Briggs & Stratton 110000 Manual Del Operario página 50

Ocultar thumbs Ver también para 110000:
Tabla de contenido

Publicidad

Idiomas disponibles
  • MX

Idiomas disponibles

  • MEXICANO, página 16
Onyo
Uvutaji nyuma kwa haraka wa kamba ya kianzishaji (kuvuta nyuma kwa haraka) kutavuta
mkono wako kuelekea kwenye injini haraka zaidi kuliko unavyoweza kuachilia. Inaweza
kupelekea mifupa kuvunjika, michubuko au kuteguka maungo. Wakati wa kuwasha
injini, vuta kamba ya kianzishaji polepole hadi uhisi inakuwa gumu kuvuta na kisha uvute
kwa haraka ili kuzuia kuvutwa nyuma kwa haraka.
8.
Kianzishaji kwa Umeme, iwapo kipo: Geuza swichi ya kianzishaji kwa umeme
hadi eneo la kuonyesha WASHA / ANZA (ON / START).
Notisi
Ili kurefusha muda wa kianzishaji, tumia misururu mifupi ya kuanzisha (upeo
wa sekunde tano). Subiri dakika moja kati ya misururu ya kuanzisha.
Kumbuka: Injini ikikosa kuwasha baada ya majaribio kadhaa, wasiliana na mtoa huduma
wako wa ndani au nenda kwenye BRIGGSandSTRATTON.com au upige simu kwa 1-
800-233-3723 (nchini Marekani).
Mfumo wa Choki
1.
Kagua oili ya injini. Tazama sehemu ya Kagua Kiwango cha Oili .
2.
Hakikisha vidhibiti vya uendeshaji kifaa, iwapo vipo, vimezimwa.
3.
Songeza vali ya kufungia mafuta (A, Kielelezo 8), ikiwa ipo, hadi eneo la kuonyesha
IMEFUGULIWA (OPEN).
4.
Songeza kidhibiti injini (B, Kielelezo 8), ikiwa kipo, hadi eneo la kuonyesha HARAKA
(FAST). Endesha injini kidhibiti kikiwa katika eneo la kuonyesha HARAKA (FAST).
5.
Songeza kidhibiti cha choki (F, Kielelezo 8), hadi eneo la kuonyesha IMEFUNGWA
(CLOSED).
Kumbuka: Kwa kawaida choki haihitajiki wakati wa kuwasha upya injini iliyochemka.
6.
Ikiwa bidhaa ina wenzo wa kusimamisha injini (C, Kielelezo 10), shikilia wenzo wa
kusimamisha injini dhidi ya sehemu ya kushika.
7.
Anzisha Upya, iwapo ipo: Kwa uthabiti shikilia sehemu ya kushika ya kamba ya
kianzishaji (E, Kielelezo 8, 9). Vuta kamba ya kianzishaji polepole hadi uhisi inakuwa
gumu kuvuta, kisha uvute kwa haraka.
Onyo
Uvutaji nyuma kwa haraka wa kamba ya kianzishaji (kuvuta nyuma kwa haraka) kutavuta
mkono wako kuelekea kwenye injini haraka zaidi kuliko unavyoweza kuachilia. Inaweza
kupelekea mifupa kuvunjika, michubuko au kuteguka maungo. Wakati wa kuwasha
injini, vuta kamba ya kianzishaji polepole hadi uhisi inakuwa gumu kuvuta na kisha uvute
kwa haraka ili kuzuia kuvutwa nyuma kwa haraka.
8.
Kianzishaji kwa Umeme, iwapo kipo: Geuza swichi ya kianzishaji kwa umeme
hadi eneo la kuonyesha WASHA / ANZA (ON / START).
Notisi
Ili kurefusha muda wa kianzishaji, tumia misururu mifupi ya kuanzisha (upeo
wa sekunde tano). Subiri dakika moja kati ya misururu ya kuanzisha.
9.
Injini inapochemka, songeza kidhibiti cha choki (F, Kielelezo 8) hadi eneo la
kuonyesha IMEFUNGULIWA / ENDESHA (OPEN / RUN).
Kumbuka: Injini ikikosa kuwasha baada ya majaribio kadhaa, wasiliana na mtoa huduma
wako wa ndani au nenda kwenye BRIGGSandSTRATTON.com au upige simu kwa 1-
800-233-3723 (nchini Marekani).
Simamisha Injini
Onyo
Mafuta na mvuke wake unaweza kuwaka moto na kulipuka ka haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha majeraha mabaya ya kuchomeka au kifo.
Ujaribu kutoruhusu hewa kuingia kwenye kabureta ili kusimamisha injini.
