Briggs & Stratton Vanguard 290000 Manual Del Operario página 46

Ocultar thumbs Ver también para Vanguard 290000:
Tabla de contenido

Publicidad

Idiomas disponibles
  • MX

Idiomas disponibles

  • MEXICANO, página 15
Usijaze tangi la mafuta kupita kiasi. Ili uruhusu uvukizi wa mafuta, usijaze hadi juu
ya chini ya shingo la tangi la mafuta.
Weka mafuta mbali na spaki, moto ulio wazi, taa za gesi, joto, na vyanzo vingine
vya mwako.
Kagua tundu za mafuta, tangi, kifuniko kama kuna nyufa na uvujaji. Badilisha kama
itahitajika.
Mafuta yakimwagika, subiri mpaka pale ambapo yatayeyuka kabla ya kuwasha injini.
Wakati wa Kuwasha Injini
Hakikisha kwamba plagi ya spaki, mafla, kifuniko cha mafuta, na kisafishaji hewa
(iwapo kipo) vimefungwa na kukazwa.
Usiwashe injini wakati kiziba cheche kimeondolewa.
Injini ikifurika, weka choki (ikiwa ipo) katika eneo la kuonyesha FUNGUA / ENDESHA
(OPEN / RUN), songeza kidhibiti injini (ikiwa kipo) hadi eneo la kuonyesha HARAKA
(FAST) na ushtue hadi injini iwake.
Wakati wa Kuendesha Kifaa
Usiinamishe injini au kifaa katika mkao unaosababisha mafuta kumwagika.
Usijaribu kutoruhusu hewa kuingia kwenye kabureta ili kusimamisha injini.
Usiwashe au kuendesha injini kamwe wakati uunganishaji wa kisafishaji hewa (iwapo
kipo) au chujio la hewa (iwapo lipo) vimeondolewa.
Wakati wa Kubadilisha Oili
Ukimwaga oili kutoka kwenye tundu la juu la kujazia oili, ni lazima tangi la mafuta
liwe tupu au mafuta yanaweza kuvuja na kusababisha moto au mlipuko.
Wakati wa Kuinamisha Kifaa ili Kutekeleza Udumishaji
Wakati unapotekeleza udumishaji unaohitaji kitengo kuinamishwa, tangi la mafuta,
iwapo limewekwa kwenye injini, lazima liwe tupu au mafuta yanaweza kuvuja na
kusababisha moto au mlipuko.
Wakati wa Kusafirisha Kifaa
Safirisha tangi la mafuta likiwa TUPU au vali ya kufungia ikiwa katika eneo la
kuonyesha IMEFUNGWA (CLOSED).
Wakati wa Kuhifadhi Mafuta Au Kifaa Kilicho na Mafuta Kwenye Tangi
Hifadhi mbali na tanuu, stovu, hita za kuchemshia maji, au vitu vingine ambavyo vina
taa za moto au vyanzo vya mwako kwa sababu vinaweza kuwasha moto kwenye
mvuke wa mafuta.
Onyo
Kuwasha injini kunatoa cheche.
Cheche zinaweza kuwasha gesi zilizo karibu ambazo zina uwezo wa kuwaka
moto.
Inaweza kusababisha mlipuko na moto.
Iwapo kuna gesi asili au ya LP iliyovuja katika eneo, usiwashe injini.
Usitumie majimaji yaliyoshinikizwa ya kuwasha kwa sababu mvuke unaweza kuwaka
moto.
Onyo
HATARI YA GESI YENYE SUMU. Eksozi ya injini ina monoksidi ya kaboni, gesi ya
sumu ambayo inaweza kukuua wewe kwa dakika chache. HUWEZI kuiona, kuinusa
wala kuionja. Hata kama huwezi kunusa mafukizo yanayotolewa, bado unaweza
kuvuta gesi ya monoksidi ya kaboni. Ukianza kuhisi mgonjwa, kizunguzungu, au
mchovu wakati unatumia bidhaa hii, nenda kwenye eneo lenye hewa safi MARA
MOJA. Mwone daktari. Huenda ukawa umeathiriwa na sumu ya kaboni monoksidi.
Tumia bidhaa hii NJE PEKEE mbali na madirisha, milango na matundu ili kupunguza
hatari ya gesi ya kaboni monoksidi kukusanyika na uwezekano wa kuwa inasambazwa
kuelekea maeneo ya nje.
Sakinisha ving'ora vya kutambua uwepo wa monoksidi ya kaboni vinavyotumia betri
pamoja na hifadhi ya betri kulingana na maagizo ya mtengenezaji. Ving'ora vya
moshi haviwezi kutambua gesi ya monoksidi ya kaboni.
