Descargar Imprimir esta página

Briggs & Stratton Victa 46 23HP Manual Del Operador página 88

Publicidad

Idiomas disponibles
  • MX

Idiomas disponibles

  • MEXICANO, página 22
6. Usiwahi kuwabeba abiria.
7. Usikate nyasi ukirudi nyuma isipokuwa kama inahitajika.
Daima tazama chini na nyuma kabla na wakati unaporudi
nyuma.
8. Usielekeze vitu vinavyotolewa kueleke kwa mtu yeyote.
Epuka kuelekeza kwenye ukuta au kizuizi, vitu
vinavyotolewa. Vitu hivyo vinaweza kurudi nyuma kuelekea
mwendeshaji. Simamisha visu unapovuka sehemu zenye
changarawe.
9. Usiendeshe mashine bila kifaa kizima cha kukamata nyasi,
kifaa cha kutoa nyasi (kibadilishaji mwelekeo), au vifaa
vingine vya usalama.
10. Punguza kasi kabla ya kugeuka.
11. Usiwahi kuwacha kifaa kilichowashwa bila kushughulikiwa.
Kila wakati zima PTO, weka breki ya kuegesha, zima injini,
na uondoe funguo kabla ya kabla ya kushuka.
12. Zima visu (PTO) wakati haukati nyasi. Zima injini na usubiri
sehemu zote zisimame kabisa kabla ya kusafisha mashine,
kuondoa kifaa cha kukamata nyasi, au kuzibua kifaa cha
kutoa nyasi.
13. Endesha mashine tu wakati wa mchana au katika taa yenye
mwangaza mzuri.
14. Usiendeshe kifaa hicho ukiwa mlevi wa pombe au dawa.
15. Jichunge na magari unaopendesha karibu na makutano ya
barabara.
16. Kuwa mwangalifu zaidi wakati wa kupakia au kupakua kifaa
hicho kwenye trela au gari.
17. Daima vaa kitu cha kulinda macho wakati wa kuendehsa
kifaa hiki.
18. Data inaonyesha kwamba waendeshaji, wenye umri wa
miaka 60 na zaidi, wanahusika katika asilimia kubwa ya
majeraha yatokanayo na vifaa vinavyoendeshwa kaw
umeme. Waendeshaji hawa wanapaswa kutathmini uwezo
wao wa kuendesha kifaa hicho kwa usalama wa kutosha
kiasi cha kujilinda wao wenyewe na wengine kutokana na
kujeruhiwa.
19. Fuata mapendekezo ya mtengenezaji ya uzito wa matairi
au uzito.
20. Kumbuka kwamba mwendeshaji anawajibikia ajali
zinazowapata watu wengine au mali.
21. Madereva wote wanafaa kutafuta na kupata maagizo ya
kitaalamu na fanisi.
22. Daima vaa viatu na suruali ngumu. Usiwahi kuendesha
ukiwa miguu tupu au umevaa malapa.
23. Kabla ya kutumia, kila wakati, kwa kutazama, kagua
kwamba visu na zana visu zipo, zimefungwa vizuri, na ni
salama. Badilisha sehemu zilizochakaa au kuharibika.
24. Ondoa viabatisho kabla ya: kuongeza mafuta, kuondoa
kiambatisho, kufanya mabadiliko (isipokuwa ikiwa
mabadiliko hayo yanaweza kutekelezwa ukiwa kwenye kiti
cha mwendeshaji).
88
25. Wakati mashine imeegeshwa, imehifadhiwa, au imeachwa
bila kushughulikiwa, punguza njia za kukata ispokuwa ikiwa
kifuli kizuri kinatumika.
26. Kabla ya kuondoka kwenye kiti cha mwendeshaji kwa ajili
ya sababu yoyote, zima PTO, weka breki za kuegesha
(ikiwa zipo), zima injini, na uondoe ufunguo.
27. Ili kupunguza hatari ya moto, weka kifaa hicho bila nyasi,
majani, na oili nyingi kupita kiasi. Usisimame au kuegesha
juu ya majani makavu, nyasi kavu, au vitu vinavyoweza
kushika moto.
28. Ni ukiukaji wa Kanuni ya Rasilimali za Umma ya California
Sehemu ya 4442 kutumia au kuendesha injini kwenye au
karibu na uwanja wowote wenye msitu, kichaka au nyasi
isipokuwa kama mfumo wa ekzosi una kishika cheche
kinachotimiza sheria zozote husika za ndani au jimbo.
Majimbo au maeneo mengine ya shirikisho huenda yakawa
na sheria sawia.
Usafirishaji na Hifadhi
1. Wakati wa kusafirisha kifaa kwenye trela wazi, hakikisha
kimeangalishwa upande wa mbele, kulingana na mwelekeo
wa safari. Ikiwa kifaa hicho kimeangalishwa upande wa
nyuma, kuinuliwa na upepo kunaweza kuku\aharibu kifaa
hiki.
2. Daima zingatia mazoea salama ya ujazaji mafuta upya na
ushughulikiaji mafuta wakati wa kujaza mafuta upya kwenye
kifaa baada ya usafirishaji au hifadhi.
3. Usiwahi kukiweka kifaa (kikiwa na mafuta) katika jengo
lililofungana lisilo na hewa safi. Mivuke ya mafuta inaweza
kusafiri hadi kwenye chanzo cha mwako (kama vile tanuu,
hita ya kuchemshia maji, n.k) na kusababisha mlipuko.
Mvuke wa mafuta pia ni sumu kwa binadamu na wanyama.
4. Daima fuata maagizo yanayotolewa na mwongozo wa injini
kuhusu maandalizi ya hifadhi kabla ya kuhifadhi kifaa hiki
kwa vipindi vifupi na virefu.
5. Daima fuata maagizo yanayotolewa na mwongozo wa injini
ya taratibu mwafaka za kuwasha kifaa wakati wa kukirejesha
kifaa hicho kwenye huduma.
6. Usiwahi kukiweka kifaa au kontena ya mafuta mahali ndani
ambapo kuna moto wazi au taa ya kibatali au stova, kama
vile hita ya kuchemshia maji. Kiache kifaa kipoe kabla ya
kukihifadhi.

Publicidad

loading