Descargar Imprimir esta página

Briggs & Stratton 130000 Manual Del Operador página 40

Ocultar thumbs Ver también para 130000:

Publicidad

Idiomas disponibles
  • MX

Idiomas disponibles

  • MEXICANO, página 24
N. Chujio la Hewa (iwapo ipo)
O. Mafla (iwapo ipo)
Ishara za Kudhibiti Injini na Maana
Kasi ya Injini - HARAKA 
Kasi ya Injini - SIMAMA
Kuwasha Injini
Choki IMEFUNGWA
Kifuniko cha Mafuta
Kizima Mafuta -
KIMEFUNGULIWA
Kiwango cha Mafuta -
Upeo
Usijaze Kupita Kiasi
Uendeshaji
Mapendekezo ya Oili
Kiwango cha Oili: Tazama sehemu ya Vipimo.
NOTISI 
Injini hii ililetwa kutoka Briggs & Stratton bila oili. Watengenezaji au wauzaji vifaa
huenda waliongeza oili kwenye injini. Kabla ya kuwasha injini kwa mara ya kwanza,
hakikisha umekagua kiwango cha oili ni sahihi. Ongeza oili kama ilivyobainishwa na
maagizo kwenye mwongozo huu. Ukiwasha injini bila oili, injini itaharibika na haiwezi
kukarabatiwa chini ya waranti.
Tunapendekeza matumizi ya oili Zilizoidhinishwa na Hakikisho la Briggs & Stratton
kupata utendakazi bora. Oili nyingine za usafishaji zinaruhusiwa ikiwa zimebainishwa
kwa huduma ya SF, SG, SH, SJ au ya juu zaidi. Usitumie vitegemezi maalum. 
Tumia chati kuchagua mnato bora zaidi kwa hali joto ya nje inayotarajiwa. Injini katika
vifaa vingi vya nje zinafanya kazi vyema zikitumia oili ya 5W-30 Synthetic. Kwa vifaa
vinavyoendeshwa katika joto la juu, oili ya Vanguard
bora.
A
SAE 30 - Chini ya 40 °F (4 °C) matumizi ya SAE 30 yatasababisha ugumu wa
kuwasha.
B
10W-30 - Juu ya 80 °F (27 °C) matumizi ya 10W-30 yanaweza kusababisha
ongezeko la matumizi ya oili. Kagua kiwango cha oili mara nyingi.
C
5W-30
D
Sinthetiki 5W-30
E
®
Vanguard
 Synthetic 15W-50
Kagua Kiwango cha Oili
Kabla ya kukagua au kuongeza oili
Hakikisha injini inadumisha mizani.
Safisha vifusi kutoka kwenye eneo la kujazia oili.
40
Kasi ya Injini - POLEPOLE
WASHA - ZIMA
Kuwasha Injini
Choki IMEFUNGULIWA
Kizima Mafuta -
KIMEFUNGWA
®
 ili
®
15W-50 Synthetic inatoa ulindaji
Rejelea sehemu ya Vipimo ili kujua kiwango cha oili.
NOTISI 
Injini hii ililetwa kutoka Briggs & Stratton bila oili. Watengenezaji au wauzaji vifaa
huenda waliongeza oili kwenye injini. Kabla ya kuwasha injini kwa mara ya kwanza,
hakikisha umekagua kiwango cha oili ni sahihi. Ongeza oili kama ilivyobainishwa na
maagizo kwenye mwongozo huu. Ukiwasha injini bila oili, injini itaharibika na haiwezi
kukarabatiwa chini ya waranti.
1.
Ondoa kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 5) na upanguze kwa
kitambaa safi.
2.
Weka na ukaze kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 5).
3.
Ondoa kifaa cha kupima oili na ukague kiwango cha oili. Hakikisha kwamba
kiwango cha oili kiko juu ya alama inayoashiria kujaa (B, Kielelezo 5) kwenye kifaa
cha kupima kiwango cha oili.
4.
Iwapo kiwango cha oili kiko chini, polepole weka oili kwenye eneo la kujazia oili ya
