Mfumo wa Ulinzi wa Chini wa Mafuta
(iwapo upo)
Baadhi ya modeli zina kihisio cha mafuta ya chini. Iwapo mafuta yako chini, kihisio aidha
kitaamilisha mwangaza wa tahadhari au kusimamisha injini. Simamisha injini na ufuate
hatua hizi kabla ya kuwasha tena injini.
•
Hakikisha injini iko katika sehemu laini.
•
Angalia kiwango cha mafuta. Tazama sehemu Kuangalia Kiwango cha Mafuta.
•
Iwapo kiwango cha mafuta kiko chini, ongeza kiwango sahihi cha mafuta. Washa
injini na uhakikishe mwangaza wa tahadhari (iwapo upo) haujaamilishwa.
•
Iwapo kiwango cha mafuta hakiko chini, usiwashe injini. Wasiliana na Mtoa Huduma
wa Briggs & Stratton Aliyeidhinishwa ili kurekebisha matatizo ya mafuta.
Mapendekezo ya Fueli
Lazima fueli ikithi mahitaji haya:
•
Petroli safi, freshi, yasiyo na isiyo na lead.
•
Kiwango cha chini cha 87 okteni/87 AKI (91 RON). Matumizi ya mwinuko wa juu,
tazama hapa chini.
•
Petroli iliyo na hadi ethanoli 10% (gasohol) inakubalika.
Notisi
Usitumie petroli isiyoidhinishwa, kama vile E15 na E85. Usichanaganye mafuta
kwenye petroli au kurekebisha injini ili kuendesha fueli mbadala. Usitumie fueli
isiyoidhinishwa itaharibu vipengele vya injini, ambavyo havitashughulikiwa chini ya
udhamini.
Ili kulinda mfumo wa fueli kutokana na utengenezaji wa gundi, changanya kiimarishaji cha
fueli kwenye fueli. Tazama Hifadhi . Fueli zote sio sawa. Iwapo matatizo ya kuanza au
utendakazi yatatokea, badilisha mtoaji fueli au badilisha chapa. Injini hii imeidhinishwa
kuendesha kutumia petroli. Mfumo wa kudhibiti uchafuzi wa injini hii ni EM (Marekebisho
ya Injini).
Mwinuko wa Juu
Katika mwinuko wa zaidi ya futi 5,000 (mita1524), kiwango cha chini cha okteni 85 /85 AKI
(89 RON) petroli inakubaliwa.
Kwa injini iliyo na kabureta, marekebisho ya mwinuko wa juu yanahitajika ili kudumisha
utendakazi. Oparesheni bila marekebisho unaweza kusababisha kupunguka kwa
utendakazi, matumizi ya fueli yalioongezeka, na uchafuzi ulioongezeka. Wasiliana na Mtoa
Huduma wa Briggs & Stratton Aliyeidhibishwa kwa maelezo ya marekebisho ya mwinuko
wa juu. Oparesheni wa injini katika mwinuko wa chini ya futi 2,500 (mita 762) na
marekebisho ya mwinuko wa juu hayapendekezwi.
Kwa injini za Uinjizaji wa Fueli wa Kielektriki (EFI), hakuna marekebisho ya mwinuko wa
juu yanahitajika.
Ongeza Mafuta
Tazama Kelelezo: 5
Onyo
Fueli na mvuke wako unawaka na kulipuka haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka vikali au kifo.
Wakati wa kuongeza fueli
•
Zima injini na uruhusu injini kupoa angalau dakika 2 kabla ya kuondoa kifuniko cha
fueli.
•
Jaza tangi la fueli nje au katika eneo linaruhusu hewa kuingia vizuri.
•
Usijaze tangi la fueli kupita kiasi. Ili kuruhusu upanukaji wa fueli, usijaze kupita chini
ya shingo la tangi la fueli.
•
Hifadhi fueli mbali na cheche, miale iliyo wazi, taa za mwongozo, joto na vyanzo
vingine vya uwakaji.
•
Angalia tundu, tangi, kifuniko na kurekebisha mara kwa mara kwa nyufa na uvujaji.
Badilisha ikiwezekana.
•
Iwapo fueli itamwagika, subiri hadi ivukize kabla ya kuwasha injini.
1.
Safisha kifuniko cha fueli kutokana na uchafu. Ondoa kifuniko cha fueli.
2.
Jaza tangi la fueli kwa fueli (A, Kielelezo 5). Ili kuruhusu upanuzi wa fueli, usijaze
juu ya chini ya shingo la tangi la fueli (B).
3.
Sakinisha upya kifuniko cha fueli.
Washa na Uzime Injini
Tazama Kielelezo: 6
48
Washa Injini
Onyo
Mafuta na mvuke wake unaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha majeraha mabaya ya kuchomeka au kifo.
Wakati wa Kuwasha Injini
•
Hakikisha kwamba plagi ya spaki, mafla, kifuniko cha mafuta na kisafishaji hewa
(iwapo kipo) vimefungwa na kulindwa.
