Descargar Imprimir esta página

Briggs & Stratton Victa 46 23HP Manual Del Operador página 87

Publicidad

Idiomas disponibles
  • MX

Idiomas disponibles

  • MEXICANO, página 22
mara moja ikiwa mfumo hautapita majaribio yote ya kiusalama
yaliyo katika mwongozo huu.
Vitu Vinavyorushwa
Kifaa hiki kina visu vya kukatia nyasi vinavyozunguka. Visu hivi
vinaweza kuinua na kurusha vifusi ambavyo vinaweza kumjeruhi
mtu aliyesimama kando vibaya sana. Hakikisha umesafisha
eneo linalokatwa nyasi KABLA ya kuanza kukata nyasi.
Usiendeshe kifaa hiki bila kifaa kizima cha kukamata nyasi,
kifaa cha kutoa nyasi (kibadilishaji mwelekeo), au vifaa vingine
vya usalama.
Pia, usimruhusu mtu yeyote katika eneo hilo wakati kifaa
kinaendeshwa! Mtu akiingia kwenye eneo hilo, zima kifaa mara
moja mpaka atakapoondoka.
Mafuta na Udumishaji
Daima zima swichi zote, zima injini, na uondoe ufunguo kabla
ya kufanya usafi, kuongeza mafuta, au huduma yoyote.
Petroli na mivuke yake zinaweza kushika moto haraka sana.
Usivute sigara ukiwa unaendesha kifaa au unapoongeza mafuta.
Usiongeze mafuta wakati injini ipo moto au inaguruma. Ruhusu
injini ipowe kwa angalau dakika 3 kabla ya kuongeza mafuta.
Usiongeze mafuta ndani ya nyumba, katika trela lililofunikwa,
gereji, au maeneo mingine yoyote yaliyofungwa ambayo hayana
hewa safi. Petroli iliyomwagika inafaa kusafishwa kwa haraka
na kabla uanze kuendesha kifaa.
Petroli inafaa kuhifadhiwa katika kontena zilizofungwa vizuri
zilizoidhinishwa kuhifadhia mafuta.
Udumishaji mwafaka ni muhimu kwa usalama na utendakazi
wa kifaa chako. Weka kifaa bila nyasi, majani na oili nyingi
kupita kiasi. Hakikisha unafanya taratibu za udumishaji
zilizoorodheshwa katika mwongozo huu, hasa mara kwa mara
kujaribu mifumo ya usalama.
Kuta za Pembeni, Maeneo Yaliyoshuka Ghafla,
na Maji,
Kuta za pembeni na maeneo yaliyoshuka ghafla, na maji ni
hatari zinazotokea mara nyingi. Kaa mbali na hatari hizi kwa
kuacha nafasi sawia na ya mashine mbili za kukatia nyasi
unapotumia mashine ya kushika kwa mkono au ya kusukuma.
Magurudumu kuanguka upande ule mwingine wa kuta za
pembeni, mitaro au ndani ya maji kunaweza kusababisha kifaa
kubingirika, jambo linaloweza kupelekea jeraha mbaya, kifo au
kufa maji.
Maagizo ya Usalama wa Uendeshaji Jumla
Onyo
Soma kanuni hizi za usalama na uzifuate kwa makini. Kukosa
kutii kanuni hizi kunaweza kupelekea kushindwa kudhibiti
kifaa, jeraha mbaya sana la kimwili au kifo chako, au kwa
watu waliosimama kando, au hasara kwa mali au kifaa. Deki
hii ya mashine ya kukatia nyasi ina uwezo wa kukata
mikono na miguu na kurusha vitu. Alama ya pembe tatu
katika maandishi inamaanisha tahadhari au onyo muhimu
ambazo ni lazima zifuatwe.
Uendeshaji kwa Jumla
1. Soma, uelewa, na ufuate maagizo yote katika mwongozo
na kwenye kifaa kabla ya kuanza.
2. Usiweka mikono au miguu karibu na sehemu zinazozunguka
au chini ya mashine. Kaa mbali na mwanya unaotoa nyasi
nyakati zote.
3. Ruhusu tu watu wazima wanaowajibika, ambao
wanafahamu maagizo, kuendesha kifaa hicho (sheria za
ndani zinaweza kuwekea kikwazo umri wa mwendeshaji).
4. Safisha eneo kutokana na vifaa kama vile mawe, vitu vya
watoto kuchezea, waya, n.k., ambavyo vinaweza kuinuliwa
na kurushwa na visu vya kifaa.
5. Hakikisha eneo hilo halina watu wengine kabla ya kukata
nyasi. Simamisha kifaa mtu yeyote akiiingia eneo hilo.
87

Publicidad

loading