Descargar Imprimir esta página

Briggs & Stratton Victa 46 23HP Manual Del Operador página 99

Publicidad

Idiomas disponibles
  • MX

Idiomas disponibles

  • MEXICANO, página 22
Kagua utendaji salama wa visu vya mashine ya kukatia nyasi.
Tazama Majaribio ya Mfumo Salama wa Intaloki. Kisu kinafaa
kuwacha kuzunguka ndani ya sekunde 5 au chache baada ya
kusogeza kidhibiti cha kisu hadi eneo linaloonyesha ZIMA (OFF).
Udumishaji Betri
Onyo
Hatari ya Mlipuko na Moto
Wakati wa kuondoa au kuweka kebo za betri, tengenisha kebo
hasi (negative) KWANZA na kisha iunganishe tena ikiwa ya
MWISHO. Ikikosa kufanyika kwa mpangilio huu, kichwa
chanya (positive) kinaweza kupata shoti kwenye fremu na
zana.
Kusafisha Betri Na Kebo
1. Tenganisha kebo na betri, kebo hasi (negetive) kwanza (B,
Kielelezo 17).
2. Safisha ncha za betri na ncha za kebo na brashi yenye
waya mpaka zing'ae.
3. Ingiza betri tena na uweke kebo za betri tena, kebo chanya
(positive) kwanza (A, 17).
4. Paka ncha za betri na kebo mafuta ya mgando au upake
grisi isiyopitisha umeme.
5. Hakikisha unabadilisha kifuniko kwenye kichwa chanya
(positive) (A, Kielelezo 17.
Kuchaji Betri
Onyo
Hatari ya Mlipuko na Moto
Weka moto wazi na cheche mbali na betri; gesi zinazotoka
kwenye betri zina uwezekano mkubwa sana wa kulipuka.
Weka betri kwenye hewa safi wakati wa kuichaji.
Betri iliyokufa au ambayo ni dhaifu sana kuwasha injini inaweza
kusababisha dosari katika mfumo wa kuchaji au kijenzi kingine
cha umeme. Ikiwa kuna shaka yoyote kuhusu sababu ya tatizo,
mtembelee muuzaji wako.
Ili kuchaji betri, fuata maelekezo yaliyotolewa na mtengenezaji
kifaa cha kuchaji betri na vilevile onyo zote zilizojumuishwa
katika sehemu ya sehemu ya Usalama wa Mwendeshaji ya
mwongozo huu. Chaji betri hadi lijae kabisa. Usichaji katika
kiwango kikubwa zaidi kuliko 10 amps.
Urekebishaji Kiti na Wenzo za Kasi ya
Ardhini
Kiti na wenzo za kasi ya ardhini zinafaa kurekebishwa ili wenzo
za kasi ya ardhini ziweze kusongezwa kati ya msongo wake
kamili bila kugusa miguu ya mwendeshaji.
Urekebishaji Kiti
1. Inua kiti.
2. Legeza sehemu za urekebishaji (A au B, Kielelezo 18,
kulingana na aina ya kiti) chini ya eneo la kiti.
3. Telezesha kiti mbele na nyuma kwenye nafasi unayotaka.
4. Kaza sehemu za kushikilia hadi 80 lb-in (9 Nm).
Usongezaji Wenzo za Kasi ya Ardhini
1. Legeza sehemu zinazoshikilia wenzo za kasi ya ardhini (A,
Kielelezo 19) ili kusongeza wenzo mbele na nyuma.
2. Ondoa sehemu zilizoshikilia ili uinue au uteremshe wenzo.
3. Kila wakati hakikisha kusongeza wenzo zote mbili ili
zilingane (B, Kielelezo 19).
4. Baada ya usongezaji kukamilika, kaza sehemu za kushikilia
hadi kwenye 13 lb-ft (18 Nm).
Ubadilishaji wa Mizani ya Kasi (Ufuatiliaji)
Ikiwa kifaa kinaelekea kulia au kushoto wakati wenzo za kasi
ya ardhini zipo katika eneo la mbele kabisa, kasi ya juu zaidi
ya kila moja ya wenzo hizi inaweza kusawazishwa. Badilisha
tu kasi ya gurudumu linalokwenda haraka zaidi.
1. Kaza kirungu (A, Kielelezo 20) ya gurudumu lenye kasi zaidi
kwa kuzungusha kwa kongeza mizunguko ya nusu
(mwenendo wa saa) mpaka kifaa kiende (fuata) sambamba.
Onyo
Hatari ya Uendeshaji Usio Salama
USIBADILISHE kifaa ili kuongeza kasi jumla ya kwenda
mbele au kurudi nyuma kuliko kilivyotengenezwa.
Kubadilisha Oili
Oili iliyotumika ni bidhaa taka na hatari na ni lazima itupwe kwa
njia mwafaka. Usitupe pamoja na taka za nyumbani. Wasiliana
na mamlaka yako ya ndani, kituo cha huduma au muuzaji ili
kupata zana salama za kutupa/kutumia tena.
Kumwaga Oili
1. Injini ikiwa imezimwa lakini bado ina joto, tenganisha waya
ya plagi ya spaki (A, Kielelezo 21) na uiweke mbali na plagi
ya spaki.
2. Ondoa kifaa cha kupima kiwango cha oili (B, Kielelezo 21).
Kifuniko cha Tundu la Umwagaji Oili wa Kawaida
1. Ondoa kifuniko cha tundu la umwagaji oili (C, Kielelezo 21).
Mwaga oili katika kontena iliyoidhinishwa.
2. Baada ya oili kumwagwa, weka na ukaze kifuniko cha tundu
la umwagaji oili.
Umwagaji Oili kwa Haraka wa Hiari
99

Publicidad

loading