•
Usishtue injini wakati plagi ya spaki imeondolewa.
•
Injini ikifurika, weka choki (ikiwa ipo) katika eneo la kuonyesha FUNGUA / ENDESHA
(OPEN / RUN), sogeza kidhibiti injini (ikiwa kipo) hadi eneo la kuonyesha HARAKA
(FAST) na ushtue hadi injini iwake.
Onyo
HATARI YA GESI YENYE SUMU. Eksozi ya injini ina monoksidi ya kaboni, gesi ya
sumu ambayo inaweza kukuua wewe kwa dakika chache. HUWEZI kuiona, kuinusa
wala kuionja. Hata kama huwezi kunusa mafukizo yanayotolewa, bado unaweza
kuvuta gesi ya monoksidi ya kaboni. Iwapo utaanza kuhisi mgonjwa, kisunzi , au
mchovu wakati unatumia bidhaa hii, izime na uende eneo lenye hewa safi MARA
MOJA. Mwone Daktari. Huenda ukawa umeathiriwa na sumu ya monoksidi ya
kaboni.
•
Tumia bidhaa hii nje PEKE YAKE, mbali na madirisha, milango na matundu ya hewa
ili kupunguza hatari ya gesi ya monoksidi ya kaboni kukusanyika na uwezekano wa
kuwa inasambazwa kuelekea maeneo yenye watu.
•
Weka ving'ora vya kutambua uwepo wa monoksidi ya kaboni vinavyotumia betri
pamoja na betri ya ziada kulingana na maagizo ya mtengenezaji. Ving'ora vya moshi
haviwezi kutambua gesi ya kaboni monoksidi.
•
USIENDESHEE bidhaa hii ndani ya nyumba, gereji, vyumba vya chini ya ardhi, ubati,
vibanda, au majengo mengine yaliyobanwa hata kama unatumia viyoyozi ama
umefungua milango na madirisha ili hewa safi iingie. Gesi ya monoksidi ya
kaboniinaweza kukusanyika kwa haraka katika maeneo haya na inaweza kusalia
hewani kwa saa nyingi, hata baada ya bidhaa hii kuzimwa.
•
KILA WAKATI weka bidhaa hii upande ambao upepo unaelekea na uelekeze ekzosi
ya injini mbali na maeneo yenye watu.
Notisi
Injini hii ililetwa kutoka Briggs & Stratton bila oili. Kabla ya kuwasha injini,
hakikisha umeongeza oili kulingana na maagizo yaliyo kwenye mwongozo huu. Iwapo
utawasha injini bila oili, itaharibika hadi kushindwa kukarabatiwa na hutafidiwa chini ya
udhamini huu.
Tambua Mfumo wa Kuwasha
Kabla ya kuwasha injini, ni lazima utambue aina ya mfumo wa kuwasha unaotumika katika
injini yako. Injini yako ina mojawapo ya aina zifuatazo.
•
Mfumo wa Elektroniki wa Kudhibiti Mafuta: Mfumo huu una Kitengo cha Udhibiti
cha Elektroniki kinachofuatilia hali ya injini na halijoto. Aina hii haina choki au prima
ya kuendesha.
•
Mfumo wa Choki: Mfumo huu una choki ya kutumiwa kuwasha injini katika halijoto
baridi. Baadhi ya aina ya bidhaa hii zitakuwa na kidhibiti cha choki tofauti huku aina
zingine zitakuwa na muunganiko wa kidhibiti cha choki na cha injini. Aina hii haina
prima.
Ili kuwasha injini yako, fuata maelekezo ya aina yako ya mfumo wa kuwasha.
Kumbuka: Kifaa kinaweza kuwa na vidhibiti vya mbali. Tazama mwongozo wa kifaa ili
utambue mahali ambapo vidhibiti vya mbali viko na jinsi ya kuvitumia..
Mfumo wa Elektroniki wa Kudhibiti Fueli
1.
Angalia mafuta ya injini. angalia Angalia Kiwango cha Mafuta sehemu.
2.
Hakikisha vidhibiti vya kiendeshaji cha kifaa, iwapo vipo, vimetenganishwa.
3.
Weka kizima fueli (A, Kielelezo 6), iwapo kipo, kwenye eneo la KUFUNGUA .
4.
Sukuma swichi ya kusimamisha (F, Kielelezo 6), iwapo ipo, kwenye eneo la
KUWASHA .
5.
Sogeza kidhibiti cha transfoma ndogo (B, Kielelezo 6), iwapo kipo, kwenye eneo la
HARAKA . Endesha injini ikiwa katika eneo la HARAKA.
6.
Rejesha nyuma Anza, iwapo kuna swichi ya ufunguo: Weka swichi ya ufunguo
(D, Kielelezo 6) kwenye eneo la KUWASHA.
7.
Vingirisha Anza, iwapo ipo: Shikilia kwa nguvu mshikio wa waya wa stata (E,
Kielelezo 6). Vuta mshikio wa kamba ya stata polepole hadi uhisi upinzani, kisha
vuta haraka.
VanguardEngines.com