Descargar Imprimir esta página

Vanguard 25E300 Manual Del Operador página 43

Ocultar thumbs Ver también para 25E300:

Publicidad

Idiomas disponibles
  • MX

Idiomas disponibles

  • MEXICANO, página 20
Ongeza Mafuta
ONYO 
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Unapoongeza mafuta
Zima injini. Kabla ya kufunua kifuniko, subiri angalau dakika mbili (2) ili
kuhakikisha injini imepoa.
Jaza tangi la mafuta ukiwa nje au katika eneo lenye hewa nyingi safi.
Usiweke mafuta mengi kupita kiasi kwenye tangi. Kwa ajili ya uvukizi wa mafuta,
usijaze hadi juu ya chini ya shingo la tangi la mafuta.
Weka mafuta mbali na spaki, moto ulio wazi, taa za gesi, joto, na vyanzo vingine
vya mwako.
Mara kwa mara kagua tundu la tangi, tangi la mafuta, kifuniko cha mafuta, na
mirija kama kuna nyufa na uvujaji. Badilisha sehemu zilizoharibika.
Mafuta yakimwagika, subiri mpaka yakauke kabla ya kuwasha injini.
1.
Safisha kifuniko cha mafuta kutokana na uchafu na vifusi. Ondoa kifuniko cha fueli.
2.
Jaza tangi la mafuta (A, Kielelezo 6) kwa mafuta. Kwa ajili ya uvukizi wa mafuta,
usijaze zaidi ya chini mwa shingo ya tangi la mafuta (B).
3.
Weka kifuniko cha mafuta.
Washa Injini
ONYO 
HATARI YA GESI YENYE SUMU. Eksozi ya injini ina kaboni monoksidi, gesi ya
sumu ambayo inaweza kukuua kwa dakika chache. Ingawa hauwezi kunusa
mafukizo yanayotolewa, bado unaweza kuvuta gesi hatari ya monoksidi ya
kaboni. Ukihisi mgonjwa, kizunguzungu, au mchovu unapotumia bidhaa hii,
nenda kwenye eneo lenye hewa safi MARA MOJA. Mwone daktari. Huenda ukawa
umeathiriwa na sumu ya kaboni monoksidi.
Gesi ya kaboni monoksidi inaweza kujikusanya katika maeneno yenye watu.
Ili kupunguza hatari ya gesi ya kaboni monoksidi, tumia bidhaa hii TU nje na
mbali na madirisha, milango na matundu.
Sakinisha ving'ora vya kutambua uwepo wa kaboni monoksidi vinavyotumia
betri pamoja na hifadhi ya betri kama ilivyobainishwa na maagizo ya
mtengenezaji. Ving'ora vya moshi haviwezi kutambua gesi ya kaboni
monoksidi.
USIENDESHEE bidhaa hii ndani ya nyumba, gereji, vyumba vya chini ya ardhi,
ubati, vibanda, au majengo mengine yaliyobanwa hata kama unatumia viyoyozi
ama kufungua milango na madirisha ili hewa safi iingie. Baada ya kuendesha
bidhaa hii, gesi ya kaboni monoksidi inaweza kukusanyika kwa haraka katika
maeneo haya na inaweza kukwama kwa saa kadhaa.
KILA WAKATI weka bidhaa hii upande ambao upepo unaelekea na uelekeze
ekzosi ya injini mbali na maeneo yenye watu.
ONYO 
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Unapowasha injini
Hakikisha kwamba plagi ya spaki, mafla, kifuniko cha mafuta, na kisafishaji
hewa (iwapo kipo) vimefungwa vizuri.
Usishtue injini wakati plagi ya spaki imeondolewa.
Ikiwa injini imefurika, choki (iwapo ipo) imewekwa kwenye eneo la
IMEFUNGULIWA au ENDESHA. Songeza kidhibiti injini (iwapo kipo) hadi
kwenye eneo la HARAKA na ushtue hadi injini iwake.
Iwapo kuna gesi asili au ya LP iliyovuja katika eneo hilo, usiwashe injini.
Kwa sababu mvuke unaweza kuwaka moto, usitumie firigiji zilizoshinikizwa za
kuwasha.
ONYO 
Sehemu zinazozunguka zinaweza kunasa mikono, miguu, nywele, nguo, au
vifuasi na kupelekea kukatwa viungo au ngozi vibaya.
Endesha kifaa vilinzi vikiwa vimesakinishwa vizuri.
Weka mikono na miguu mbali na sehemu zinazozunguka.
Vua vipuli na uhakikishe kwamba nywele ndefu ziko mbali na sehemu
zinazozunguka.
Usivae nguo zilizolegea au vipengee vinavyoweza kushikwa.
ONYO 
Uvutaji nyuma wa haraka wa kamba ya kianzishaji (kuvuta nyuma kwa haraka)
kutavuta mkono wako kuelekea kwenye injini haraka kuliko unavyoweza
