Onyo la Kishika Cheche la California
Onyo
Ni ukiukaji wa Kanuni za Rasilimali za Umma za California,
Sehemu ya 4442, kutumia au kuendesha injini katika eneo
linalozungukwa na msitu, lililozungukwa na brashi, au lililo na
nyasi isipokuwa mfumo wa ekzosi una kishika spaki, kama
ilivyobainishwa katika Sehemu ya 4442, kilichodumishwa
katika hali fanisi ya kufanya kazi. Mamlaka mengine ya
Majimbo au shirikisho yanaweza kuwa na sheria sawia.
Wasiliana na mtengenezaji asilia wa kifaa, muuzaji rejareja,
au muuzaji ili kupata kishika spaki kilichobuniwa kwa ajili ya
mfumo wa ekzosi uliowekwa kwenye injini hii.
Onyo la Kaboni Monoksidi
Onyo
HATARI YA GESI YENYE SUMU. Eksozi ya injini ina
monoksidi ya kaboni, gesi ya sumu ambayo inaweza
kukuua wewe kwa dakika chache. HUWEZI kuiona,
kuinusa wala kuionja. Hata kama huwezi kunusa mafukizo
yanayotolewa, bado unaweza kuvuta gesi ya monoksidi
ya kaboni. Iwapo utaanza kuhisi mgonjwa, kisunzi , au
mchovu wakati unatumia bidhaa hii, izime na uende eneo
lenye hewa safi MARA MOJA Mwone Daktari. Huenda
ukawa umeathiriwa na sumu ya kaboni monoksidi.
• Tumia bidhaa hii NJE PEKEE mbali na madirisha, milango
na matundu ili kupunguza hatari ya gesi ya kaboni
monoksidi kukusanyika na uwezekano wa kuwa
inasambazwa kuelekea maeneo ya nje.
• Sakinisha ving'ora vya kutambua uwepo wa monoksidi
ya kaboni vinavyotumia betri pamoja na hifadhi ya betri
kulingana na maagizo ya mtengenezaji. Ving'ora vya
moshi haviwezi kutambua gesi ya monoksidi ya kaboni.
• USIENDESHEE bidhaa hii ndani ya nyumba, gereji,
vyumba vya chini ya ardhi, ubati, vibanda, au majengo
mengine yaliyobanwa hata kama unatumia viyoyozi ama
kufungua milango na madirisha ili hewa safi iingie. Gesi
ya kaboni monoksidi inaweza kukusanyika kwa haraka
katika maeneo haya na inaweza kukwama kwa saa nyingi,
hata baada ya bidhaa hii kuzimwa.
• KILA WAKATI weka bidhaa hii upande ambao upepo
unatelekea na uelekeze ekzosi ya injini mbali na maeneo
yenye watu.
Usalama wa Uendeshaji
Mwendeshaji yuko salama wakati kifaa kinachotumia nishati
kipo salama. Kikitumiwa vibaya, au kikikosa kudumishwa
ipasavyo, kinaweza kuwa hatari! Kumbuka, unawajibikia
usalama wako na wa waliosimama kando yako.
Tumia hisia za kawaida, na ufikirie unachofanya. Ikiwa hauna
uhakika kwamba shughuli unayotaka kufanya inaweza kufanywa
kwa njia salama ukitumia kifaa ambacho umechagua, wasiliana
na mtaalamu: wasiliana na muuzaji aliyeidhinishwa aliye karibu
nawe.
85