ONYO HATARI YA GESI YA SUMU. Eksozi ya
injini ina monoksidi ya kaboni, gesi ya sumu
ambayo inaweza kukuua wewe kwa dakika
chache. HUWEZI kuiona, kuinusa wala kuionja.
Hata kama huwezi kunusa mafukizo ya eksozi,
bado unaweza kuvuta gesi ya monoksidi ya kaboni.
Ukianza kuhisi mgonjwa, kisunzi, au mnyonge wakati
unatumia bidhaa hii, nenda mahali penye hewa safi
MARA MOJA. Mwone daktari. Huenda ukawa
umeathiriwa na sumu ya monoksidi ya kaboni.
• Endesha kifaa hiki nje PEKEE mbali na madirisha,
milango na matundu ili kupunguza hatari ya gesi ya
monoksidi ya kaboni kukusanyika na kuenda maeneo
yenye watu.
• Weka ving'ora vya betri vya monoksidi ya kaboni
au weka ving'ora vya betri vya monoksidi ya kaboni
kulingana na maelekezo ya mtengenezaji. Ving'ora vya
moshi haviwezi kutambua gesi ya monoksidi ya kaboni.
• USIENDESHE mtambo huu ndani ya nyumba, gereji,
vyumba ya chini ya ardhi, ubati, vibanda, au majengo
mengine yaliyobanwa hata kama unatumia viyoyozi
ama kufungua milango na madirisha kwa hewa.
Monoksidi ya kaboni inaweza kukusanyika haraka
katika maeneo haya na ibakie kwa saa kadhaa, hata
baada ya kifaa hiki kuzimwa.
• Weka kifaa hiki upande upepo unatoka WAKATI
WOTE na ulenge ekzosi mbali na maeneo yenye watu.
ONYO Matumizi ya pampu ya maji yanaweza
kusababisha vidimbwi na sakafu telezi ambazo
huenda zikasababisha kuanguka kunakoweza
kuleta kifo au majeraha mabaya.
• Endesha pampu ya maji juu ya sakafu iliyo dhabiti.
• Eneo linapaswa kuwa na miteremko ya kutosha na
mifereji ya maji taka ili kupunguza uwezekano wa
kuanguka kutokana na sakafu telezi.
ONYO Kurudi kwa kamba ya kiasha mtambo
(kunywea haraka) kwaweza kuvuta mkono
kuuelekekeza kwenye mashine kwa kasi
kuliko unavyoweza kuachilia ambako
kunaweza sababisha kuvunjika kwa mkono,
kuvunjika mifupa, kupata miparuzo ama kuteguka na
kusababisha majeraha mabaya.
• Wakati unapowasha injini, vuta kamba polepole mpaka
pale ambapo utaweza kuhisi upinzani na kisha uvute kwa
haraka ili kuepuka kukataa kuwashwa kwa mtambo.
• Weka mikono na mwili mbali na pampu ya kumwaga.
• Hifadhi bomba la kumwaga kuzuia kugongwa.
ONYO Stata na sehemu zingine zinazozunguka
zaweza kunasa mkono, nywele, nguo ama
vivalio vingine na kusababisha majeraha
mabaya.
• USIDHUBUTU kuweka mikono au sehemu zingine
za mili katika pampu inayonguruma ama katika
mabomba.
• USIWAHI kuendesha kioshaji kwa presha bila ya
sehemu za kukifunika au vifuniko.
• USIVALIE mavazi yaliyolegea, mapambo au kitu
chochote kilicholegea kinachoweza kukamatwa
kwenye kiwashi au sehemu nyingine zinazozunguka.
• Funga nywele ndefu na uondoe mapambo.
NOTISI Pampu hii imeundwa kupiga maji ambayo si ya
matumizi na binadamu.
NOTISI Matumizi mabaya ya mtambo huu yanaweza
kuuharibu na kufupisha maisha yake.
• Kama unayo maswali kuhusu matumizi yaliyonuiwa,
mwulize mwuzaji au wasiliana na kituo cha huduma
kinachofaa.
• Hakikisha kuwa chumba cha pampu kimejazwa maji
kabla ya kungurumisha mtambo. Usiendeshe pampu
bila ya kujaza maji ya msukumo.
• Tumia bomba lisilojikunja upande wa kufyonza wa
pampu.
• Tumia mtambo huu kwa matumizi yaliyokusudiwa
pekee.
• Kuvuta maji ya bahari, vileo au vinywaji, asidi,
michakato ya kemikali, ama kioevu kingine
kinachodumisha kutu vyaweza kuharibu mtambo.
• Hakikisha viunganishi vyote havivuji hewa.
• USIKINGE bomba la kufyonza wala la kumwaga kwa
njia yoyote.
• USIENDESHE mtambo bila kapu la kuchujia katika
upande wa kufyonza.
• USIZIDISHE kiwango cha kilele cha kufyonza na jumla
ya kilele (angaliaVipimo Maalum). Tumia kilele cha
kufyonza kilicho kifupi iwezekanavyo.
• USIRUHUSU magari kukanyaga mabomba. Iwapo
utatumia bomba kuvuka barabara, tumia vipande vya
mbao katika kila upande wa bomba kuruhusu magari
kupita bila kukinga wala kubonyeza bomba.
• Hifadhi pampu kuhakikisha "halitembei" wala
kuyumba, hasa kama liko karibu ya mtaro ama pembe
ya bonde. Mtambo huenda ukatumbukia.
• Weka mtambo mbali na ukingo wa mto ama bahari
kuhakikisha ukingo hauporomoki.
• USIINGIZE vitu vyovyote katika mianya ya kupumua.
• USIWAHI kutumia mashine haya yakiwa na sehemu
zilizovunjika au zinazokosekana, au bila ya sehemu
yake inayoyafunika au vifuniko.
• USIPUUZE kifaa chochote cha usalama katika
mashine hii.
• USISONGESHE mtambo kwa kuvuta mabomba -
tumia shikio.
• USIWARURHUSU watu wasiohitimu ama watoto
kuendesha mtambo wala kuukarabati.
• Angalia kuvuja katika mfumo wa mafuta au alama za
kuzorota, kama vile bomba lililochibuka au kuchafuka,
mabano yaliyolegea au kutoka, tangi au kifuniko
vilivyoharibika. Rekebisha makosa yote kabla ya
kuendesha pampu ya maji.
• Kifaa hiki kimeundwa kutumiwa na vipuri
vilizoidhinishwa vya Briggs & Stratton pekee. Ikiwa
mtambo huu utatumia vipuri ambavyo HAVIAMBATANI
na vipimo maalum, mtumizi atachukua majukumu yote
ya hatari na gharama.
5