ardhini zimefungwa katika eneo linaloonyesha
ANZA/EGESHA (START/PARK).
Kumbuka: Breki ya kuegeshea huwekwa kiotomatiki wakati
wenzo za kasi ya kwenye ardhi zimefungwa katika eneo la
kuonyesha ANZA/EGESHA (START/PARK.)
2. Weka kidhibiti cha kasi ya injini kupita eneo la kuonyesha
HARAKA (FAST) hadi kwenye eneo la kuonyesha CHOKI
(CHOKE).
Kumbuka: Injini iliyoshika joto haihitaji choki.
Kumbuka: Baadhi ya injini zina udhibiti tofauti wa choki.
Kumbuka: Baadhi ya injini zina kipengele cha ReadyStart®, na
hazina choki.
3. Ingiza ufunguo kwenye swichi ya kuwashia na uzungushe
hadi ANZA (START).
4. Baada ya injini kuwaka, zima choki (ikiwa ipo), na upashe
injini joto kwa kuingurumisha kwa angalau dakika moja
kabla ya kuwasha swichi ya PTO au kuendesha kifaa.
5. Baada ya kupasha injini joto, kila wakati endesha kifaa kwa
kasi ya juu zaidi ya injini wakati unakata nyasi.
Katika hali ya dharura injini inaweza kusimamishwa kwa
urahisi kwa kuzungusha switchi ya kuwashia kwenye
SIMAMA. Tumia njia hii tu katika hali za dharura. Ili kuzima injini
kwa njia ya kawaida fuata utaratibu uliotolewa katika
Kusimamisha Kifaa Na Injini .
Kusimamisha Kifaa
1. Rejesha wenzo za kasi ya ardhini hadi eneo la katikati (au
bila gia 'N' ) ili kusimamisha mwendendo wa kifaa. Zungusha
wenzo upande wa nje ili kuzifunga katika eneo
linaloonyesha ANZA/EGESHA (START/PARK).
Kumbuka: Kusongeza wenzo za kasi ya kwenye ardhi kwenye
nafasi ya ANZA/EGESHA huweka breki ya kuegeshea
kiotomatiki.
2. Zima PTO kwa kusukuma chini kwenye swichi ya PTO.
3. Songeza kidhibiti cha kasi ya injini hadi kwenye eneo
linaloonyesha POLEPOLE (SLOW) na uzungushe ufunguo
wa kuwashia hadi eneo linaloonyesha ZIMA (OFF). Ondoa
ufunguo.
Kukata Nyasi
1. Hakikisha swichi ya PTO imezimwa, wenzo za udhibiti wa
kasi ya ardhini zimefungwa katika eneo la kuonyesha
ANZA/EGESHA (START/PARK), na mwendeshaji amekalia
kiti.
2. Washa injini. Tazama Kuwasha Injini .
3. Weka urefu wa kukatia nyasi. Tazama Ubadilishaji wa
Urefu wa Kukatia .
4. Weka kidhibiti cha kasi ya injini kuwa HARAKA (FAST).
5. Washa PTO kwa kuvuta juu swichi ya PTO.
6. Zungusha wenzo za kasi ya ardhini upande wa ndani kutoka
eneo linaloonyesha ANZA/ EGESHA (START/ PARK) hadi
eneo linaloonyesha hakuna gia, 'N'.
7. Anza kukata nyasi. Tazama Usalama wa Mwendeshaji ili
kupata madokezo kuhusu mazoea salama ya kukata nyasi.
8. Ukimaliza, zima PTO.
9. Zima injini. Tazama Kusimamisha Kifaa Na Injini .
Kusukuma Kifaa kwa Mikono
Onyo
Hatari ya Uendeshaji Usio Salama.
USIONDOE gia na kuteremka miteremko bila gia. USITUMIE
mbinu ya Kulegeza Vyuma ili kutoa gia isipokuwa iwe kwamba
mwendo wa mashine unaweza kudhibitiwa na injini imezimwa.
Notisi
Usivute kifaa. Kuvuta kifaa kutasababisha uharibifu kwenye
klachi na gea. Usitumie gari jingine kusukuma au kuvuta kifaa.
1. Zima PTO, funga wenzo wa kasi ardhini kwenye eneo
linaloonyesha ANZA/PAKIA (START/PARK), ZIMA injini,
ondoa ufunguo, na usubiri sehemu zote zinazozunguka
zisimame.
2. Ili kuondoa gia, songeza wenzo za kulegeza vyuma (A au
B, Kielelezo 5, kulingana na muundo), katika eneo la
kuonyesha SUKUMA (PUSH) kama ilivyoonyeshwa.
3. Zungusha ndani wenzo za kasi ya kwenye ardhi kutoka
katika sehemu ya ANZA/EGESHA hadi gia huru ya 'N' kuteo
breki ya kuegeshea. Sasa kifaa kinaweza kusukumwa kwa
mkono.
4. Baada ya kusogeza kifaa, weka upya gia kwa kusongeza
wenzo za kulengeza vyuma kwenye eneo linaloonyesha
ENDESHA (DRIVE).
Uendeshaji
Mazoezi ya Uendeshaji wa Kugeukia Mahali
Pamoja
Kabla ya kijaribu kuendesha mashine ya kukatia nyasi ya
kugeukia mahali pamoja hakikisha kwamba umesoma sehemu
ya Vipengele na Vidhibiti na umeelewa eneo na utendaji wa
vidhibiti vyote vya kifaa.
Wenzo za kudhibiti kasi ya ardhini za mashine ya kukatia nyasi
iya kugeukia mahali pamoja zinafanya kazi vizuri, na kujifunza
kupata udhibiti rahisi na fanisi wa kifaa kuenda mbele, kurudi
nyuma, na kugeuza kutalazimu kufanya mazoezi.
Kuchukua muda kuoitia mienendo iliyoonyeshwa na
kujifahamisha na jinsi kifaa kinavyoongeza kasi, kinavyosafiri,
na kinavyoendesheka, kabla ya kuanza kukata nyasi, ni
95