1.
Wenzo wa Kusimamisha Ijini, iwapo upo: Ondosha wenzo wa kusimamisha injini
(E, Kielelezo 10).
50
Swichi ya Kusimamisha, iwapo ipo: Songeza swichi ya kusimamisha (D, Kielelezo
9) hadi kwenye eneo la kuonyesha ZIMA (OFF).
Kidhibiti Injini, iwapo kipo: Songeza kidhibiti Injini (B, Kielelezo 8) kwenye eneo
la kuonyesha SIMAMISHA (STOP).
Ufunguo wa Kianzishaji kwa Umeme, iwapo upo: Geuza ufunguo wa kianzishaji
kwa umeme hadi eneo la kuonyesha ZIMA / SIMAMISHA (OFF / STOP). Ondoa
ufunguo na uuweke katika mahali salama mbali na watoto.
2.
Baada ya injini kusimamishwa, songeza vali ya kufungia mafuta (A, Kielelezo 8),
ikiwa ipo, hadi kwenye eneo la kuonyesha IMEFUNGWA (CLOSED).
Udumishaji
Notisi
Iwapo injini imeinamishwa wakati wa udumishaji, tangi la fueli, iwapo liko
kwenye injini, lazima liwe tupu na upande wa kuziba cheche lazima uwe juu. Iwapo
tangi la fueli sio tupu na iwapo injini imeinamishwa katika mwelekeo mwingine, inaweza
kuwa vigumu kuwaka kwa sababu ya mafuta au petroli kuchafua kuchuja hewa na/au
kuziba cheche.
Onyo
Wakati unapotekeleza udumishaji unaohitaji kitengo kuinamishwa, tangi la fueli, iwapo
limewekwa kwenye injini, lazima liwe tupu au fueli inaweza kumwagika nje na
kusababisha moto au mlipuko.
Tunapendekeza kuwa umwone Mtoa Huduma yeyote wa Briggs & Stratton Aliyeidhinishwa
kwa udumishaji na huduma zote za injini na sehemu za injini.
Notisi
Vijenzi vyote vilivyotumiwa kujenga injini hii lazima visalie sawa kwa uendeshaji
bora.
Onyo
Cheche zisizotarajiwa zinaweza kusababisha moto au mshtuko wa kielektriki.
Uwashaji usiotarajiwa unaweza kusababisha kunaswa, kukatwa kwa viungo kwa
kiwewe, au majeraha makali ya ukataji wa ngozi.
Madhara ya moto
Kabla ya kutekeleza marekebisho au ukarabati:
Tenganisha waya ya kuziba cheche na uhifadhi mbali na kuziba cheche.
Tenganisha betri katika mwisho wa chanya (injini zilizo na kiwashaji wa kielektriki
tu.)
Tumia zana sahihi tu.
Usihitilifiane na springi ya kithibiti, viunganishi au sehemu zingine ili kuongeza kasi
ya injini.
Sehemu za ubadilishaji lazima ziwe sawa na zilizosakinishwa katika eneo sawa
kama sehemu asili. Sehemu zingine huenda zisitekeleze vilevile, zinaweza kuharibu
kitengo, na inaweza kusababisha majeraha.
Usigonge gurudumu la kuongeza kasi ya injini kwa nyundo au kifaa kigumu kwa
sababu gurudumu la kuongeza kasi ya injini linaweza kuvunjika wakati wa kuendesha.
Wakati wa kujaribu cheche:
Tumia kijaribio cha kuziba cheche kilichoidhinishwa.
Usikague injini wakati kuziba cheche imeondolewa.
Huduma ya Udhibiti wa Mafukizo
Udumishaji, ubadilishaji, au ukarabati wa vifaa na mifumo ya kudhibiti mafukizo
unaweza kutekelezwa na kituo chochote au mtu yeyote wa kukarabati injini. Hata
hivyo, ili kupata huduma ya kudhibiti mafukizo ya "bila malipo", ni lazima kazi ifanywe na
mtoa huduma aliyeidhinishwa na kiwanda. Tazama Taarifa ya Udhibiti wa Mafukizo.
Ratiba ya Udumishaji
Udhumishaji na Huduma
Saa 5 za Kwanza
Badilisha oili ( Hakuhitajiki kwenye miundo ya Just Check & Add™ )
Kila Baada ya Saa 8 au Kila Siku
BRIGGSandSTRATTON.com

Publicidad

Tabla de contenido
loading

Este manual también es adecuado para:

120000

Tabla de contenido