kuachilia. Kunaweza kusababisha mifupa kuvunjika, michubuko amu maungo
kuteguka.
Ili kuzuia kuvuta nyuma kwa haraka wakati wa kuwasha injini, vuta kamba ya
kianzishaji polepole hadi uhisi upinzani na kisha uvute haraka.
kabla ya kuwasha injini, ondoa vifaa vyote vya nje/mizigo yote ya injini.
Hakikisha kwamba vijenzi vya kifaa kilichounganishwa moja kwa moja kama
vile, lakini sio tu, bapa, mashine ya kusogeza majimaji, makapi, na proketi,
vimeambatishwe salama.
KUMBUKA: Kifaa chako kinaweza kuwa na vidhibiti vya mbali. Rejelea mwongozo wa
kifaa ili utambue mahali ambapo vidhibiti vya mbali viko na jinsi ya kuvitumia.
Uwashaji wa Umeme
1.
Kagua kiwango cha oili. Rejelea sehemu ya Kagua Kiwango cha Oili.
2.
Zima vidhibiti vya uendeshaji kifaa, iwapo vipo.
3.
Sogeza vali ya kufunga mafuta, iwapo ipo, hadi kwenye eneo linaloonyesha
FUNGUA.
4.
Geuza swichi ya ufunguo (A, Kielelezo 7) hadi eneo linaloonyesha ANZISHA.
NOTISI Unapoachilia swichi ya ufunguo (A, Kielelezo 7), ufunguo utaenda kwenye hadi
eneo linaloonyesha WASHA. Injini itaendelea kuwaka isipokuwa ijini igurumishwe. Ili
kuzima mtindo huu wa kuwaka geuza swichi ya ufunguo (A) hadi eneo linaloonyesha
ZIMA. Injini ikikosa kuwasha, fanya hatua zifuatazo.
5.
Hakikisha kwamba swichi ya ufunguo (A, Kielelezo 7) iko kwenye hadi eneo
linaloonyesha ZIMA. Subiri sekunde mbili.
6.
Geuza swichi ya ufunguo (A, Kielelezo 7) hadi eneo linaloonyesha ANZISHA.
7.
Injini ikikosa kuwaka, achana na mtindo wa kuwaka na uwasiliane na Mtoa Huduma
Aliyeidhinishwa wa Briggs & Stratton.
Uwashaji wa Kuvuta Kamba
NOTISI Uwashaji wa Umeme ndio mbinu inayopendekezwa ya kuwasha injini yako.
1.
Kagua kiwango cha oili ya injini. Rejelea sehemu ya Kagua Kiwango cha Oili.
2.
Zima vidhibiti vya uendeshaji kifaa, iwapo vipo.
3.
Hakikisha kwamba injini imeunganishwana betri ya volti 12 iliyo na chaji.
4.
Sogeza vali ya kufunga mafuta, iwapo ipo, hadi kwenye eneo linaloonyesha
FUNGUA.
5.
Geuza swichi ya ufunguo (A, Kielelezo 8) hadi eneo linaloonyesha WASHA. Kisha,
vuta kishikio cha kamba ya kiazishaji (B).
Zima Injini
1.
Geuza swichi ya ufunguo (A, Kielelezo 7) hadi eneo linaloonyesha ZIMA.
2.
Ondoa ufunguo. Weka mahali salama mbali na watoto.
3.
Baada ya injini kuzima, sogeza vali ya kufunga mafuta, iwapo ipo, hadi kwenye
eneo linaloonyesha IMEFUNGWA.
Taa ya Kagua Injini
Taa ya kagua injini (B, Kielelezo 7) inaashiria tatizo kwenye injini. Ikiwa taa ya
kagua injini IMEWASHA wakati injini inatumika, zungumza na Muuzaji Huduma
Aliyeidhinishwa wa Briggs & Stratton ili kusuluhisha tatizo punde iwezekanavyo au
wakati utakapokamilisha kazi yako. Ikiwa taa ya kagua injini IMEWASHA na injini
imezima otomatiki, chukua hatua zifuatazo:
1.
Hakikisha injini haijainama.
2.
Kagua kiwango cha oili. Rejelea sehemu ya Kagua Kiwango cha Oili.
3.
Washa injini. Rejelea sehemu ya Washa Injini.
4.
Ikiwa taa ya kagua injini itaendelea kukaa ikiwa IMEWASHA na injini iendelee
kuzima otomatiki, usitumie injini. Wasiliana na Muuzaji Huduma Aliyeidhinishwa wa
Briggs & Stratton mara moja ili kurekebisha tatizo hilo.
Udumishaji
Maelezo ya Udumishaji
ONYO 
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Wakati wa huduma ya udumisha ikiwa ni muhimu kuinamisha kifaa, ikiwa tangi la
mafuta limeshikana na injini, hakikikisha kwamba ni tupu na upande wa plagi ya spaki
uko juu. Ikiwa tangi la mafuta si tupu, mafuta yanaweza kuvuja na kusababisha moto au
mlipuko. Ikiwa injini imeinama katika mkao tofauti, haitaguruma kwa urahisi kwa sababu
ya kuchafuka kwa chujio la hewa au plagi ya spaki kwa oili au mafuta.
43

Publicidad

loading