Descargar Imprimir esta página

Briggs & Stratton Victa 46 23HP Manual Del Operador página 90

Publicidad

Idiomas disponibles
  • MX

Idiomas disponibles

  • MEXICANO, página 22
4. Kwenye miteremko, uzito wa kifaa kinachokokotwa unaweza
kusababisha kifaa kupoteza udhibiti.
5. Nenda polepole na uwache nafasi ya ziada kwa ajili ya
kusimama.
6. Usihamishie kwenye gia huru na kuteremka kwenye
mteremko.
Watoto
Ajali za kuhuzunisha zinaweza kutokea ikiwa mwendeshaji
hayuko makini kwa kuwepo kwa watoto. Mara nyingi watoto
huvutiwa na kifaa hicho na shughuli ya kukata nyasi. Usiwahi
dhania kwamba watoto watasalia kukaa pale ulipowaona mara
ya mwisho.
1. Weka watoto mbali na eneo linalokatwa nyasi na chini ya
uangalizi mkubwa wa mtu mzima anayewajibika.
2. Kuwa makini na uzime kifaa watoto wakiingia katika eneo
hilo.
3. Kabla na wakati wa kuendesha ukirudi nyuma, tazama
nyuma na chini kama kuna watoto wadogo.
4. Usiwahi kubeba watoto, hata kama visu vimezimwa.
Wanaweza kuanguka na kujeruhiwa vibaya sana au
kuhitilafiana na uendeshaji salama wa kifaa. Watoto ambao
wamewahi kubebwa na kifaa hapo awali huenda wakatokea
ghafla katika eneo linalokatwa nyasi wakitaka kubebwa
tena na wagongwe au kusukumwa na mashine hiyo.
5. Usiwahi kuruhusu watoto kuendesha kifaa hicho.
6. Kuwa mwangalifu zaidi unapokaribia kona usizoweza kuona
mbali, vichaka, miti, au vitu vingine ambavyo vinaweza
kuzuia kuona.
Mafukizo
1. Moshi wa injini unaotolewa na bidhaa hii una kemikali
zinazojulikana, katika viwango fulani, kusababisha saratani,
ulemavu wa kuzaliwa, au madhara mengine ya uzazi.
2. Tazama Kipindi ambacho Mafukizo Yanadumu na Maelezo
ya Hali ya Hewa kwenye lebo ya mafukizo ya injini.
Mfumo wa Kuwasha
1. Mfumo huu wa kuwasha kutumia spaki unaambatana na
Kiwango cha Kanada cha ICES-002.
Huduma Na Udumishaji
Utumizi Salama wa Petroli
1. Zima sigara, viko, na vyanzo vingine vyote vya mwako.
2. Tumia tu kontena za petroli zilizoidhinishwa.
3. Usiwahi kuondoa kifuniko cha petroli au kuongeza mafuta
wakati injini imewashwa. Wacha injini ipoe kabla ya
kuongeza mafuta.
4. Usiwahi kuongeza mafuta kwenye mashine ikiwa mahali
ndani.
90
5. Usiwahi kuweka kifaa au kontena ya mafuta mahali ambapo
kuna moto ulio wazi, cheche, au taa ya kibatali kama vile
karibu na hita ya kuchemshia maji au vifaa vingine.
6. Usiwahi kujaza makontena ndani ya gari au katika eneo la
mizigo ukitumia kifaa cha plastiki cha kulazwa kwenye gari.
Daima weka makontena chini ardhini mbali na gari lako
kabla ya kuongeza mafuta.
7. Ondoa vifaa vinavyoendeshwa kwa petroli kutoka kwenye
gari au trela na uviongeze mafuta vikiwa chini ardhini. Ikiwa
hili haliwezekani, basi ongeza mafuta kwenye kifaa hicho
kwenye trela kwa kutumia kontena inayobebeka, badala ya
ncha ya kimiminio cha petroli.
8. Weka ncha igusane na ukingo wa tangi la mafuta au kinywa
cha kontena muda wote mpaka kujaza mafuta kukamilike.
Usitumie kifaa cha kufunga na kufungua ncha.
9. Mafuta yakimwagikia nguo, badilisha nguo hizo mara moja.
10. Usiwahi kujaza tangi la mafuta kupita kiasi. Rejesha kifuniko
cha mafuta na ukikaze kwa usalama.
11. Kuwa mwangalifu zaidi unapotumia petroli na mafuta
mingine. Yanaweza kushika moto na mivuke inaweza
kulipuka.
12. Mafuta yakimwagika, usijaribu kuwasha injini lakini zongeza
mashine mbali na eneo ambapo mafuta yamemwagika na
uepuke kuunda chanzo chochote cha mwako mpaka mivuke
ya mafuta iishe kabisa.
13. Rejesha vifuniko vyote vya tangi la mafuta na vifuniko vyote
vya kontena ya mafuta kwa usalama.
Huduma na Udumishaji
1. Usiwahi kuendesha kifaa katika eneo lisilo wazi ambapo
mafukizo ya kaboni monoksidi yanaweza kukusanyika.
2. Weka nati na bolti, haswa bolti za kiambatisho cha kisu,
zikiwa zimekazwa na uweke vifaa katika hali nzuri.
3. Usiwahi kuhitilafiana na vifaa vya usalama. Kagua
utendakazi wake mara kwa mara na ufanye ukarabati
unaohitajika ikiwa havifanyi kazi vizuri.
4. Weka kifaa bila nyasi, majani, au vifusi vingine
vilivyosongamana. Safisha oili na mafuta yaliyomwagika,
na uondoe vifusi vyovyote vilivyoloa mafuta. Wacha mashine
ipoe kabla ya kuihifadhi.
5. Ukigonga kitu, simama na ukague mashine. Karabati, ikiwa
yahitajika, kabla ya kuiwasha tena.
6. Usiwahi kufanya mabadiliko au ukarabati huku mashine
ikiwa imewashwa.
7. Kagua vijenzi vya kifaa cha kukamata nyasi na cha kutoa
nyasi mara nyingi na ubadilishe ukitumia sehemu
inayopendekezwa na mtengenezaji, inapohitajika.
8. Visu vya kukatia nyasi vina makali. Funga kisu au uvalie
glavu, na ukue mwangalifu zaidi unapovifanyia huduma.
9. Kagua utendakazi wa breki mara nyingi. Badilisha na
ufanyie huduma inavyohitajika.
10. Dumisha au badilisha lebo za usalama na maagizo,
inavyohitajika.

Publicidad

loading