Descargar Imprimir esta página

Briggs & Stratton Victa 46 23HP Manual Del Operador página 97

Publicidad

Idiomas disponibles
  • MX

Idiomas disponibles

  • MEXICANO, página 22
Ili kubadilisha urefu wa kukata:
1. Sukuma kabisa pedali ya kubadilisha urefu wa kukata (A,
Kielelezo 13) mpaka sehemu ya kuruhusu uendeshaji (B)
ifunge deki katika eneo la juu zaidi (eneo la kusafiri).
2. Ondoa pini (C, Kielelezo 13) kwenye mabano ya ubadilishaji,
na uiweke katika shimo unalotaka.
Kumbuka: Hakikisha pini hiyo imeingizwa kwenye mashimo
yaliyo kwenye visahani vyote viwili vya juu na vya chini vya
mabano ya ubadilishaji.
3. Sukuma pedali ya kubadilisha urefu wa kukata, songeza
sehemu ya kuruhusu uendeshaji hadi upande wa nje, na
uwachilie pedali polepole hadi ilalie pini.
Uondoaji na Ufungaji wa Mashine ya
Kukatia Nyasi
Rejelea Mwongozo wa Deki ya Mashine ya Kukatia Nyasi ili
kupata maagizo kuhusu uondoaji na uwekaji deki ya mashine
ya kukatia nyasi.
Usawazishaji Deki ya Mashine ya Kukatia
Nyasi
Rejelea Mwongozo wa Deki ya Mashine ya Kukatia Nyasi ili
kupata maagizo kuhusu usawazishaji deki ya mashine ya kukatia
nyasi.
Eneo la Mzigo (miundo fulani)
Eneo la mzigo limeundwa kubeba hadi pauni 50 (kilo 22.7).
Sehemu zilizo upande wa nyuma eneo la mzigo zinaweza
kubebea vitu vya 2 x 4 au 2 x 6 ili kusaidia kushikia mizigo
wakati wa usafirishaji.
Onyo
Hatari ya Kukatwa Kiungo cha Mwili
Visu vinavyozunguka zinaweza kukata mikono na miguu.
Usiwahi kubeba watu (hasa watoto) hata kama visu
vimezimwa. Wanaweza kuanguka au wakaribie mashine
wakati hautarajii.
Onyo
Hatari ya Kukosa Udhibiti na Kubingirika
Kuendesha kukiwa na mizigo yenye uzani wa zaidi ya pauni
50 (kilo 22.7) kunaweza kuwa hatari na kusababisha kukosa
udhibiti na kubingirika.
Eneo la mzigo linaweza kuinuliwa ili kufikia chumba cha injini
bila ya kuliondoa.
Kuinua eneo la mizigo
1. Inua kiti (A, Kielelezo 14).
2. Vuta juu kwa nguvu kwenye sehemu ya nyuma ya eneo la
mzigo (B, Kielelezo 14).
3. Wakati unateremsha eneo la mzigo, bonyeza chini kwa
nguvu ili ufunge sehemu ya nyuma ya eneo la mzigo katika
mahali pake ukitumia klipu za kufunga (D).
Ili kuondoa eneo la mzigo
1. Ondoa pini (C, Kielelezo 14) zinazofungilia sehemu ya
mbele ya eneo la mzigo kwenye fremu ya kifaa.
2. Vuta juu kwa nguvu kwenye sehemu ya nyuma ya eneo la
mzigo ili kuwachilia klipu za kufunga (D, Kielelezo 14).
3. Inua na uondoe eneo la mzigo kwenye kifaa.
Tahadhari
Ili kuepuka majeraha, usaidizi unahitajika wakati wa kuondoa
au kuweka eneo la mzigo.
Kuweka eneo la mzigo
1. Weka eneo la mzigo juu ya chumba cha injini, linganisha
mashimo yaliyo mbele ya eneo la mzigo pamoja na
mashimo yaliyo katika mabano ya fremu.
2. Weka pini (C, Kielelezo 14) ndani ya mashimo haya.
3. Teremsha sehemu ya nyuma ya eneo la mzigo, ukibonyeza
chini kwa nguvu ili ufunge ukitumia klipu za kufunga (D,
Kielelezo 14).
Tahadhari
Ili kuepuka majeraha, usaidizi unahitajika wakati wa kuondoa
au kuweka eneo la mzigo.
Kibadilishaji Mwangiko (Suspension)
(ikiwa upo)
Ufunganishaji wa shoki (A, Kielelezo 15 - sehemu ya mbele
imeonyeshwa, inafanana na nyuma) unaweza kubadilishwa ili
kubadilisa viwango vya uzito wa awali unaowekelewa springi.
Hili linamwezesha mwendeshaji kubinafsisha kifaa kulingana
na uzani wa mwendeshaji na hali za uendeshaji.
Uzito Mchache wa Awali:
• Uzito wa chini wa mwendeshaji
• Uendeshaji usio na msukosuko
• Mwafaka zaidi kwa maeneo tambarare
Uzito Mwingi wa Awali:
• Uzito wa juu wa mwendeshaji
• Uendeshaji wenye msukosuko zaidi
• Urahisi wa kuendesha na ustabi mzuri zaidi kwenye sehemu
zenye milima
Kubadilisha Uzito wa Awali kwenye Springi:
1. Egesha mashine kwenye eneo tambarare, bila milima. Zima
PTO, weka wenzo za kasi ya ardhini katika eneo la
kuonyesha ANZA/ EGESHA (START/ PARK), na uzime
injini.
97

Publicidad

loading