Masharti Wastani ya Hakikisho
Jina la Bidhaa
Vanguard™; Msururu wa Kibiashara
Injini Zenye Mkono wa Kalibu ya Chuma ya Dura-Bore™
Injini Nyingine Zote
1
Haya ni masharti yetu wastani ya hakikisho, lakini mara kwa mara huenda kukawa
na vipengele vya ziada vinavyosimamiwa na hakikisho ambavyo havikusimamiwa
wakati wa uchapishaji. Ili kupata orodha ya masharti ya sasa ya hakikisho la injini
yako, nenda kwenye BRIGGSandSTRATTON.com au uwasiliane na Muuzaji Huduma
wako Aliyeidhinishwa wa Briggs & Stratton.
2
Hakuna hakikisho kwa injini za vifaa vilivyotumiwa kutoa nishati badala ya kifaa
kinachofaa; jenereta ya akiba kwa madhumuni ya kibiashara, magari ya kubebea
mizigo yanayozidi 25 MPH, au injini zinazotumiwa katika mashindano ya mbio au
kwenye viwanja vya kibiashara au vya kukodishwa.
3
Vanguard imesakinishwa kwenye jenereta za akiba: Matumizi ya kibinafsi ya miezi
24, hakuna hakikisho kwa matumizi ya kibiashara. Msururu wa Kibiashara wenye
tarehe ya kutengenezwa ya kabla ya Julai 2017: Matumizi ya kibinafsi ya miezi 24,
matumizi ya kibiashara ya miezi 24.
4
Nchini Australia - Bidhaa zetu huja na hakikisho ambalo haziwezi kutojumuishwa
chini ya Sheria ya Mtumiaji ya Australia. Una haki ya kubadilishiwa au kurudishiwa
pesa kwa ajili ya hitilafu kuu au fidia kwa uharibifu au hasara nyingine yoyote ya siku
za usoni. Pia una haki ya bidhaa kufanyiwa ukarabati au kubadilishwa endapo bidhaa
hazitakuwa za ubora unaokubaliwa na hitilafu haimaanishi kuharibika kwa njia kubwa.
Ili kupata huduma ya hakikisho, tafuta Muuzaji Huduma Aliyeidhinishwa aliye karibu
zaidi nawe kwenye ramani yetu ya kutafuta wauzaji kwenye
BRIGGSandSTRATTON.COM, au kwa kupiga simu kwa nambari 1300 274 447, au
kwa kutuma barua pepe kwa salesenquiries@briggsandstratton.com.au, au kutuma
barua kwa Briggs & Stratton Australia PtyLtd, 1 Moorebank Avenue, Moorebank,
NSW, Australia, 2170.
Kipindi cha hakikisho kinaanzia tarehe ya ununuzi wa mtumiaji wa kwanza wa rejareja au
wa kibiashara. "Matumizi ya kibinafsi" inamaanisha matumizi ya kibinafsi ya nyumbani ya
mtumiaji wa rejareja. "Matumizi ya kibiashara" inamaanisha matumizi mengine yote,
yakijumuisha matumizi kwa madhumuni ya kibiashara, ya kuzalisha mapato au ya
kukodisha. Pindi tu injini inapopitia matumizi ya kibiashara, baada ya hapo itazingatiwa
kuwa injini ya matumizi ya kibiashara kwa ajili ya hakikisho hili.
Hifadhi risiti yako ya ushahidi wa ununuzi. Ukikosa kutoa ushahidi wa tarehe ya
kwanza ya ununuzi wakati huduma ya hakikisho inapoombwa, tarehe ya utengenezaji
wa bidhaa itatumiwa kung'amua kipindi cha hakikisho. Usajili wa bidhaa hauhitajiki
ili kupata huduma ya hakikisho kwa bidhaa za Briggs & Stratton.
Kuhusu Hakikisho Lako
Hakikisho hili lenye kipimo linasimamia tu nyenzo zinazohusiana na injini na/au utendakazi,
na sio kubadilishiwa au kurudishiwa pesa ulizonunua kifaa ambacho kina injini husika.
Udumishaji, uimarishaji, marekebisho ya mara kwa mara au kuchakaa na kuchanika kwa
kawaida hazijasimamiwa na hakikisho hili. Vile vile, hakikisho halitumiki ikiwa injini
imehitilafiwa au kubadilishwa au ikiwa nambari tambulishi ya injini imeharibiwa ua
kuondolewa. Hakikisho hili halisimamii uharibifu kwenye injini au matatizo ya utendakazi
wa injini yanayosababishwa na:
1.
Matumizi ya sehemu ambazo si sehemu halisi za Briggs & Stratton;
2.
Kuendesha injini zilizo na oili isiyotosha, chafu, au ya ubora usio sahihi;
3.
Matumizi ya mafuta machafu au yaliyoharibika, petroli yaliyotengenezwa kwa zaidi
ya 10% ya ethanoli, au matumizi ya mafuta kama vile petroli iliyoevuka au gesi asili
kwenye injini ambazo hazijaundwa/kutengenezwa tangu mwanzo na Briggs & Stratton
kuendeshwa kwa mafuta kama hayo;
4.
Uchafu ulioingia kwenye injini kwa sababu ya udumishaji kwa kutumia kisafishaji
hewa kisichofaa au ufunganishaji mbaya;
5.
Kugonga kitu kwa visu vya kukata vya mashine ya kukatia nyasi, adapta, impela au
vifaa vingine vya shafti kombo ambavyo vimelegea au havijawekwa ifaavyo au ukazaji
wa v-belt kupita kiasi;
6.
Sehemu au vifaa vinavyohusiana kama vile klachi, gia, vidhibiti vya kifaa, nk.,
ambavyo havijatolewa na Briggs & Stratton;
7.
Joto kupita kiasi kutokana na vipande vya nyasi, uchafu na vifusi, au viota vya panya
vinavyoziba au kufunika vifaa vya kupoesha au eneo la gurudumu la kuongeza kasi,
au kuendesha injini bila uingizaji hewa wa kutosha;
8.
Mtetemo kupita kiasi kwa ajili ya kasi kupita kiasi, uwekaji injini ikilegea, visua kukata
au impele ambazo zimelegea au havijasawazishwa, au uunganishaji vibaya wa
vipengele vya vifaa kwenye shafti kombo;
9.
Matumizi mabaya, ukosefu wa udumishaji wa mara kwa mara, usafirishaji,
ushughulikiaji, au uwekaji injini vibaya.
Huduma ya hakikisho inapatikana tu kupitia Wauzaji Huduma Walioidhinishwa wa
Briggs & Stratton. Tafuta Muuzaji Huduma Aliyeidhinishwa aliye karibu zaidi nawe
kwenye ramani yetu ya kutafuta wauzaji kwenye BRIGGSandSTRATTON.COM au
kwa kupiga simu kwa nambari 1-800-233-3723 (nchini Marekani).
1, 2, 3
Matumizi ya
Matumizi ya
Kibinafsi
Kibiashara
3
Miezi 36
Miezi 36
Miezi 24
Miezi 12
Miezi 24
Miezi 3
80004537 (Rev. D)
53