USIENDESHEE bidhaa hii ndani ya nyumba, gereji, vyumba vya chini ya ardhi, ubati,
vibanda, au majengo mengine yaliyobanwa hata kama unatumia viyoyozi ama
kufungua milango na madirisha ili hewa safi iingie. Gesi ya kaboni monoksidi inaweza
46
kukusanyika kwa haraka katika maeneo haya na inaweza kukwama kwa saa nyingi,
hata baada ya bidhaa hii kuzimwa.
KILA WAKATI weka bidhaa hii upande ambao upepo unatelekea na uelekeze ekzosi
ya injini mbali na maeneo yenye watu.
Onyo
Uvutaji nyuma kwa haraka wa kamba ya kianzishaji (kuvuta nyuma kwa haraka)
kutavuta mkono kuelekea kwenye injini haraka kuliko unavyoweza kuachilia.
Inaweza kupelekea mifupa kuvunjika, michubuko au kuteguka maungo.
Wakati wa kuwasha injini, kuzuia kurudi nyuma kwa haraka, vuta kamba ya kianzishi
polepole hadi uhisi upinzani na kisha uvute haraka ili kuzuia kuvuta nyuma kwa
haraka.
Ondoa vifaa cha nje/ mizigo yote ya injini kabla ya kuwasha injini.
Vijenzi vya kifaa kilichounganishwa moja kwa moja kama vile, lakini visivyo tu, bapa,
mashine ya kusogeza majimaji, makapi, proketi, n.k., lazima viambatishwe salama.
Onyo
Sehemu zinazozunguka zinaweza kugusana au kunasa mikono, miguu, nywele,
nguo, au vifuasi.
Inaweza kusababisha ukataji wa viungo wenye kiwewe au majeraha mabaya ya
ukataji ngozi.
Endesha kifaa na vilinzi vikiwa karibu.
Weka mikono na miguu mbali na sehemu zinazozunguka.
Funga nywele ndefu na uondoe mapambo.
Usivae nguo zisizokubana vizuri, kamba za nguo zinazomwayamwaya au vipengee
vinavyoweza kushikwa.
Onyo
Injini zinazoguruma zinatoa joto. Sehemu za injini, hususan mafla, huwa moto
zaidi.
Unaweza kuchomeka vibaya sana ukiigusa.
Uchafu unaoweza kuwaka moto, kama vile majani, nyasi, brashi n.k. unaweza
kushika moto.
Ruhusu mafla, silinda ya injini na mapezi yapoe kabla ya kugusa.
Ondoa uchafu uliokusanyika kutoka kwenye eneo la mafla na eneo la silinda.
Ni ukiukaji wa Kanuni za Rasilimali za Umma za California, Sehemu ya 4442, kutumia
au kuendesha injini katika eneo linalozungukwa na msitu, lililozungukwa na brashi,
au lililo na nyasi isipokuwa mfumo wa ekzosi una kishika spaki, kama ilivyobainishwa
katika Sehemu ya 4442, kilichodumishwa katika hali fanisi ya kufanya kazi. Mamlaka
mengine ya Majimbo au shirikisho yanaweza kuwa na sheria sawia. Wasiliana na
mtengenezaji asilia wa kifaa, muuzaji rejareja, au muuzaji ili kupata kishika spaki
kilichobuniwa kwa ajili ya mfumo wa ekzosi uliowekwa kwenye injini hii.
Onyo
Spaki zinazotokea bila kusudi zinaweza kusababisha moto au mrusho wa stima.
Uwashaji usiokusudiwa unaweza kusababisha kunaswa, kukatwa kwa viungo kwa
kiwewe, au majeraha mabaya ya ukataji wa ngozi.
Hatari ya moto
Kabla ya kutekeleza marekebisho au ukarabati:
Tenganisha waya ya kizibo cha cheche na iweke mbali na kizibo cha cheche.
Tenganisha betri katika kichwa cha hasi (injini tu zenye kianzishi cha umeme).
Tumia zana sahihi pekee.
Usihitilafiane na springi ya kidhibiti, viungo, au viungo vingine ili kuongeza kasi ya
injini.
Sehemu za kubadilishia ni lazima ziwe za aina sawia na ziwekwe katika eneo sawia
kama sehemu asilia. Sehemu nyingine huenda zisitfanye kazi kwa njia sawia,
zinaweza kuharibu kifaa, na inaweza kusababisha majeraha.
VanguardEngines.com

Publicidad

Tabla de contenido
loading

Este manual también es adecuado para:

Vanguard 300000Vanguard 350000Vanguard 380000

Tabla de contenido