini. Iwapo injini itazima au taa nyekundu ya kiashiria
oili chache itawaka unapobonyeza swichi ya kuamilisha,
kagua kiwango cha oili ya injini.
Hatua ya 3: Kugurumisha Jenereta
Kielelezo
1 3 9
Ondoa vyombo vyote vya umeme vilivyounganishwa na
jenereta. Tumia maagizo yafuatayo ya kuwasha:
1. Hakikisha kifaa kiko nje kwenye eneo tambarare.
ILANI Kukosa kutumia kifaa hiki kwenye eneo
tambarare kunaweza kusababisha kifaa kuzima.
2. Zungusha vali ya mafuta (1, X) kuelekea upande
wa kulia hadi eneo linaloonyesha washa (
Kugurumisha kwa Mbali
3. Bonyeza kitufe cha washa/zima (3, A) kwenye kidude
cha kuwasha kwa mbali ili kuamilisha jenereta.
4. Ndani ya sekunde 5, bonyeza kitufe cha kuwasha
(3,B). Kitufe cha washa/zima kwenye jenereta
kitamweka mwangaza wa buluu wakati mitambo
inapopokewa na jenereta kuguruma.
Kugurumisha kwa Kuvuta Kamba au Kiumeme
3. Bonyeza swichi ya kuamilisha 1 (1, B) ili kuwasha
skrini. Kitufe cha washa/zima 2 (1, Z) kitamweka
mwangaza wa buluu kwa muda wa dakika moja.
ILANI Ikiwa kitufe cha washa/zima hakitamweka
mwangaza wa kijani, betri haijaunganishwa au iko chini
sana kuweza kuwasha jenereta.
ILANI Kifaa hiki kimewekwa mfumo wa choki
elektroniki. Mfumo wa choki elektroniki unamaanisha
kwamba hakuna priming au choking kwa njia ya kawaida
mradi tu betri iwe imeunganishwa na imechajiwa.
4A. Kugurumisha kiumeme; bonyeza na ushikilie
kitufe cha washa/zima 2 (1, Z) kwa sekunde moja
huku kikimweka mwangaza wa kijani ili kugurumisha
jenereta. Jenereta inapoguruma, kitufe cha washa/
zima kitageuka buluu kuonyesha kwamba jenereta
iko tayari kutumika.
ILANI Jenereta ikikosa kuguruma, kitufe cha washa/
zima kitageuka chekundu kwa sekunde 5, kisha kimweke
mwangaza wa kijani kwa hadi dakika moja. Rudia hatua 4A.
4B. Kugurumisha kawaida; kamata mpini-nywea (L)
na uvute polepole mpaka uhisi ugumu kidogo. Kisha
vuta kwa haraka ili kuwasha injini, choki elektroniki
bado itatumika betri ikiwa chini.
ILANI Jenereta ikiendelea kutowasha, betri yako
huenda imeisha nishati na utahitaji kugurumisha injini kwa
njia ya kawaida. Ondoa kifuniko cha udumishaji na uweke
wenzo wa choki (9, A) kwenye eneo la katikati. Mfumo
wa choki elektroniki utazima choki kiotomatiki baada ya
jenereta kuguruma. Rudisha kifuniko cha udumishaji.
ILANI Injini ikiwasha lakini ikose kunguruma, tazama
Kiashiria Oili Chache.
). Usiinamishe injini au
).
Kuzuilia Ugurumishaji kwa Mbali
Ugurumishaji kwa mbali unaweza kuzuiliwa ili jenereta
yako isiweze kugurumishwa kwa mbali. Ili kuzuilia
ugurumishaji kwa mbali, bonyeza swichi ya kuamilisha
1 (1, B) ili kuwasha skrini, bonyeza na ushikilie kitufe
cha washa/zima (1, Z) kwenye jenereta kwa sekunde
10. Taa ya washa/zima itamweka mwangaza mwekundu
mara tatu kuonyesha kwamba utendaji wa ugurumishaji
kwa mbali umezuilia. Ili kuacha kuzuilia, rudia.
Kubonyeza kitufe kwenye kidude cha kuwasha kwa
mbali, kitufe cha washa/zima kitamweka mwangaza
mwekundu mara 3 wakati utendaji umefungwa na
kitamweka mwangaza wa buluu mara 3 wakati utendaji
umefngwa.
QPT™ (QUIET POWER TECHNOLOGY™) Kielelezo
Kipengele hiki inaimarisha utumizi wa mafuta.
Wakati swichi ya QPT (E) IMEWASHWA, kasi ya
injini itaongezeka kadri vifaa vinavyotumia umeme
vinapounganishwa, na kupunguka kadri vifaa
vinavyotumia umeme vinapoondolewa.
Swichi ikiwa imezimwa, injini itanguruma kwa kasi zaidi.
Kurejesha Nishati Nyumbani kwa Kutumia
Swichi ya Ubadilishaji
Uunganishaji kwenye mfumo wa umeme wa nyumba
yako ni lazima utumie swichi ya ubadilisha isiyo otomatiki
iliyowekwa na fundi wa umeme aliyehitimu. Muunganisho
huu ni lazima utenganishe nishati ya jenereta na umeme
wa kawaida na uambatane na sheria na kanuni zote
husika za umeme.
Kurejesha Nishati kwa Kutumia Kebo Ndefu
Matumizi ya umeme ya jenereta hii, hayafai kupita uwezo
wa nguvu za umeme zilizopendekezwa, katika hali
iliyopendekezwa, kama ilivyoonyeshwa kwenye lebo ya
data ya kifaa. Punguza matumizi ya umeme unapotumia
jenereta katika hali ambazo hazijapendekezwa.
Tumia nyaya-enezi za ubora wa juu kuambatana na IEC
60245-4 na nyaya za kutoa umeme za kutoa umeme wa
AC kwenye jenereta za volti 230. Kagua nyaya-enezi
kabla ya kila tumizi. Hakikisha kwamba nyaya-enezi zote
zina vipimo mwafaka na hazijaharibika. Unapotumia
nyaya-enezi chini ya 40° C, jumla ya urefu wa nyaya kwa
sehemu ya msalaba ya 1.5 mm² haifai kuzidi mita 50 au
kwa sehemu ya msalaba ya 2.5 mm² haifai kuzidi mita 80.
ONYO! Nyaya-enezi zilizozidisha kiwango cha
vitumizi zinaweza kupata joto kubwa, kupinda,
na kuchomeka na kusababisha kifo au majeraha
mabaya.
• Vifaa vya elektroniki, pamoja na kebo na vizibo vya
kuunganisha, havifai kuwa na hitilafu.
1. Weka ving'ora vya kaboni monoksidi.
2. Unapoendesha jenereta ukitumia kebo ndefu,
hakikisha ipo mahali wazi, nje, angalau mita
6.1 mabla na mahali kuna watu na ekzosi ikiwa
umeelekezwa mbali.
3. Kebo ndefu zinazoelekea moja kwa moja hadi
ndani ya nyumba, na kuendesha vifaa vya ndani ya
nyumba HAIPENDEKEZWI.
1
7