10
Ili uepuke majeraha kutokana na visu vinavyozunguka, kaa
mbali na ukingo wa deki na ukatie nyasi mbali na watu wengine.
Ujumbe wa Usalama
Onyo
Soma, uelewa, na kutii maagizo na maonyo yote katika
Mwongozo wa Mwendeshaji na kwenye mashine, injini,
na viambatisho kabla ya kuendesha mashine hii. Kukosa
kuzingatia maagizo ya usalama katika mwongozo huu na
kwenye kifaa kunaweza kusababisha kifo au majeraha
mabaya.
• Ruhusu tu waendeshaji wanaowajibika, waliopitia
mafunzo na wanaofahamu maagizo na wana uwezo wa
kimwili wa kuendesha mashine hii.
• Usiendeshe mashine ukiwa mlevi wa pombe au dawa.
• Vaa miwani za usalama na viatu vilivyofungika.
• Usiweka mikono au miguu karibu na sehemu
zinazozunguka au chini ya mashine. Kaa mbali na
mwanya unaotoa nyasi nyakati zote.
• Weka mashine katika hali nzuri ya kufanya kazi.
Badilisha sehemu zilizochakaa au kuharibika.
• Kuwa mwangalifu unapofanyia visu huduma. Funga
visu au uvalie glavu. Badilisha visu vilivyoharibika.
Usifanyie visu ukarabati au kuhitilafiana navyo.
• Tumia vifaa pana unapopakia na kupakua mashine kwa
ajili ya usafiri.
• Tazama kiambatisho au kikorokoro ili kujua uzani
mwafaka wa magurudumu.
• Ili kusaidia kuzuia moto, wek mashine bila nyasi,
majani, au vitu vingine visivyotakikana. Safisha oili au
mafuta yoyote yaliyomwagika. Ondoa vifusi vilivyoloa
mafuta na uache mashine ipoe kabla ya kuiweka.
Onyo
Injini inayofanya kazi kaboni monoksidi, gesi isio na harafu,
wala rangi na ni ya sumu. Kupumua kaboni monoksidi
kunaweza kusababisha kuumwa na kichwa, uchovu,
kizunguzungu, kutapika, kichanganyikiwa, shtuko la moyo,
kichefuchefu, kuzirai au kifo.
• Endesha kifaa nje PEKE YAKE.
• Zuia gesi za ekzosi zisiingie eneo lililofungwa kupitia
madirisha, milango, sehemu zingine za kuingiza hewa,
au mianya mingine.
Vipengele na Vidhibiti
Linganisha herufi katika Kielelezo 3 na vipengele na vidhibiti
vinavyolingana na mashine yako iliyoorodeshwa katika
jedwali ambatani.
Ishara za Udhibiti na Maana Yake
A
Chaguo la Kukata Nyasi Ukirudi Nyuma
B
Mita ya Saa (ikiwa ipo)
C
Swichi ya Kuwasha
D
Swichi ya Kuwasha Nishati ikiwa Juu, Washa Visu
E
Kuwasha Nishati
F
Swichi ya Kuwasha Nishati ikiwa Chini, Zima Visu
G
Kidhibiti Uendeshaji
H
Breki ya Kuegesha
I
Kidhibiti Injini
J
Kidhibiti Injini katika Eneo la Linaloonyesha
POLEPOLE (SLOW)
K
Kidhibiti Injini katika Eneo la Linaloonyesha
HARAKA (FAST)
ZIMA (OFF)
ENDESHA (RUN)
Washa
Swichi ya Taa za Mbele
67