injini (C, Kielelezo 5). Usiongoze oili nyingi kupita kiasi.
5.
Subiri dakika moja na ukague tena kiwango cha oili. Hakikisha kwamba kiwango
cha oili ni sahihi.
6.
Weka na ukaze kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 5).
Mfumo wa Ulinzi dhidi ya Oili Chache (iwapo upo)
Kihisio cha oili chache kimesakinishwa kwenye baadhi ya injini. Iwapo oili iko chini,
kihisio kitaonyesha mwangaza wa onyo au kuzima injini. Zima injini na ufuate hatua
zifuatazo kabla ya kuwasha injini.
Hakikisha injini haijainama.
Kagua kiwango cha oili. Rejelea sehemu ya Kagua Kiwango cha Oili.
Iwapo kiwango cha oili kiko chini, ongeza kiwango sahihi cha oili. Washa injini
na uhakikishe kwamba mwangaza wa onyo (iwapo upo) hauwashi.
Iwapo kiwango cha oili hakiko chini, usiwashe injini. Wasiliana na Muuzaji
Huduma Aliyeidhinishwa wa Briggs & Stratton ili kurekebisha tatizo hilo la oili.
Mapendekezo ya Mafuta
Mafuta ni lazima yatimize mahitaji haya:
Petroli safi, freshi, isiyo na risasi (unleaded).
Kiwango cha chini zaidi cha okteni 87/AKI 87 (91 RON). Matumizi katika
mwinuko wa juu, tazama hapa chini.
Petroli iliyo na hadi ethanoli 10% (gasoholi) inaruhusiwa.
NOTISI 
Usitumie petroli ambayo haijaidhinishwa, kama vile E15 na E85. Usichanganye oili
kwenye petroli au kurekebisha injini ili itumie mafuta mbadala. Matumizi ya mafuta
ambayo hayajaidhinishwa yataharibu vipengele vya injini, na haitakarabatiwa chini ya
waranti.
Ili kulinda mfumo wa mafuta kutokana na utengenezaji wa gundi, na ubabuzi,
changanya kiimarishaji mafuta bila alkoholi na tiba ya ethanoli ndani ya mafuta. Rejelea
sehemu ya Uhifadhi. Mafuta yote si sawa. Iwapo matatizo ya kuwasha au utendakazi
yatatokea, badilisha unakonunua mafuta au ubadilishe aina. Injini hii imeidhinishwa
kuendeshwa kutumia petroli. Mfumo wa kudhibiti mafukizo wa injini za kabureta ni EM
(Engine Modifications (Marekebisho ya Injini)). Mifumo ya kudhibiti mafukizo kwa injini
zilizo na unyonyaji mafuta kielektroniki ni ECM (Engine Control Module (Moduli ya
Kidhibiti Injini)), MPI (Multi Port Injection (Unyonyaji kwa Matundu Kadhaa)) na ikiwa ina
O2S (Oxygen Sensor (Sensa ya Oksijeni)).
Mwinuko wa Juu
Katika minuko zaidi ya fiti 5,000 (mita 1524), kiwango cha chini cha okteni 85 / AKI 85
(RON 89) cha petroli kinakubalika.
Kwa injini iliyo na kabureta, marekebisho ya mwinuko wa juu yanahitajika ili kudumisha
utendakazi. Uendeshaji bila marekebisho haya unaweza kusababisha kupunguka kwa
utendakazi, matumizi ya mafuta kuongezeka, na mafukizo kuongezeka. Wasiliana na
Mtoa Huduma wa Briggs & Stratton Aliyeidhinishwa kwa maelezo ya marekebisho ya
mwinuko wa juu. Uendeshaji injini katika mwinuko wa chini ya fiti 2,500 (mita 762) na
marekebisho ya mwinuko wa juu hayapendekezwi.
Kwa injini za Uingizaji Mafuta wa Kielektroniki (EFI), hakuna marekebisho ya mwinuko
wa juu yanahitajika.

Publicidad

loading

Este manual también es adecuado para:

250000