Descargar Imprimir esta página

Briggs & Stratton Victa 46 23HP Manual Del Operador página 91

Publicidad

Idiomas disponibles
  • MX

Idiomas disponibles

  • MEXICANO, página 22
11. Usiondoe chujio la mafuta injini ikiwa moto kwani petroli
iliyomwagika inaweza kuwaka moto. Usitawanye vibanio
vya laini ya mafuta mbali zaidi kuliko inavyohitajika.
Hakikisha vibanio vinakamata mabomba ya mafuta kwa
uthabiti juu ya chujio baada ya kuwekwa.
12. Usitumie petroli ambayo ina METHANOL, gasoholi iliyo na
ETHANOL zaidi ya asilimia 10%, nyongeza za petroli, au
gesi nyeupe kwa sababu inaweza kupelekea uharibifu wa
mfumo wa injini/mafuta.
13. Ikiwa mafuta yote ni lazima yatolewe kwenye tangi la
mafuta, yanafaa kumwagiwa nje ya nyumba.
14. Badilisha vipunguzaji kelele/mafla zenye dosari.
15. Tumia tu sehemu za kubadilishia zilizoidhinishwa na
kiwanda wakati wa kufanya ukarabati.
16. Daima tii maagizo ya kiwandani kwenye mipangilio na
mabadiliko yote.
17. Ni maeneo ya huduma yaliyoidhinishwa tu yanafaa
kutumiwa kwa ajili ya huduma kubwa na mahitaji ya
ukarabati.
18. Usiwahi jaribu kufanyia kifaa hiki ukarabati mkubwa
isipokuwa uwe umepitia mafunzo mwafaka. taratibu
zisizofaa za huduma zinaweza kupelekea uendeshaji hatari,
uharibifu wa vifaa na kubatilishwa kwa hakikisho la
mtengenezaji.
19. Kwenye mashine za kukata nyasi zenye visu vingi, kuwa
mwangalifu kwani kuzungusha kisu kimoja kunaweza
kusababisha visu vingine vizunguke.
20. Usibadilishe mipangilio ya kidhibiti injini au kuendesha injini
kwa kasi ya juu kupita kiasi. Kuendesha injini kwa kasi ya
juu kupita kiasi kunaweza kuongeza hatari ya mtu kujijeruhi
mwenyewe.
21. Zima viambatisho vya kuendeshea, zima injini, ondoa
ufunguo, na utenganishe waya za plagi ya spaki: kuzibua
vizibo na chuti, kutekeleza huduma, kugonga kitu, au ikiwa
kifaa kinatetemeka kwa namna isiyo ya kawaida. Baada ya
kugonga kitu, kagua mashine kama kuna uharibifu na
ufanye ukarabati kabla ya kuiwasha tena na kuendesha
kifaa hicho.
22. Usiwahi kuweka mikono karibu na sehemu zinazosonga,
kama vile viyoyozi vya kupoesha pampu ya haidro, wakati
mashine imewashwa. (viyoyozi vya pampu ya haidro kwa
kawaida viko juu ya ekseli ya kuendeshea).
23. Vifaa vyenye pampu za haidroliki, mabomba, au mota:
ONYO: Mafuta ya haidroliki yanayovuja chini ya shinikizo
yanaweza kuwa na nguvu ya kutosha kupenyeza ngozi na
kusababisha jeraha. Mafuta ya kigeni yakiingia ngozini ni
lazima ni lazima yaondolewe kwa kufanyiwa upasuaji ndani
ya saa chache na daktari ambaye anafahamu aina hii ya
jeraha au eneo hilo linaweza kuoza. Weka mwili na mikono
mbali na tundu za pini au ncha ambazo zinavuja mafuta ya
haidroliki chini ya shinikizo kubwa. Tumia karatasi au
kadibodi, na sio mikono, ili kutafuta maeneo yanayovuja.
Hakikisha kwamba miunganisho yote ya mafuta ya haidroliki
imekazwa na mabomba yote ya haidroliki ipo katika hali
nzuri kabla ya kuweka shinikizo kwenye mfumo. Uvujaji
ukitokea, hakikisha kifaa kimefanyiwa huduma maramoja
na muuzaji aliyeidhinishwa.
24. ONYO: Kifaa cha nishati kilichohifadhiwa. Kufungua springi
vibaya kunaweza kusababisha mtu kijijeruhi vibaya sana.
Springi zinafaa ziondolewe na fundi aliyeidhinishwa.
25. Miundo imetayarishwa na radieta ya injini: ONYO: Kifaa
cha nishati kilichohifadhiwa. Ili kuzuia jeraha mbaya la
mwilini kutokana na kipoeshaji moto au mlipuko wa mvuke,
usiwahi jaribu kuondoa kifuniko cha radieta wakati injini
imewashwa. Zima injini na subiri mpaka ipoe. Hata baada
ya hapo, kuwa mwangalifu zaidi unapoondoa kifuniko.
Lebo za Usalama na Maagizo
Kabla ya kuendesha kifaa chako, soma na uelewe lebo za
usalama na maagizo (linganisha Kielelezo 1 na jedwali lililo
hapa chini). Tahadhari, onyo, na maagizo ni kwa ajili ya usalama
wako. Ili uepuke majeraha ya mwili au kuharibu kwa kifaa hiki,
elewa na ufuate lebo zote.
Lebo zozote za usalama au maagizo zikichakaa au kuharibika,
na haziwezi kusomeka, agiza lebo za kubadilishia kutoka kwa
muuzaji wako.
A
Lebo, Kibadilishaji
Ufuatiliaji
Na. ya Sehemu
1759724
B
Lebo, Usalama
Mkuu (Miundo ya
Nje ya ANSI)
Na. ya Sehemu
1759648
C
Lebo, Urefu wa
Kukatia
Na. ya Sehemu
1759253
D
Lebo, Kasi ya Injini
(Choki)
Na. ya Sehemu
7105770
91

Publicidad

loading