Mfumo wa Upasuaji wa LL-CO
KUUNGANISHA VIUNGO VYA CHOMBO NA JINSI YA KUTUMIA CHOMBO
TAHADHARI: Lazima silinda ya gesi ifungwe ili kuizuia kuanguka. Wallach hutoa rukwama kwa lengo
hili. Kwa maelezo zaidi tafadhali muulize mwakilishi wako wa huduma kwa wateja.
1. Ondoa vazi la kinga ambalo hufunika neli ya friza ya chombo. Weka vizuri vazi hilo la kinga kama
utahitaji kusafirisha chombo wakati wowote katika siku zijazo kwa sababu neli ya ndani yaweza
kuvunjika upesi.
2. Chagua ncha jitwalia ya kifaa cha upasuaji safi kabisa iliyo na ngao dhahiri ya plastiki na uiweke
kwa kutumia utaratibu usio na bacteria. Funga vizuri kwa mkono pekee – usitumie nyenzo kukaza.
ONYO: Unapobadilisha ncha, lazima uwe umezima vali ya WASHA/ZIMA (ON/OFF).
Kuhakikisha kuwa gesi haipiti kupitia kwa kipima kidonda, subiri angalau muda wa dakika 5 kabla
ya kuondoa ncha baada ya kutumia. Kuondoa ncha kabla ya dakika 5 kwaweza kusababisha
uharibifu usiotarajiwa wa ncha na pia kudhuru nyama za mkono wa daktari ambazo hazijazuiliwa.
3. Kaza kiunganishi cha nira ya silinda kwa silinda iliyo na gesi ya dioksidi kaboni ya gredi ya
matibabu.
4. Ukiwa umefungua wazi vali ya silinda, na kipima kidonda unachotaka kikiwa mahali pake,
"WASHA" vali ya WASHA/ZIMA (ON/OFF).
FAHAMU: Kwa kutahini operesheni sahihi elekeza ncha upande wa sakafu wakati unafinya
chombo cha utaratibu.
5. Tia kichwa cha kipima kidonda kwenye tishu zinazohitaji kutibiwa.
6. Finya kwa nguvu chombo cha kutia baridi utaratibu kugandisha au shinikiza chombo hiki mbele ili
kukifungilia mahali pake wakati wa kugandisha (wakati wa kawaida wa kugandisha ni dakika
1 hadi 3).
7. Baada ya wakati wa kugandisha, achilia chombo cha utaratibu ili kuyeyusha barafu.
8. ZIMA vali ya ON/OFF (WASHA/ZIMA) na ujitayarishe kwa utaratibu unaofuata.
9. Ukimaliza tiba, "ZIMA" vali ya WASHA/ZIMA (ON/OFF) na uzime kabisa vali ya silinda ya
gesi.
FAHAMU: Ikiwa utahitaji zaidi ya ncha moja kukamilisha matibabu, ni muhimu "KUZIMA" vali
ya WASHA/ZIMA (ON/OFF) na kuzima vali ya silinda ya gesi wakati wa kubadilisha ncha.
Baada ya dakika tano, toa parafujo kwa ncha inayotumika kwa sasa, na kwa kutumia utaratibu usio
na bacteria badilisha ili kuweka ncha unayotaka.
KUZIMA
1. Ukiwa UMEZIMA vali ya WASHA/ZIMA (ON/OFF), unaweza kuondoa kiunganishi nira ya
silinda, au unaweza kubadilisha ncha.
2. Mwisho wa utaratibu – au ifikapo mwisho wa siku — funga silinda ya ugavi kwa kuzungusha vali
ya silinda kama ilivyoonyeshwa kwenye vali.
MAELEZO ZAIDI YA UTUMIAJI WA CHOMBO
Inapendekezwa kuwa silinda za dioksidi kaboni (CO
gesi uweze kutoka kwa shinikizo inayostahili. Mara kwa mara, silinda zilizohifadhiwa nje hasa
wakati wa baridi hukoma kutoa gesi kwa shinikizo inayohitajika. Ni lazima silinda hizi zipashwe
joto ili zifikie joto la kawaida ndiposa zifanye kazi ya kuridhisha.
Usijaribu kutoa nira ya kuunganisha silinda kabla ya kuzima kwanza usambazaji wa gesi.
Usitoe parafujo ya kipima kidonda au kutoa waya ya kipima kidonda ya kitenganishi – haraka bila
KUZIMA vali ya WASHA/ZIMA (ON/OFF) na kuachilia chombo cha utaratibu kwenye mpini
wa kipima kidonda.
Katika tukio la uhaba wa kuganda au kuyeyuka barafu kabla ya wakati wake, peleleza mambo
yafuatayo:
37295 • Rev. B • 2/12
™ • Jinsi ya Kutumia Kifaa (Kiswahili / Swahili)
2
) ziwe kwenye joto la kawaida ili ugavi wa
2
49
Wallach Surgical Devices