Descargar Imprimir esta página

Victa SPX2342F Manual Del Operador página 74

Publicidad

Idiomas disponibles
  • MX

Idiomas disponibles

  • MEXICANO, página 19
7. Paka vichwa vya betri na kebo mafuta ya mgando au
upake grisi isiyopitisha umeme.
Chaji Betri
Onyo
Weka moto wazi na cheche mbali na betri; gesi zinazotoka
kwenye betri zina uwezekano mkubwa sana wa kulipuka.
Weka betri kwenye hewa safi wakati wa kuichaji.
Betri iliyokufa au ambayo ni dhaifu sana kuwasha injini
inaweza kusababisha dosari katika mfumo wa kuchaji au
kijenzi kingine cha umeme. Ikiwa kuna shaka yoyote kuhusu
sababu ya tatizo, mtembelee muuzaji wako. Ikiwa unahitaji
kubadilisha betri, fuata hatua za Kusafisha Betri na Kebo.
Ili kuchaji betri, fuata maagizo yaliyotolewa na mtengenezaji
kifaa cha kuchaji betri na vilevile onyo zote zilizojumuishwa
katika sehemu ya kanuni za usalama za kitabu hiki. Chaji
betri hadi ijae kabisa. Usichaji katika kiwango kikubwa zaidi
kuliko 10 amps.
Muda wa Kusimama wa Visu vya Kukatia
Nyasi
Onyo
Visu vya mashine ya kukatia nyasi vikikosa kusimama
kabisa ndani ya sekunde 5, ni lazima klachi isogezwe.
Usiendeshe mashine mpaka urekebishaji mwafaka uwe
umefanywa na Muuzaji Huduma Aliyeidhinishwa wa Briggs
& Stratton. 
Visu vya kukatia nyasi na mkanda wa kuendeshea mashine
ya kukatia ni lazima zisimame ndani ya sekunde tano baada
ya swichi ya Kuwasha Nishati (PTO) KUZIMWA. Ikiwa
mkanda wa mashine ya kukatia nyasi hautasimama ndani ya
sekunde tano, mtembelee Muuzaji Huduma Aliyeidhinishwa
wa Briggs & Stratton ili kufanya ukarabati. 
Badilisha Oili ya Injini
1. Washa injini hadi ipate joto.
2. Weka kifaa katika eneo tambarare (rejelea Kielelezo 11).
3. Zima injini na kisha uondoe ufunguo wa kuwasha ingiza
(A, Kielelezo 11) au ufunguo.
4. Safisha vifusi vyovyote kutoka sehemu za kujaza na
kuchuka oili.
5. Ondoa kijiti cha kupimia oili. (B) na kisha ukiweke kwenye
kitambaa safi.
6. Tenganisha bomba la umwagaji oili (A, Kielelezo 12).
7. Ondoa kifuniko kwa makini (B) na uteremshe bomba
kwenye kontena iliyoidhinishwa (C).
8. Baada ya oili kumwagwa, funika na uikaze, kisha
uunganishe bomba kwenye upande wa injini.
9. Ondoa kichujio cha oili (B, Kielelezo 13) na utupe kwa
njia bora
74
10. Lainisha kidogo kichujio oili cha gasketi (A) kwa kutumia
oili nzuri, safi..
11. Weka kichujio cha oili ukitumia mkono hadi gasketi
igusane na adapta ya kichujio cha oili, (C), kisha ukaze
kichujio cha oili kwa mizunguko ya 1/2 hadi 3/4.
12. Ongezea oili (rejelea katika Kagua na Uongeze Oili ya
Injini sehemu).
Mkusanyiko wa Kichujio cha Hewa
(Katriji pamoja na kisafishaji cha
kwanza)
Onyo
Usiwahi kuwasha au kuendesha injini huku kisafishaji hewa
au chujio la hewa zikiwa zimeondolewa kwani ni hatari ya
kusababisha moto.
Notisi
Usitumie hewa au maji yaliyoshinikizwa kusafishia chujio.
Hewa iliyoshinikizwa inaweza kuharibu chujio na maji
yatayeyusha chujio.
1. Legeza sehemu za kufunga (A, Kielelezo 14) na uondoe
kifuniko (B).
2. Ondoa mkusanyiko wa kisafishaji cha hewa (C) na
uondoe mkusanyiko husika.
3. Ondoa vifuzi vyovyote ambavyo vinaweza kuingia ndani
ya kabureta (D).
4. Ondoa kisafishaji cha kwanza kutoka kwenye kichujio cha
hewa.
5. Ili kulegeza vifusi, gongesha taratibu kichujio cha hewa
kwa utaratibu kwenye eneo gumu. Ikiwa kichujio cha
hewa ni kichafu kupita kiasi, badilisha kwa kichujio kipya.
6. Osha kisafishaji cha kwanza katika sabuni ya maji na
maji. Kisha kiwache kikauke kabisa kwenye hewa kavu.
Usipake oili kwenye kisafishaji cha kwanza.
7. Funga kisafisha cha kwanza kwenye kichujio cha hewa.
8. Weka mkusanyiko wa kichujio cha hewa.
9. Weka kifuniko na ukaze sehemu za kukazia.
Kagua Plagi za Spaki
Onyo
Cheche zisizokusudiwa zinaweza kusababisha moto au
mrusho wa umeme. 
Uwashaji usiokusudiwa unaweza kusababisha kunaswa,
kukatwa kwa viungo kwa kiwewe, au majeraha makali ya
ukataji wa ngozi. 
 Wakati wa kujaribu cheche: 
• Tumia kifaa kilichoidhinishwa cha kujaribu plagi ya
spaki. 
• Usikague cheche huku plagi ya spaki ikiwa
imeondolewa. 

Publicidad

loading

Este manual también es adecuado para:

2691498