1. Tenganisha bomba la umwagaji oili (H, Kielelezo 22) kutoka
kwenye upande wa injini.
2. Geuza na uondoe kifuniko cha tundu la umwagaji oili (I,
Kielelezo 22). Kwa uangalifu mwaga oili ukitumia eneo la
kutolea (H) katika kontena iliyoidhinishwa (J).
3. Baada ya oili kumwagwa, funga kifuniko cha tundu la
umwagaji oili. Unganisha bomba la umwagaji oili kwenye
upande wa ijini.
Kubadilisha Chujio la Oili
Kwa mpishano wa ubadilishaji, tazama Ratiba ya Udumishaji.
1. Mwaga oili kutoka kwenye injini. Tazama Kumwaga Oili .
2. Ondoa chujio a hewa (K, Kielelezo 23) na utupe kwa njia
inayofaa.
3. Kabla ya kuweka chujio mpya la oili, lainisha kidogo kwenye
gasketi ya chujio la oili ukitumia oili safi.
4. Weka chujio la oili ukitumia mkono hadi gasketi igusane na
adapta ya chujio la oili, kisha ukaze chuji la oili kwa
mizunguko ya 1/2 hadi 3/4.
5. Ongeza oili. Tazama Uendeshaji - Kagua Kiwango cha
Oili .
6. Washa na uendeshe injini. Injini inapochemka, kagua kwa
uvujaji wa oili.
7. Zima injini na ukague kiwango cha oili.
Kufanya Udumishaji kwenye Chujio la
Hewa
Onyo
Hatari ya Moto na Mlipuko
Mafuta na mvuke wake unaweza kuwaka moto na kulipuka
kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha majeraha mabaya ya
kuchomeka au kifo.
• Usiwahi kuwasha au kuendesha injini huku kisafishaji
hewa au chujio la hewa zikiwa zimeondolewa.
Notisi
Usitumie hewa au maji yaliyoshinikizwa kusafishia chujio.
Hewa iliyoshinikizwa inaweza kuharibu chujio na maji
yatayeyusha chujio.
1. Legeza sehemu za kufunga (A, Kielelezo 24) na uondoe
kifuniko (B).
2. Ili kuondoa chujio (C, Kielelezo 24), inua mwisho wa chujio.
3. Ondoa kisafishaji cha kwanza (D, Kielelezo 24), ikiwa kipo,
kutoka kwenye chujio.
4. Ili kulegeza vifusi, gongesha chujio kwa utaratibu kwenye
eneo gumu. Ikiwa chujio ni chafu kupita kiasi, badilisha kwa
chujio mpya.
100
5. Osha kisafishaji cha awali kwa kutumia sabuni ya maji na
maji. Kisha kiwache kikauke kabisa kwenye hewa kavu.
Osipake oili kwenye kisafisha cha awali.
6. Funga kisafisha cha awali kwenye chujio.
7. Weka chujio ndani ya injini (E, Kielelezo 24) na usukume
chini hadi chujio liingie kwenye mahali pake.
8. Funika.
Kusafisha
1. Safisha uchafu na vifusi kwenye kifaa na deki ya mashine
ya kukatia nyasi.
Kumbuka: Deki nyingine za mashine ya kukatia nyasi zina eneo
la kusafishia. Tazama Kuosha Deki ya Mashine ya Kukatia
Nyasi .
2. Safisha vifusi vyovyote vilivyo katika chumba cha injini na
juu au kando ya injini.
Onyo
Hatari ya Moto
Vifusi vya uwanjani vinaweza kuwaka moto.
• Safisha uchafu na vifusi kwenye kifaa na deki ya mashine
ya kukatia nyasi.
• Safisha vifusi vilivyokusanyika kando ya injini.
Kuosha Deki ya Mashine ya Kukatia Nyasi
Eneo la kusafishia linakuwezesha kuunganisha mfereji wa
kawaida wa bustani kwenye upande wa kushoto wa deki ya
mashine ya kukatia nyasi ili kuondoa nyasi na vifusi kutoka
sehemu ya mvunguni.
Onyo
Hatari ya Kukatwa Viungo vya Mwili na Vitu
Vinavyorushwa
Kugusana na visu vya mashine ya kukatia nyasi, au vitu
vingine vinavyorushwa na visu vya mashine ya kukatia nyasi,
kunaweza kusababisha kifo au majeraha mabaya.
• Kabla ya kuendesha mashine ya kukatia nyasi, hakikisha
mfereji umeunganishwa ipasavyo na hauguzani na visu.
• Wakati mashine ya kukatia nyasi inaendeshwa na na visu
vimewashwa, ni lazima mtu anayesafisha deki ya mashine
ya kukatia nyasi awe kwenye kiti cha mwendeshaji, na
kusiwe na waliosimama kando.
1. Weka kifaa kwenye enoe tambarare.
2. Unganisha sehemu ya kutenganisha haraka (A, Kielelezo
25) kwenye mfereji wa bustani (B) na uunganishe kwenye
eneo la kusafishia (C) kwenye deki ya mashine ya kukatia
nyasi.
3. Pitisha maji ili kuondoa nyasi na vifusi kutoka mvunguni
mwa deki ya mashine ya kukatia nyasi.