Descargar Imprimir esta página

Vanguard 25E300 Manual Del Operador página 42

Ocultar thumbs Ver también para 25E300:

Publicidad

Idiomas disponibles
  • MX

Idiomas disponibles

  • MEXICANO, página 20
Uendeshaji
ONYO 
Mvuke wa mafuta unaweza kushika moto na kulipuka kw aharaka sana. Moto au
mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Ukinusa gesi
Usiwashe injini.
Usiwashe swichi za kiumeme.
Usitumie simu katika eneo hilo.
Ondoka kwenye eneo hilo.
Wasiliana na idara ya wazima moto.
Unapoendesha kifaa
Usiinamishe injini au kifaa katika mkao unaosababisha mafuta kumwagika.
Unapohamisha kifaa hadi eneo nyingine
Hakikisha kwamba tangi la mafuta ni TUPU au kwamba vali ya kufunga mafuta
ipo katika eneo linaloonyesha IMEFUNGWA.
Kagua Kiwango cha Oili
Kabla ya kukagua au kuongeza oili
Hakikisha injini haijainama.
Safisha vifusi vyote kutoka kwenye eneo la oili.
Rejelea sehemu ya Vipimo ili kujua kiwango cha oili.
NOTISI 
Injini hii ililetwa kutoka Briggs & Stratton bila oili. Watengenezaji au wauzaji vifaa
huenda waliongeza oili kwenye injini. Kabla ya kuwasha injini kwa mara ya kwanza,
hakikisha umekagua kiwango cha oili ni sahihi. Ongeza oili kama ilivyobainishwa na
maagizo kwenye mwongozo huu. Ukiwasha injini bila oili, injini itaharibika na haiwezi
kukarabatiwa chini ya waranti.
1.
Ondoa kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, B, C, Kielelezo 4). Tumia kitambaa
kufuta oili kwenye kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, B, C).
2.
Weka kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, B, C, Kielelezo 4).
a.
Kifaa Kilicho Chini cha Kupima Kiwango cha Oili, iwapo kipo, (B, Kielelezo
4): Hakikisha kwamba alama zinazoashiria oili kujaa zilizo kwenye kifaa cha
kupima kiwango cha oili (B) zinaangalia juu ya injini.
b.
Kifaa Kifupi cha Kupima Kiwango cha Oili au Kifuniko cha Tundu la Kujazia
Oili, ikiwa kipo (C, Kielelezo 4): Weka na ukaze kifaa cha kupima kiwango cha
oili (C).
3.
Ondoa kifaa cha kupima kiwango cha oili tena (A, B, C, Kielelezo 4).
4.
Kagua kiwango cha oili. Hakikisha kwamba kiwango cha oili kiko juu ya alama
inayoashiria kujaa (D, Kielelezo 4).
5.
Iwapo kiwango cha oili kiko chini ongeza oili polepole kwenye tundu moja la kujazia
ooili ya injini (E, F, Kielelezo 5). Usiongoze oili nyingi kupita kiasi.
6.
Subiri dakika moja. Kagua tena kiwango cha oili. Hakikisha kwamba kiwango cha
oili ni sahihi.
7.
Weka kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, B, C, Kielelezo 4).
Mapendekezo ya Oili
Kiwango cha Oili: Rejelea sehemu ya Vipimo.
Tunapendekeza matumizi ya oili Zilizoidhinishwa na Hakikisho la Briggs & Stratton
kupata utendakazi bora. Oili nyingine za usafishaji zinaruhusiwa ikiwa zimebainishwa
kwa huduma ya SF, SG, SH, SJ au ya juu zaidi. Usitumie vitegemezi maalum.
Tumia chati kuchagua mnato bora zaidi kwa hali joto ya nje inayotarajiwa. Injini kwenye
vifaa vingi vya kutumiwa nje zinafanya kazi vyema zikitumia oili ya 5W-30 Synthetic.
Kwa vifaa vinavyoendeshwa katika joto la juu, oili ya Vanguard
inatoa ulindaji bora.
