muhimu sana ili kunufaika zaidi na mashine ya kukatia nyasi
ya kugeukia mahali pamoja.
Tafuta eneo laini, tambarare la uwanja wako wenye nyasi,
ambalo lina nafasi tosha ya kuendeshea. Safisha eneo kwa
kuondoa vitu, watu, na wanyama kabla ya kuanza. Endesha
kifaa kwa kasi wastani wakati wa kipindi hiki cha mazoezi
(DAIMA endesha kwa kasi kamili wakati wa kukata nyasi), na
ugeuke polepole ili kuzuia magurudumu kuchimbua na kuharibu
uwanja wako.
Tunapendekeza uanzie na utaratibu wa Mwendo Laini na kisha
uendelee na mienendo ya kuenda mbele, kurudi nyuma, na
kugeuka.
Mwendo Laini
Vidhibiti vya wenzo vya kifaa cha kugeukia mahali pamoja
zinafanya kazi.
Njia BORA zaidi ya kutumia wenzo za kudhibiti kasi ya ardhini
ipo katika hatua tatu — kama inavyoonyeshwa katika Kielelezo
6.
KWANZA weka mikono yako kwenye wenzo kama
inavyoonyeshwa.
PILI, ili kwenda mbele kwa utaratibu sukuma wenzo mbele
ukitumia viganja vyako.
TATU, ili kuongeza kasi sogeza wenzo mbele zaidi. Ili
kupunguza mwendo kwa utaratibu, sogeza wenzo polepole
kuelekea katikati.
Uendeshaji wa Msingi
Mazoezi ya Kwenda Mbele
Kwa utaratibu songeza wenzo zote mbili za kasi ya ardhini —
kwa usawa KWENDA MBELE kutoka katikati. Punguza kasi na
urudie tena.
KUMBUKA: Kwenda mbele bila kuyumbayumba kunahitaji
mazoezi. Ikiwa yahitajika, kasi ya juu inaweza kubadilishwa
kulingana na usawazishaji — tazama Ubadilishaji Usawazishaji
Kasi katika sehemu ya Ubadilishaji karibu na upande wa nyuma
wa mwongozo huu.
Mazoezi ya Kurudi Nyuma
TAZAMA CHINI na NYUMA, kisha kwa utaratibu songeza wenzo
zote mbili za kasi ya ardhini kwa usawa kwenda NYUMA kutoka
katikati. Punguza kasi na urudie tena.
KUMBUKA: Fanya mazoezi ya kurudi nyuma kwa dakika kadhaa
kabla ya kujaribu kufanya hivyo karibu na vitu. Kifaa hugeuka
haraka sana kinaporudi nyuma na vilevile kinapoenda mbele,
na kurudi nyuma bila kuyumbayumba kunahitaji mazoezi.
Fanya Mazoezi ya Kupiga Kona
Wakati wa kwenda mbele ruhusu wenzo moja kurudi nyuma
kwa utaratibu kuelekea katikati. Rudia mara kadhaa.
KUMBUKA: Ili kuzuia kuzungukia moja kwa moja kwenye matairi
yaliyosimama, ni bora kufanya hivyo huku yakienda mbele
angalau polepole.
96
Fanya Mazoezi ya Kugeukia Mahali Pamoja
Ili kugeukia mahali ulipo, "Kugeukia Mahali Pamoja," kwa
utaratibu songeza mbele wenzo moja wa kasi ya ardhini kutoka
katikati na usongeze wenzo moja nyuma kutoka katikati kwa
wakati mmoja. Rudia mara kadhaa.
KUMBUKA: Kubadilisha kiwango ambacho kila wenzo
umevutwa—mbele au nyuma, kunabadilisha "eneo la kugeukia"
unalogeukia.
Uendeshaji wa Hali ya Juu
Kugeukia Mahali Pamoja katika Mwisho wa Mstari
Uwezo wa kipekee wa kifaa chako wa kugeukia mahali pamoja
unakuwezesha kugeuka mwishoni mwa safu ya kukata badala
ya kusimama na kugeusha kifaa kabla ya kuanza safu mpya.
Kwa mfano, ili kugeukia mahali pamoja kuelekea kushoto
mwishoni mwa safu:
1. Punguza kasi mwishoni mwa safu.
2. Songeza wenzo wa KULIA wa kudhibiti kasi ya ardhini
mbele kidogo huku ukisongeza wenzo wa KUSHOTO wa
kudhibiti kasi ya ardhini nyuma kuelekea katikati na kisha
nyuma kidogo kutoka katikati.
3. Anza tena kukata nyasi kwenda mbele.
Mbinu hii inageuza kifaa kuelekea KUSHOTO na kidogo
hupishanisha safu iliyokatwa —kwa kuondoa hitaji la kurudi
nyuma na kukata upya nyasi ambazo hazikukatwa.
Unavyokuwa pata ujuzi na kuwa mzoefu zaidi katika kuendesha
kifaa cha Kugeukia Mahali Pamoja, utajifunza mbinu nyingi zaidi
ambazo zitafanya muda wako wa kukata nyasi kuwa rahisi zaidi
na wa raha zaidi.
Kumbuka, unavyofanya mazoezi zaidi, ndivyo
utakavyoweza kudhibiti kifaa cha Kugeukia Mahali Pamoja
zaidi!
Kuunganisha Trela
Funga trela ukitumia pini ya klevisi yenye ukubwa unaofaa (A,
Kielelezo 12) na klipu (B). Tazama Usalama wa Mwendeshaji
ili kupata maelezo zaidi ya usalama kuhusu trela na uvutaji.
Onyo
Hatari ya Uvutaji
Mizigo inayovutwa inaweza kuwa hatari na inaweza
kusababisha ushindwe kudhibiti kifaa kwenye miteremko.
• Jumla ya juu zaidi ya uzito (trela na mzigo) wa trela ni
pauni 200 (kilo 91).
• Usiendeshe katika miteremko unaozidi digrii 5.
• Punguza kasi na uwe makini zaidi kwenye miteremko.
Ubadilishaji Urefu wa Kukata
Pedali ya kubadilisha urefu wa kukata inabadilisha urefu wa
kukata wa mashine ya kukatia nyasi. Tazama Maelezo ya wigo
wa ubadilishaji urefu wa kukata.