42
A
B
C
D
E
Mfumo wa Ulinzi dhidi ya Oili Chache (iwapo upo)
Kihisio cha oili chache kimesakinishwa kwenye baadhi ya injini. Iwapo oili iko chini,
kihisio kitaonyesha mwangaza wa onyo au kuzima injini. Zima injini na ufuate hatua
zifuatazo kabla ya kuwasha injini.
Mapendekezo ya Mafuta
Mafuta ni lazima yatimize mahitaji haya:
NOTISI 
Usitumie petroli ambayo haijaidhinishwa, kama vile E15 na E85. Usichanganye oili
kwenye petroli au kurekebisha injini ili itumie mafuta mbadala. Matumizi ya mafuta
ambayo hayajaidhinishwa yataharibu vipengele vya injini, na haitakarabatiwa chini ya
waranti.
Ili kulinda mfumo wa mafuta kutokana na utengenezaji wa gundi, na ubabuzi,
changanya kiimarishaji mafuta bila alkoholi na tiba ya ethanoli ndani ya mafuta. Rejelea
sehemu ya Uhifadhi. Mafuta yote si sawa. Iwapo matatizo ya kuwasha au utendakazi
yatatokea, badilisha unakonunua mafuta au ubadilishe aina. Injini hii imeidhinishwa
kuendeshwa kutumia petroli. Mfumo wa kudhibiti mafukizo wa injini za kabureta ni
EM (Engine Modifications (Marekebisho ya Injini)). Mifumo ya kudhibiti mafukizo kwa
injini zilizo na unyonyaji mafuta kielektroniki ni ECM (Engine Control Module [Moduli ya
Kidhibiti Injini]), MFI (Multi Port Fuel Injection [Unyonyaji Mafuta kwa Matundu Kadhaa]),
TBI (Throttle Body Fuel Injection [Unyonyaji Mafuta kwa Kifaa cha Kuingiza Hewa]) na
ikiwa ina O2S (Oxygen Sensor [Sensa ya Oksijeni]).
®
 ili
Mwinuko wa Juu
Katika minuko zaidi ya fiti 5,000 (mita 1524), kiwango cha chini cha okteni 85 / AKI 85
(RON 89) cha petroli kinakubalika.
Kwa injini iliyo na kabureta, marekebisho ya mwinuko wa juu yanahitajika ili kudumisha
utendakazi. Uendeshaji bila marekebisho haya unaweza kusababisha kupunguka kwa
®
15W-50 Synthetic
utendakazi, matumizi ya mafuta kuongezeka, na mafukizo kuongezeka. Wasiliana na
Mtoa Huduma wa Briggs & Stratton Aliyeidhinishwa kwa maelezo ya marekebisho ya
mwinuko wa juu. Uendeshaji injini katika mwinuko wa chini ya fiti 2,500 (mita 762) na
marekebisho ya mwinuko wa juu hayapendekezwi.
Kwa injini za Uingizaji Mafuta wa Kielektroniki (EFI), hakuna marekebisho ya mwinuko
wa juu yanahitajika.
SAE 30 - Chini ya 40 °F (4 °C) matumizi ya SAE 30 yatasababisha ugumu wa
kuwasha.
10W-30 - Juu ya 80 °F (27 °C) matumizi ya 10W-30 yanaweza kusababisha
ongezeko la matumizi ya oili. Kagua kiwango cha oili mara nyingi.
5W-30
Sinthetiki 5W-30
®
Vanguard
 Synthetic 15W-50
Hakikisha injini haijainama.
Kagua kiwango cha oili. Rejelea sehemu ya Kagua Kiwango cha Oili.
Iwapo kiwango cha oili kiko chini, ongeza kiwango sahihi cha oili. Washa injini
na uhakikishe kwamba mwangaza wa onyo (iwapo upo) hauwashi.
Iwapo kiwango cha oili hakiko chini, usiwashe injini. Wasiliana na Muuzaji
Huduma Aliyeidhinishwa wa Briggs & Stratton ili kurekebisha tatizo hilo la oili.
Petroli safi, freshi, isiyo na risasi (unleaded).
Kiwango cha chini zaidi cha okteni 87/AKI 87 (91 RON). Matumizi katika
mwinuko wa juu, tazama hapa chini.
Petroli iliyo na hadi ethanoli 10% (gasoholi) inaruhusiwa.

Publicidad

loading